Nashindwa kumuelewa mume wangu, nikimkosea anaishia kulia

Sasa dada umempata mume kama huyo halafu bado unachepuka? Ila saa nyingine wanawake sijui tunatakaga tupewe nini yaani!
 
Siku akichoka na Huo upuuzi wako basi jua baya linaweza kukufika hata mauti pia, Kuwa makini na Mumeo acha mapepe, Uliolewa kwa Hiari basi Jitulize

Uvumilivu unapofika kikomo basi jua lolote linaweza kutokea hapo
 
Dada ushukuru sana .
Ingekua mm una manundu na mwili mzima unakuuma na sku ya pili kikao cha familia kikubwaa
 
Mtafutie kazi ya kulia kwenye vikundi ya kulia msibani
 
Kwan wewe unahisi unajielewa?
 
Alafu unavyojisifia unadhani sifa.. yaani unajua ninavyokutamani shukuru mi sio huyo jamaa.
 
Kulia ni moja Kati ya njia zakutoa/ kupunguza sumu (maumivu ) moyoni. Lakini pia kulia ni miongoni mwa aina za hasira. Aina hiyo ya hasira ni mbaya sana mana huwa ni kuzuwia uchungu usitoke nje na kuishia ndani kwa ndani. Ko siku atakapo ruhusu hasira zikatoka nje sijui Nani atamuamua
 
Mmmh utauwawa siku si nyingi 😂
 
Huu ndo muda sahihi wa kuaga ndugu zako na kuchagua sehem ya kuzikwa huyo jamaa anakukusanyia makosa hukum ataitoa siku 1 usifikiri et ndo atalia hivyo hivyo had mzeeke wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…