Nashindwa kuamini hiki ninachokisoma kuhusu haya makato ya LUKU

Bado moto wa sufuria la tozo la line za simu na vocha linazidi kuchochewa wallah,masaa machache yajayo na lenyewe linaepuliwa 🀣 🀣 🀣
 
Kumekucha 🀣🀣🀣🀣
 
Si walisema wanakata Buku 1 kwa mwezi ,why wakate elfu 2? Mimi natumia solar huku porini so sijui hayo makato.
Kuna wakati utafika watu wataanza kuulizwa kwanini hununui Luku ili kulipia deni lako.

Dawa yao kuweka mita halafu hununui umeme unafunga solar.

Kuhusu miamala ya simu naona mwezi wa kwanza tu salamu wanazo.

Nina imani baada ya muda fulani makampuni ya simu yatafunga biashara zao na kwenda kwingine.

Sijawahi kuona serikali yenye tamaa na wavivu kifikiri kama hii.

Unalazimisha kuvuna usipopanda. Tozo na Kodi tu ndicho wanajua. Hadi kodi zinatozwa zaidi ya mara moja kwa huduma/ bidhaa moja.
 
Vipi ule Uhuru wa kuongea mnao,mlitaka kuongea bila sababu Sasa sababu mnayo semeni

USSR
 
Ndo akili zako zumekutuma huko?
President Samia hana tatizo kabisa, tatizo lilianza kwenye kupenda sifa za kijinga jinga hivi,zitatugharimu kwa miaka mingi sanaaa
Hivi mbona huwa mnapenda kumkingia kifua kana kwamba hahusiki na chochote ndani ya serikali?

Yaani katika hizi tozo unataka kusema SSH hahusiki wakati baadhi ya makusanyo yamepelekwa Zenji,?

Acheni kumlambalamba,ukweli ni kwamba amefeli sana kitu pekee anachoweza ni kusafiri.
 
Wanatuchanganyia habari hawa jamaa. Walisema wataanza tar 20/08 na sio tar 01/07.
 
Tutulie yule wa awamu ya 5 alikuwa hazunguki kwa ushamba na kutojua lugha, hivyo nchi ikawa haina mahusiano na nchi zingine.
Wa mjini acha afungue nchi tutamlipia na convoy yake
 
Marehemu Magufuli akiwa hai alikuwa anasema anawapigania wanyonge, mkawa mnamcheka na kumdharau huku mkimkebehi kwa kila namna.

Alipoapishwa huyo Madam wenu mkaanza kushangilia na kumsifia kila siku. Sasa hivi amefikisha miezi 5 tu mmeanza kuisoma namba na bado ana miaka 4 na miezi 7 ya kukaa Ikulu.

Magufuli aliwaambia "mtamkumbuka".

Au nasema uongo ndugu zangu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu hivi ni kweli pesa inakwenda zanji sio chato tena

USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…