Nasisitiza, itungwe Sheria kubeba Mimba bila ridhaa ya Mwanaume liwe kosa la jinai

Nasisitiza, itungwe Sheria kubeba Mimba bila ridhaa ya Mwanaume liwe kosa la jinai

Kwenye masuala ya faragha za watu unaipimaje ridhaa ya mtu......??

Inawezekana mtu akaridhia wakiwa faragha ili apewe kavu then kwenye kadamnasi ya watu akamkana....??

Sex ni makubaliano ya watu wazima wawili wenye akili timamu na bila shaka wanafanya wakijua matokeo yake.....unless kuna mmoja amebakwa ...

Watu wazima waliofanya jambo kwa utashi wao....wote wanapaswa kuwajibika kwenye matokeo ya jambo hilo.....

Kama hutaki kumpa mtu mimba kwanini unakazania upewe kavu kavu.....??
Mjadala umeishia hapa
 
Kumrubuni Mwanafumzi au msichana chini ya miaka 18, na akakubali kishiriki ngono. Huo ni ubakaji wa Ridhaa au bila Ridhaa?

Huo ni ubakaji bila RIDHAA
Ondoa kumrubuni.
Weka, msichana mdogo wa Miaka 16 wa kidato cha pili amekufuata umpe vitu. Ukampa, akapata Mimba. Je ni ubakaji wa RIDHAA au bila RIDHAA?

Neno kurubuni, kulaghai, kudanganywa linarejelea matumizi Mabaya kwa mtendewa,
Kurubuniwa au kulaghaiwa au kudanganywa haiwezi kuwa RIDHAA ya Mtu.
 
Kaka Nilikuwa nakuona una busara lakini akili huna, wewe ndo unawekeamo kwa hoyari, una mwaga ndani, hayo matendo yako mawili ni “invitation to treat - kwenye basic business law “ unamlaumu Vipi mwanamke?
 
Kaka Nilikuwa nakuona una busara lakini akili huna, wewe ndo unawekeamo kwa hoyari, una mwaga ndani, hayo matendo yako mawili ni “invitation to treat - kwenye basic business law “ unamlaumu Vipi mwanamke?

Hakuna anayelaumiwa hapa.
Hapa ni Sheria za HAKI.

Ni Sawa uniulize, Binti wa Miaka 15 ambaye anatumia hiyari yake kukufuata wewe umpe mjegeje ukampa, iweje wewe uonekane unamakosa?

IPO hivi, kila Sheria zina MUKTADHA wake.
Watu wanafanya ngono kwa sababu mbalimbali, na Mojawapo ya hizo Sababu ni starehe.

Starehe ya mwanaume kwenye ngono ni kumwaga, tena kumwagia ndani. Hiyo ipo naturally.
Kumzuia mwanaume asimwagie ndani Kisa kuna ujauzito wakati aliyeuumba mwili wa mwanamke kaweza tarehe za ovulation na sio kila siku ni za Hatari ni kutokuwa na maarifa ya haya mambo. Na hivyo sio ajabu watu kutozingatia MUKTADHA wa Jambo lenyewe.

Wewe kwa unavyojua, unafikiri ni Kwa nini sio Muda wowote mwanamke anaweza kupata Mimba isipokuwa kuna Muda maalumu?
 
mtibeli zingatia haya
(1)wanawake wengi hawajui Wala kumfahamu elimu ya uzazi (anapigwa Leo kavu YAI linakomaa kesho mbegu inakaa masaa 24 inatafuta pakuingia--- vikikutana hiyo imo)

(2) Pia ongezea hapo ngono bila kondom kwa wasio wanandoa -itungwe adhabu Kali wakipeana mimba

isiwe kwa mdakaji tu mimba iwe kwa wote
 
Mungu amtia Mariam Mimba bila ridha yake, ndo huyu Yesu mnae muita mwana wa Mungu kuja kuwaokoa, je Mungu angemuuliza Maria na angekataa Yesu angepatikana? Je hizi Dini zenu zinazo zungukia kwa yesu tu zingekuepo?

