Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Kwani katiba inamsaidia nini mtu aliyeko Kijijini zaidi ya wanasiasa kugombania keki ya taifa?
Hili swali inawezekana uliyeuliza ni PhD holder, lkn itoshe kusema tu nchi hii bado ina majitu majinga jinga mengi sana.
 
Jamaa nakuonaga una akili kumbe na wewe ni pimbi tu, haya hata kama sio lissu au mbowe kwanini asishabikie katiba itakayotoa fursa kwa mtz yoyote kupata madaraka kwa njia halali na ya wazi hata kama atakuwa ni yeye mwenyewe au babu yake au Dada yako?
Kumbe ww unataka kugombea urais?
 
Doh!!

Ni kati ya maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza kuhusu usimamiaji wa katiba yetu

Majibu umeyaona? Kwa hakika ni muhimu kuelewa vinginevyo unaweza kushangaa kwanini tusijikite kwenye gombesugu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Haiwezi kwani yanayopiganiwa ni maslahi ya wanasiasa pekee.
Kweli kabisa mkuu, katiba mpya ni takwa na hitaji la wanasiasa. Sisi huku vijijini mahitaji yetu makuu ni, huduma bora za afya, maji, shule, barabara, masoko ya uhakika ya kuuzia mazao yetu, nk. Hayo yote yanawezekana bila katiba mpya!
 
Kweli kabisa mkuu, katiba mpya ni takwa na hitaji la wanasiasa. Sisi huku vijijini mahitaji yetu makuu ni, huduma bora za afya, maji, shule, barabara, masoko ya uhakika ya kuuzia mazao yetu, nk. Hayo yote yanawezekana bila katiba mpya!
Uwe unasoma comments. Elimu kuhusu katiba na umuhimu wake inakuhusu sana wewe. Soma comments kuna elimu inatolewa humo. (Wewe unakwazika na tume huru ya uchaguzi) . Katiba ni zaidi ya tume huru ya uchaguzi.
Hizo huduma unazozisema kwa katiba hii kiongozi anaweza akaamua asizilete na usiwe na la kumfanya.
Hebu fikiria wakati jiji kama Mbeya linakosa barabara za uhakika jemedari akaenda kujenga airport kijijini kwake, akaweka mpaka traffic lights[emoji3]. Sababu hakuna wa kumcheck kwa mujibu wa katiba.
Soma comments mbalimbali utaelimika.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ikiwe sisi wanachadema hatuwezi kudai katiba ya CHADEMA inayotoa uenyekiti wa milele kwa Mbowe tunawezaje kupata ujasiri was kudai katiba ya nchi?

Mwamba tuvushe, wala hatutaandamana kukuondoa hakuna kama wewe, MWAMBA TUVUSHE.
 
Kwanini umlaumu spika na usiwalaumu wale wabunge at the first place?
 
Naunga mkono hoja.

Liwe takwa la wananchi na si kikundi cha wakosoaji wa utendaji wa Serikali,wasiwasingizie wananchi wakati hatujawahi kuwaona hata kidogo wakiamdamana au kuhamasishana kutaka hiyo Katiba.

Kazi iendeleee.
 
Katiba ambayo wananchi hawawezi kuisimamia unategemea watawala wataifuata kwa hisani yao? Bila sisi wenyewe kuwa na uelewa na atitude ya kuisimamia katiba hata tubadilishe katiba mara mia bado watu wataichezea tu.
Kweli tunataka katiba mpya ila wanasiasa wetu hawa wanaopigia kelele katiba mpya wakati hatujawahi kuwasikia wakipush elimu ya uraia na ujumla wake iboreshwe ni wachumia tumbo wanaotaka katiba ya kuwapa madaraka and nothing else.
 
Napinga uwanzishwaji wa mchakato wa katiba kwa sasa, Ni hadi wananchi watakapofahamu umhimu wa katiba hiyo

Kwani kwa sasa, ni kupoteza fedha za walipa kodi tu na kuwasaidia wanasiasa kuitafuta ikulu kwa manufaa yao

Tunataka kwanza wananchi wajue umhimu na namna bora ya kuilinda katiba na kuhakikisha wataitetea kwa nguvu zote na kwa gharama zote pindi mshenzi mmoja atakapoikanyaga
 
Kwani kipindi JK anafanya harakati za kupatikana kwa katiba mpya kupitia maoni ya wananchi ,wananchi walikuwa na elimu gani ya uraia kuhusu katiba?
 
Hivi mkuu kipindi Tume ya jaji warioba ilitumika kukusanya maoni kwa wananchi kuhusu katiba mpya wananchi walikuwa hawana elimu kuhusu katiba?
 
Hata katiba ya CHADEMA imemfanya Mbowe mfalme na mungu mtu. Hawezi kuibadili
 
Nitaaminije bila kuja na vipengele vya hiyo katiba, vifungu ambavyo vinaonyesha eti sipika naye amewekewa zuwio la kushitakiwa akivunja katiba pindi awapo kwenye kiti
 
Katiba inamsaidia nini mwanachi ambaye anahangaika kutafuta mlo mmoja kwa siku!?
Mnajua kabisa umuhimu wa katiba mpya yenye kujenga taasisi imara Ila kwa maksudi mnapinga kwa maslahi yenu na kuzidi kuwapumbaza Watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…