Ndio term limit ni muhimu.
Hiki kitu Chadema huwa hawakizungumzi mara kwa mara?
Hata Mbowe ashakisema, madaraka yana tabia ya kulevya.
Mbowe kafanya makubwa kwa miaka 21 ila kwa sasa apumzike apatikane kiongozi mpya kuna vitu amefeli kwa miaka ya karibuni.
Chama kilipoteza wabunge kwa hila za Magufuli 2020 akaweka azimio bila tume huru na katiba mpya hakuna kushiriki uchaguzi mwingine.
Ajabu 2024 chama kimeingia kushiriki igizo lile tena bila hivyo vitu viwili na kimeshindwa [hili halihitaji shahada kujua kingeshindwa ] kutokana na muundo wa tume inavyopatikana na kukosekana kwa katiba inayowajibisha watawala.
Sasa unafikiri kwa hali iliyopo si kitashiriki tena upuuzi wa 2025 halafu nyimbo za "tumeibiwa" ziendelee humu , yaani hujifunzi mara 3 , 2005 uibiwe, 2015 uibiwe, 2020 uibiwe na bado umo tu?
View attachment 3184068