Luka 1:26-38
26 Miezi sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alim tuma malaika Gabrieli aende katika mji wa Nazareti, ulioko Gali laya, 27 kwa msichana bikira aliyeitwa Mariamu. Yeye alikuwa ameposwa na mtu mmoja aliyeitwa Yusufu, wa ukoo wa Mfalme Daudi.
28 Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia: “Sal aamu, ewe binti uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”
29 Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, maana ya salamu hizi ni nini. 30 Ndipo malaika akamwam bia, “Usiogope, Mariamu, Mungu amependezwa nawe. 31 Sikiliza, utapata mimba, nawe utazaa mtoto wa kiume; na utamwita jina lake Yesu. 32 Mtoto huyo atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Mfalme Daudi, baba yake. 33 Atatawala juu ya nyumba ya Yakobo daima; na ufalme wake hau takuwa na mwisho!”
34 Mariamu akamwuliza malaika, “Lakini, nitapataje mimba, na mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu ata kujilia na nguvu za Mungu zitakufunika kama kivuli, na kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu na ataitwa Mwana wa Mungu. 36 Tena, miezi sita iliyopita binamu yako Elizabeti, aliyeitwa tasa, amepata mimba ingawa ni mzee sana. 37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilo wezekana.”
38 Mariamu akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.’ ’ Kisha malaika akaondoka.

 
Point,hapa mkuu leo nimekuelewa sana

Mfano kuna binti mmoja nilimuita mahali nilikuwa na job ya muda tu,huyu binti alikuwa na tatzo la uzaz,kabla ya kuja nilimwambia anakuja tule bata tu na sio kuoana lakin alivyokuja kaja na dawa za kupata mimba nilivyomuuliza ananiambia ni dawa za tumbo,mwez mmoja tu akanasa mimba,huu ni utapeli
 
Kuna jamaa pia tunasali nae, amempiga biti mkewe baada ya kubeba mimba isiyotarajiwa. Kamwambia kabisa hiyo ni yako hainihusu.
Wanawake ni vichwa vigumu huwa hawaelew,mimi mke wangu nilimwambia kwasasa tupumzike walau hata miaka 3 nikaongezea nakumwambia kuwa ukipata mimba haraka utateseka sana lakin hakuogopa hata hayo maneno,nikawa na withdrawal namwaga nje lakin akawa analalamika mim kufanya hvyo lakin siku moja akaning'ang'ania na ngoma ikatunga siku hyo hyo
 
Hili jambo Trump akiliona atakubaliana na cc moja kwa moja
 
Mwanamke ndiye mwenye Mamlaka na suala lote la Mimba

Ndio maana watu wenye Akili, miungu yenye akili, akiwepo muumba wa mbingu na nchi lazima afuate itifaki hiyohiyo.

Ikiwa Mungu atataka kumpa mwanamke mtoto hawezi kumfuata mwanaume Bali atamfuata Mwanamke husika. Na lazima apate RIDHAA ya huyo Mwanamke
Njia za kuzuia mimba zipo kwanini ukwepe kuzitumia?
Ni sawa ukatae kulala kwenye chandarua alafu ukiumwa malaria useme eti imeingia kwenye mwili wangu bila idhini.
 
NASISITIZA, ITUNGWE SHERIA KUBEBA MIMBA BILA RIDHAA YA MWANAUME LIWE KOSA LA JINAI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Mwanasheria wa Tibeli.

Andiko hili liwafae wale wapendao HAKI. Andiko hili lipitiwe na kujadiliwa na wale Wanasheria wa kusomea na wale Wanasheria wa kuzaliwa wenye MAARIFA na AKILI za juu.

