Pre GE2025 Nasikitika kusema mfumo wa CHADEMA bado hauna uwezo wa kupewa uongozi wa nchi, labda waufanyie marekebisho au tuwape muda zaidi miaka 10 au 15 ijayo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Soma Tena hoja na kuangalia maoni yaliyopita
Uelewe kwanza hoja kamanda
Usitake kutoonyesha ujinga wako wote mkuu
Nauliza tena, nchi za wanaoingia madarakani kwa kupindua na kuongoza nchi bila hiyo mifumo inakuwaje? Au unataka kutuaminisha kuongoza nchi ni jambo gumu sana linalohitaji hizi hofu unazoleta? Au unadhani kuongoza nchi ni lazima utumie wanachama wa chama chako tu? Au hiyo nchi itakuwa haina wataalam?
 
Kwani sasa tunatumia mfumo wa CCM?
 
Wao walidhani cdm itasambaratika kama cuf na vinginevyo na ndio maana wamekazana na Mbowe aachie ngazi.
 
Tumia muda wako kuwataka viongozi wa CCM waache uroho wa kujaza familia zao kwenye uongozi wa chama na serikali. Inasikitisha sana kuona wewe unafurahia kundi la viongozi na familia zao kuhodhi nchi.
 
..Ccm imehodhi uchaguzi tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

..wapeni nafasi wapinzani wateue tume na wasimamizi wa uchaguzi.
Naongelea Mfumo dhaifu wa chadema mkuu
Jaribu kupitia Tena hoja
Ccm ndo inafanya Mfumo wa Cdm uwe na mwanya wa kiongozi wa juu kuwa mkiti wa kudumu au maisha
 
Tumia muda wako kuwataka viongozi wa CCM waache uroho wa kujaza familia zao kwenye uongozi wa chama na serikali. Inasikitisha sana kuona wewe unafurahia kundi la viongozi na familia zao kuhodhi nchi.
Hoja yangu ni Mfumo dhaifu wa Cdm ambao hauwezi kubeba uongozi wa nchi hata wakipewa
Jikite hapo

Madhaifu na mapungufu ya Ccm yanajulikana wazi wazi ,
Ndo maana tunataka tupate chama kingine chenye Mfumo imara
Sio Kama Ccm
Umewahi kufikiri endapo UKAWA
Wangechukua uongozi wa nchi ingekuwaje Leo Cuf, Cdm , Nnssr, Nld Leo hata hawakai meza moja Tena

Kama Mfumo wa upinzani ni dhaifu kuliko au sawa na Ccm
Basi hamna haja ya kutoa Mfumo Ccm mkuu


Ila Cha kushangaza Kuna wapumbavu wachache wqnakuambia eti
Mbona Ccm wao wanafanya hivyo au Mfumo wao uko hivyo

Sasa Kama na upinzani Wana Mifumo ile ile ya Ccm kwanini tuwatoe ccm wenye uzoefu na Mfumo wao dhaifu
 
Naongelea Mfumo dhaifu wa chadema mkuu
Jaribu kupitia Tena hoja
Ccm ndo inafanya Mfumo wa Cdm uwe na mwanya wa kiongozi wa juu kuwa mkiti wa kudumu au maisha

..udhaifu wa vyama mbadala vya siasa unatokana na Ccm kuhodhi mifumo ya kidola, kiserikali, na kimahakama, nchi nzima.

..tulipoingia ktk mfumo wa vyama vingi hakukufanyika mabadiliko wezeshi kwa mfumo huo kama ilivyopendekezwa na Tume ya Jaji Mkuu Nyalali.
 
Ina maana Hadi katiba za vyama mbadala zinaandaliwa na Chama tawala Hadi kuwa loop hole ya kiongozi wa juu kumiliki chama na kuhodhi madaraka maisha ????
 
Sishangai watu smart kuhama Chadema
Mfumo wake bado ni dhaifu mno kuhandle watu smart
 
Ina maana Hadi katiba za vyama mbadala zinaandaliwa na ccm

..hicho sicho nilichomaanisha.

..maana yangu ni kwamba mazingira ya kisiasa tangu tuingie mfumo wa vyama vingi yameifanya Ccm iwe sawa na muamuzi na mchezaji ktk mechi ya mpira.
 
Naendelea kusikitika Sana juu ya Mfumo Chadema unaweza kukipeleka kwenye level ya akina Tlp ya Mzee mrema , Chama Cha cheyo na kule Lipumba anakoipeleka Cuf

Mfano mzuri ni pale unapokosoa Cdm baadhi ya wafuasi wake wanakutolea mfano eti mbona hukosoi hivyo vyama vya akina Cheyo na Rungwe

Wakijitahidi Sana watakutolea mfano KUTOKA chama Tawala eti mbona waoa wanafanya hivi na vile

Sasa unataka uwe mdadala alafu unafanya Yale Yale na vibaya kuliko aliyepo alafu Unataka ulete mabadiliko , how ???

Ni mwendawazimu pekee anayeamini atapata matokeo tofauti kwa kufanya Yale Yale

Ni masikitiko makubwa Sana kufikisha miaka zaidi ya 30 ya vya vingi na kutokua na chama mbadala chenye Mfumo imara kuweza kukabidhiwa madaraka
 
Laiti Cdm ingekuwa na vijana wengi werevu wangeweza kupambana ndani kwa ndani kuleta mabadiliko ya Mfumo wa Chama !!
Lakini bahati mbaya imefika mahali Cdm inakuwa na vijana machawa wa viongozi Kama chama Tawala
So sadness kwakweli
 
..hicho sicho nilichomaanisha.

..maana yangu ni kwamba mazingira ya kisiasa tangu tuingie mfumo wa vyama vingi yameifanya Ccm iwe sawa na muamuzi na mchezaji ktk mechi ya mpira.
Pamoja na udhaifu huo lakini bado vyama vya upinzani vimeonyesha udhaifu mkubwa zaidi kwenye mifumo yao ya ndani

Angalia kuanzia mfano wa vyama vikuu tangu 1995 ukianza na Nssr, Cuf, na kule Chadema inakolekea kwa Sasa Hali ZAO kwa sasa

Pia piga picha ya Mfumo wa UKAWA wa 2015 Kama wangeongoza serikali Leo Mfumo wa uongozi wa nchi yetu ingekuwa katika Hali gani ????
 
Juma duni alisema hicho ni chama cha makambare wote wana ndevu!
 
Wekweli boya Kwa akili Yako unadhani ukawa ingeshindwq kuongoza ki nchi kama tanzania chenye watu million 60 na kuleta maendeleo tofauti na anachofanya chura kiziwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…