Grahams
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 16,096
- 49,651
Depression is real
Kwa kutambua hilo, Mungu ametupa namna ya kuzishinda hali zote ngumu.
Imagine wewe na Mimi tungekuwa Ayubu, tunapitishwa kwenye yale majaribu, kweli tungeweza kuyastahimili ama ndiyo tungejiua.
Hebu soma, Zaburi 142:3
Ninapokaribia kukata tamaa kabisa, yeye (Mungu) yupo, anajua mwenendo wangu.Tujifunze kupokea nyakati zote kwenye maisha yetu.
Wakati wewe unakula Pizza pale Pizza Hut, kuna mwenzio hajui atakula nini Mchana huu wala Usiku.
Wakati wewe unafurahia kutimiza Miaka 28,30,35,40 n.k ujue kuna mwenzio anatimiza Umri huo akiwa Kaburini.
Wakati wewe unalalamika kupata Supplementary 2 ama 1 kuna mwenzio aliishia darasa la 7 kwa kushindwa kufauru kwenda Sekondari.
Wakati wewe unafurahia kuingia kwenye nyumba yako ulianza kuijenga Miaka 2 ama 3 iliyopita ujue kuna mwenzio amefukuzwa na Baba Mwenye nyumba kwa kushindwa kulipa Kodi ya shilingi 240,000 ambayo ni kodi ya miezi 6.
Mungu ni mwema kila wakati 🙏🙏🙏🙏