Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Hiyo katiba ya china umeshaisoma?maana na yenyewe wamekua wakiifanyia maboresho kila baada ya miaka kadhaa.sasa jiulize kwanini wanafanya hivyo kama maendeleo yao hayachagizwi na uwepo wa katiba bora.
 
Nani kasema anataka katiba mpya ili kuondoa umasikini? Watu wengine mpaka kero, alafu unakuta jitu lenyewe ni jitu zima lakini la hovyo sana.
Kwako katiba mpya ina impact gani?
 
Akija jiwe mwingine hawa wote wanaobeza katiba mpya watalia na kusaga meno.
Ni kweli kwamba kwa katiba hii ya sasa tutakuja kupata rais wa hovyo ambaye Magufuli hataona ndani.

Eti katiba ya nchi inakuwa na ibara fulani fulani zinazosema "Kama ikimpendezea Mheshimiwa Rais". Hiyo sio katiba.. ni waraka fulani ya kihuni tu.
 
Hakuna kitu kinaogopwa na CCM hapa duniani kama katiba mpya ya Tanzania.
 
Mkuu, ili uwe mwanajeshi unahitaji upite wapi na wapi, au unahitaji upewe amri pekee??

Hao achana nao, kwani wao wanapitia mafunzo kwanza kabla ya kila kitu

Sasa wewe, unaenda kudai tu katiba bila ya kuwafundisha wananchi namna ya kuilinda hiyo katiba, na ndiyo maana hatutapata anayewajibika kuilinda kwa sababu kila mmoja anajua hiyo katiba ni ya watu fulani na fulani
 
Tatizo linaanzia ktk katiba yenyewe, maandamano na mahakama ndo kiboko ya kuwawajibisha wavunja katiba, haya tumeeandamana polisi hao wanatumwa na mamlaka ya juu kutawanya maandamano kwa silaha za moto, maaskari na mahakama hawawezi kukataa maagizo ya mamlaka toka juu make ndo inayomteua na kumfukuza, endapo katiba itamhakikishia security hawa maafisa pindi wakikataa maagizo batili toka juu, hakika wavunja katiba dawa yao ni maandamano yasiyo na kikomo mpaka waachie ngazi.
 
Tunawetaka katiba mpya lakini sio hiyo wanayoitaka wao ya kuwaingiza ikulu kufanya biashara
Huwa nahisi wewe ni ccm lakini hapa umeandika tofauti na ccm wenzako wanaodhani katiba ni kwaajili ya chadema.
Tudai katiba kwaajili ya nchi ,vyama vipambane vyenyewe kufuata matakwa ya wananchi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo katiba ya china umeshaisoma?maana na yenyewe wamekua wakiifanyia maboresho kila baada ya miaka kadhaa.sasa jiulize kwanini wanafanya hivyo kama maendeleo yao hayachagizwi na uwepo wa katiba bora.
Hivi katiba itakataza viongozi wa nchi kuwapigia magoti wachina na wazungu?
 
Hii kwangu ndio hoja ya msingi! Unashabikia katiba ili Mbowe anufaike na kumuingiza Lissu madarakani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ni akili au matope hayo!
Jamaa nakuonaga una akili kumbe na wewe ni pimbi tu, haya hata kama sio lissu au mbowe kwanini asishabikie katiba itakayotoa fursa kwa mtz yoyote kupata madaraka kwa njia halali na ya wazi hata kama atakuwa ni yeye mwenyewe au babu yake au Dada yako?
 

..kuna nchi zimekuwa zikihubiri HAKI na wananchi wao wana mwamko wa kulinda katiba.

..hapa Tz tumekuwa tukihubiriwa kuhusu AMANI na wananchi wetu wamekuwa wapole wasioweza kuzi-challenge mamlaka.
 
Mkuu,Ujue sipika halindwi na katiba pindi anapovunja katiba

lakini kwa nini sasa hakuna anayemshughilikia?

