Nasimama na Mkuu wa mkoa wa Dar, kutukumbusha kuwajibika

Kulipa kodi haimaanishi upate huduma za bure hospital.
Kwahio Nurse ndio anakusanya michango ya Gloves ?, Kwanini aishie kwenye gloves pekee na asiseme kabisa aje na msaidizi wa wa kumsaidia kubeba vidonge au atoke navyo nyumbani, na Je hayo ndio makusanyo official au ni ya pembeni ? Sababu hospitali karibia zote sasa hivi bado kuna watu wanalipia vitanda na mambo mengine mengi tu.

Sasa kama hi ni official kutoka kwa Utawala kwamba kila mtu kivyake basi na kwenye kukatana matozo waache wakafungue biashara za nyanya part time na wao wajilipe mishahara.

Extract from NHS UK (Yaani hata kama ukiwa sio Entitled kwanza utatibiwa alafu mambo mengine baadae)
 
Na kwa hiyo wao hakakufanya projection ya mahitaji ya vifaa tuwachukulie wako chini ya viwango vya utendaji?
Vifaa vipo changia gharama pale walipopungukiwa
Wamejenga hospital, madaktari, wauguzi na wakunga wapo
We kuchangia elfu 50 ili mkeo ajifungue, unalia kama punda aliyepoteza ndama
 
Duuuh ujuaji
 
Vifaa vipo changia gharama pale walipopungukiwa
Wamejenga hospital, madaktari, wauguzi na wakunga wapo
We kuchangia elfu 50 ili mkeo ajifungue, unalia kama punda aliyepoteza ndama
Walitamka huduma hizo ni free
Watimize ahadi
 
Umeandika ujinga sana.
Huduma za kujifungua, watoto chini ya miaka 5 na wazee zaidi ya miaka 60 ilipaswa kuwa bure kwa hospitali zote za umma.
Wanaotaka kugharamia si huwa wanaenda private?
 
Walitamka huduma hizo ni free
Watimize ahadi
Huduma ni Bure
Sasa unataka udai serikali ikupe nepi, pampasi, mavazi, na maziwa ya mtoto. Bure
Jiongeze mkuu
 
Umeandika ujinga sana.
Huduma za kujifungua, watoto chini ya miaka 5 na wazee zaidi ya miaka 60 ilipaswa kuwa bure kwa hospitali zote za umma.
Wanaotaka kugharamia si huwa wanaenda private?
Huduma ni Bure mkuu
Kuchangia gloves hakuondoi Nia njema ya serikali
Tusitake maneno matamu
 
Sio kweli mkuu
Hata kama, kuchangia gharama za kujifungua haipaswi kuwa jambo la kupigia kelele
Sasa tutawezaje kupinga rushwa za rasimali zetu, ikiwa hata mtu unashindwa kuchangia elfu 50 ili mkeo ajifungue
...Unapolipa Kodi na Tozokibao, Hela wanapeleka Wapi ??...
 
Vifaa vipo changia gharama pale walipopungukiwa
Wamejenga hospital, madaktari, wauguzi na wakunga wapo
We kuchangia elfu 50 ili mkeo ajifungue, unalia kama punda aliyepoteza ndama
Aliyejenga hospital ni nani ?
 
Ukilipa Kodi ndo usiwe na bima ya afya,
Tuwape wanawake mimba, uwasukumie serikali?
...Serikali inaposema inapunguza Vifo vya Kina mama na Watoto, inahusika vipi, lakini kwenye glovu haihusiki ???
 
...Unapolipa Kodi na Tozokibao, Hela wanapeleka Wapi ??...
Ukilipa tozo ndo usinunue nepi, usinunue gloves, usinunue kitabu cha mwanao shule, usilipe pesa ya tuition ya mwanao
Hebu kuwa serious acha dezo
 
Serikali ni watu
Sawa nilitaka nijue hilo mana kwenye comment zako inaonesha huyo serikali ni mtu tu mfano wa bakhera anachukua pesa zake kwenye kibubu halafu anajijengea hosptal..
 
Sawa nilitaka nijue hilo mana kwenye comment zako inaonesha huyo serikali ni mtu tu mfano wa bakhera anachukua pesa zake kwenye kibubu halafu anajijengea hosptal..
Hapana hospital tumejenga sisi
Lakini haituzuii kuwajibika kama waume na baba wa watoto
 
Hapana hospital tumejenga sisi
Lakini haituzuii kuwajibika kama waume na baba wa watoto
Una mtoto ushawahi kulea mimba ?..ghalama za kulea mimba na mtu mwenye mimba ni kubwa mara dufu zaidi ya hiyo 50000, sasa ikitokea mtu akasuasua kwenye hiyo 50000 kaa naye umpe muda akuelezee kipi kinachomsibu usimkejeri eti kiasi kidogo wakati katumia gharama kubwa zaidi ya hizo
 
Unaenda kinyume na sera ya afya, hao wanafadhili na UZAZI salama, kupunguza vifo vya mama na mtoto, pesa hizo zinaenda wapi?
 
Nakuelewa sana mkuu
Huo utu upo
Me nazungumzia watu kuona kama afya ya uzazi ni Bure na kuwaachia serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…