Nashindwa kuamini hiki ninachokisoma kuhusu haya makato ya LUKU

Nashindwa kuamini hiki ninachokisoma kuhusu haya makato ya LUKU

Mimi nimenunua umeme wa 50,000 sasa hivi, ujumbe wangu huu hapa

Cost 39,344.27
VAT 18% 7,081.96
EWURA 1% 393.44
REA 3% 1,180.33
Debt Collected 2,000.00
TOTAL 50,000.00 20/08/21 22:19

Yaani nimepata umeme wa 39,344 tu, elfu 10,656 ni jumla ya makato,,,, makato ya kununua umeme ni makubwa zaidi kama tozo ya kutuma hela....... hapo ukumbuke, nimenunua kwa simu, tigopesa wamenikata 1,000 ya zaidi....... hii nchi inajitafutia laana, hela ya dhuluma haijengagi hata siku moja
Bado moto wa sufuria la tozo la line za simu na vocha linazidi kuchochewa wallah,masaa machache yajayo na lenyewe linaepuliwa 🤣 🤣 🤣
 
Muda huu baada ya kuona huu uzi , nimetest kununua units za miatano (chini ya kiwango chao wanachotaka 1000tsh), ngoma inagoma kabisa wanadai eti "tender more money😝"

Nimemwambia mke wangu ajaribu na yeye wanamuandikia hivyo.

Nilichogundua ni kwamba hii tozo ya luku atakatwa mtu yoyote bila kujali anamiliki nyumba au laa

Huu ni upuuzi mkubwa sana,yani hawaridhiki na hela za miamala na mafuta sasa wamehamia kwenye LUKU, na kibaya zaidi hela zetu zinatumiwa na mpumbavu mmoja kufanya ziara za kijinga tu, kutwa anazunguka na misafara kwenye nchi za watu kijinga kijinga tu.

Muda si mrefu watatuletea na Tozo za pumbu Sasa🤒.
Kumekucha 🤣🤣🤣🤣
 
Si walisema wanakata Buku 1 kwa mwezi ,why wakate elfu 2? Mimi natumia solar huku porini so sijui hayo makato.
Kuna wakati utafika watu wataanza kuulizwa kwanini hununui Luku ili kulipia deni lako.

Dawa yao kuweka mita halafu hununui umeme unafunga solar.

Kuhusu miamala ya simu naona mwezi wa kwanza tu salamu wanazo.

Nina imani baada ya muda fulani makampuni ya simu yatafunga biashara zao na kwenda kwingine.

Sijawahi kuona serikali yenye tamaa na wavivu kifikiri kama hii.

Unalazimisha kuvuna usipopanda. Tozo na Kodi tu ndicho wanajua. Hadi kodi zinatozwa zaidi ya mara moja kwa huduma/ bidhaa moja.
 
Vipi ule Uhuru wa kuongea mnao,mlitaka kuongea bila sababu Sasa sababu mnayo semeni

USSR
 
Ndo akili zako zumekutuma huko?
President Samia hana tatizo kabisa, tatizo lilianza kwenye kupenda sifa za kijinga jinga hivi,zitatugharimu kwa miaka mingi sanaaa
Hivi mbona huwa mnapenda kumkingia kifua kana kwamba hahusiki na chochote ndani ya serikali?

Yaani katika hizi tozo unataka kusema SSH hahusiki wakati baadhi ya makusanyo yamepelekwa Zenji,?

Acheni kumlambalamba,ukweli ni kwamba amefeli sana kitu pekee anachoweza ni kusafiri.
 
Habari za jioni wateja wetu.
Kuanzia leo sheria ya kulipa kodi ya jengo kupitia manunuzi ya umeme imeanza kutekelezwa.
Kwa hiyo mteja akinunua umeme atakatwa shs 2000 ikiwa ni kodi ya Jengo inayodaiwa na Tra.kodi hii ilitakiwa kuanza tarehe 01.07.2021 lakini imeanza leo.
Hivyo mteja akinunua umeme kuanzila leo atakatwa shs 2000 ambayo ni kodi ya jengo ya miezi miwili ya (Julai na Agasti.)
Tunawashauri wateja wetu wanunue umeme wa kuanzia 3000 ili walipie kodi ya jengo 2000 na shs 1000 wapate umeme.
Imetolewa na:
Ofisi ya uhusiano na huduma kwa wateja
TANESCO
20.08.2021

Copy and paste
Wanatuchanganyia habari hawa jamaa. Walisema wataanza tar 20/08 na sio tar 01/07.
 
Muda huu baada ya kuona huu uzi , nimetest kununua units za miatano (chini ya kiwango chao wanachotaka 1000tsh), ngoma inagoma kabisa wanadai eti "tender more money[emoji13]"

Nimemwambia mke wangu ajaribu na yeye wanamuandikia hivyo.

Nilichogundua ni kwamba hii tozo ya luku atakatwa mtu yoyote bila kujali anamiliki nyumba au laa

Huu ni upuuzi mkubwa sana,yani hawaridhiki na hela za miamala na mafuta sasa wamehamia kwenye LUKU, na kibaya zaidi hela zetu zinatumiwa na mpumbavu mmoja kufanya ziara za kijinga tu, kutwa anazunguka na misafara kwenye nchi za watu kijinga kijinga tu.

Muda si mrefu watatuletea na Tozo za pumbu Sasa[emoji855].
Tutulie yule wa awamu ya 5 alikuwa hazunguki kwa ushamba na kutojua lugha, hivyo nchi ikawa haina mahusiano na nchi zingine.
Wa mjini acha afungue nchi tutamlipia na convoy yake
 
Marehemu Magufuli akiwa hai alikuwa anasema anawapigania wanyonge, mkawa mnamcheka na kumdharau huku mkimkebehi kwa kila namna.

Alipoapishwa huyo Madam wenu mkaanza kushangilia na kumsifia kila siku. Sasa hivi amefikisha miezi 5 tu mmeanza kuisoma namba na bado ana miaka 4 na miezi 7 ya kukaa Ikulu.

Magufuli aliwaambia "mtamkumbuka".

Au nasema uongo ndugu zangu 😂😂😂
 
Hivi mbona huwa mnapenda kumkingia kifua kana kwamba hahusiki na chochote ndani ya serikali?

Yaani katika hizi tozo unataka kusema SSH hahusiki wakati baadhi ya makusanyo yamepelekwa Zenji,?

Acheni kumlambalamba,ukweli ni kwamba amefeli sana kitu pekee anachoweza ni kusafiri.
Mkuu hivi ni kweli pesa inakwenda zanji sio chato tena

USSR
 
Back
Top Bottom