Kuna wale wanawake ambao hutamani kuzaa na waume wa watu waliowapenda wajihi wao, hutaka kubeba mimba nao. Pia kuna wale wasiokuwa na mvuto wa kutongozwa hawatongozwi mpaka wanaanza kuzeeka nao hutamani mwanaume yeyote awasaidie kupata mimba wapate watoto, kuna walemavu wa aina mbalimbali nao hutaka kujamiana na kupata watoto, je hawa hawana haki? Approach yao ikoje ili nao wapate haki ya kujamiana bila kudhulumiwa?
Mungu ameumba watu kimadaraja, Makundi, jamii .
Hakuna mtu ambaye atakosa wa kufanana naye.
Ndio hapohapo tunarejea kwenye suala la HAKI,
Wewe upo daraja F ukafanya hila ukazaa na mtu wa daraja A bila RIDHAA yake hiyo ni dhulma. Kwani utakuwa umemkosea Yule.
Kuna hii,
Mwanamke anaweza akajichubua, akajichonga kwa hila ili ampate mwanaume au wanaume wa aina Fulani.
Sasa wewe umekuja zako, ulikuwa unataka kwenye maisha yako uzae na mwanamke mwenye rangi nyeupe, mwenye shape, kwa bahati mbaya ukakutana na huyu aliyefanya hila kujibadilisha.
Ukamuoa, mkazaa watoto lakini wale watoto hawafanani na vile ulivyokuwa umetarajia, kutokana na udanganyifu wa mama Yao.
Baadaye ukagundua Mkeo alijikoboa na kujibadilisha. Je utakuwa umetendewa HAKI?
Jibu la ukweli Kabisa ni kuwa, utakuwa umedhulumiwa,
Hiyo sio Haki
Haina tofauti Sana na mwanamke kubeba Mimba wakati wewe haukuwa na Nia ya Jambo hilo isipokuwa starehe tuu