Ni nani wa kumshughulikia
Ni kwasabb katiba yetu imemfanya rais kuwa juu ya katiba. Kwahiyo rais anamlinda spika. Hakuna wa kumgusa spika maana analindwa Γ±a rais.
 
Wewe ndio hujui umuhimu wa katiba na jinsi inavyofanya kazi.jielimishe kwanza ndo urudi kwenye mjadala.

..labda ungeanza naye taratibu. Jamaa ni mgumu kuelewa, pia inawezekana ametumwa.

..swali la kwanza je tuwe na katiba, au tusiwe na katiba?

..kama anataka tuwe na katiba, je, iwe katiba mzuri inajali maslahi na haki za watu wote? Au iwe katiba mbaya inayojali na kuwalinda viongozi peke yao?
 
Hizi fikra ni duni kabisa, hakuna ubaya wowote hata kama anayelilia katiba mpya ni mmoja tu nchi nzima, cha msingi anayelilia hiyo katiba mpya kaanisha madhaifu ya zamani na kapendekeza mambo mapya bora kabisa, so cha muhimu hao wanaopinga waone umuhimu wa kumsapoti anayedai make wajue tz itaendelea kuwepo ila wao ni wapitaji.
 
Hizi ni fikra mfu na za kipumbavu, akina nyerere wkt wanapgania Uhuru haikuwa ajenda ya watz wote Bali ilikuwa ni kakundi kadogo tu, thanks God kwa ilikuwa ni kwa manufaa ya weusi wote bila kujali idadi ya waliokuwa mstari wa mbele kudai, pia ktk hili la katiba hakuna ubaya tukapata katiba bora hata kama alieishupalia ni lissu pekee, make itakuwa ni kwa faida ya watz wote bila kujali kakundi kadogo
 
Nikikuuliza wewe hio katiba iliyopo inakusaidia nini so far? Unaweza kunijibu kwa ufasaha labda! Inakunufaisha in what ways mpaka utake nyingine as if you have stakes on it!?
Katiba iliyopo ni mbovu inanufaisha waliopo madarakani ndo maana tunadai mpya itakayo nufaisha hata wasio na madaraka.
 

Hahaahaaa haa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

"Nionyesheni ni wapi ambapo huyo mkuu wa mhimili huu wa Bunge alipohalalishiwa na katiba hii mbovu tuliyonayo kwamba naye hawezi kuwajibishwa,"

Kwamba hujui ilishapitishwa kuwa wakuu wa mihimili na manaibu wao hawawezi kushitakiwa kwa makosa yoyote yatokanayo na utekelezaji wa majukumu yao na hii sasa ni sehemu ya sheria kwa mujibu wa katiba?

Pia hutambui kuwa mapungufu ya katiba iliyopo ndiyo yanayoyaleta mikanganyiko unayoiongelea sasa?

Kimsingi kama hufahamu hali nzima ni kama hivi:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe.
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe.
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu.
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi.
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe.
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi.
7. Kuna utitiri wa vigogo wenye mapato yasiyoakisi tija, wala kuwa na ridhaa ya wananchi na wasiolipa kodi (stahiki) wanaopata uhalali kwenye katiba hii.
8. Nk nk.

Kwenye mazingira haya asiyewajibishwa kwa mujibu wa katiba atawajibika vipi kwa katiba hiyo?

Hadi hapo bado huoni umuhimu wa katiba muafaka zaidi tena katika hali ya dharura inayowezekana?

Unadhani ni mazingira yapi yalitufikisha tulikofika na awamu ya ile?

Katiba mpya yenye kuyaangazia kikamilifu mapungufu yote yaliyomo ni suluhisho kwa haki, usawa, na uhuru wetu, watoto wetu na hata watoto wa watoto wetu.

Hili ni hitajio sahihi na la msingi ambalo si sawa kupuuzwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…