Liwe kosa la jinai kumpa mwanafunzi au mtoto mdogo Mimba. Hilo ni kosa tayari na adhabu yake inafanyika.

Liwe kosa la jinai kumbaka mtu yeyote mtu mzima na hapa tunazungumzia ubakaji wa aina mbili,

1) ubakaji wa RIDHAA
2) ubakaji usio wa RIDHAA.
Ubakaji wa RIDHAA ni ule ambao unatokana na makubaliano ya ngono ambayo yamekiukwa. Ubakaji huu hufanyiwa Wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba.

Mfano; Mwanaume kakubaliana na Mwanamke wakishafanya ngono atatoa 50,000/= lakini baada ya tendo Hilo kufanyika. Mwanaume akagoma kutoa Ile elfu 50 Kabisa au akatoa nusu ya Ile Pesa.

Hiyo ndio tunaita ubakaji wa RIDHAA. Yaani walikubaliana lakini baadaye Mwanamke akageukwa. Hivyo tendo lile linageuka kuwa ubakaji kwa Sababu baada ya tukio makubaliano hayakufuatwa na hiyo ikapelekea mwanamke kulipinga tendo la ngono lililokwisha kufanyika na kuhisi kuonewa.

Kwa sisi watibeli, Wanasheria wa Tibeli, majaji na mahakimu,na makadhi na majina yote yahusuyo utoaji wa Haki na uchambuzi wa Haki na sheria. Tunaita tendo Hilo ni ubakaji.

Mfano wa pili katika UBAKAJI WA RIDHAA.

Mwanamke kaenda kwa mganga wa kienyeji au mtu yeyote labda ni mtu ajiitaye Nabii au jina lolote lenye kiwakilishi cha Watumishi wa miungu.

Mwanamke huyo akaambiwa ili Dawa ifanye Kazi itampasa alale na Mganga wa kienyeji au mtu huyo ajiitaye Nabii au jina lolote la wawakilishi wa miungu. Ili apate Msaada.

Kwamba kuingiziwa uume mwilini mwake ndio Dawa. Akaridhia ili shida yake ipate Dawa. Tendo hilo la ngono linakuwa sio ubakaji kwa Sababu mwanamke aliridhia mwenyewe kwa Maslahi yake. Lakini ikatokea, shida yake haijatatuliwa, na kumbe alilaghaiwa. Hapo ndipo tendo lile la ngono litaitwa Ubakaji wa RIDHAA. Na ni Kosa.

Jambo linakuwa kosa kutegemeana na mambo Makuu yafuatayo;

1. Linamdhuru mtendewa hasa mwenye shida na mnyonge.
2. Haliendani Sheria za mahali husika

UBAKAJI USIO WA RIDHAA huu unafahamika katika jamii nyingi duniani. Sina haja ya kuuelezea.

Matokeo ya ubakaji ni Mengi lakini Makubwa ni Mimba zisizo tarajiwa, Magonjwa, kuathirika kisaikolojia na kimwili, kumdhalilisha mtu na kumharibia mtu hadhi yake.

Tukirudi kwenye Mada.

Kwa Watibeli, ni kosa la jinai KUBEBA MIMBA BILA RIDHAA ya MWANAUME.

Ikiwa mwanaume atafanya mapenzi/ngono na mwanaume mwanamke mwenye umri sahihi kwa RIDHAA ya mwanamke, Kwa lengo la kustarehe tuu bila lengo jingine.
Alafu ikatokea mwanamke huyo akabeba Mimba iwe kwa makusudi au bahati mbaya bila RIDHAA ya MWANAUME. Tendo Hilo litachukuliwa kama KOSA la jinai.

Kwani mwanaume atakuwa mkosewa, hakuwa na mpango wowote wa Kumpa mwanamke Ujauzito. Ni hakika taarifa ya ujauzito itamuumiza na kumkosea.

Ili mwanamke abebe mimba itampasa apewe ruhusa na Mwanaume. Sio kujibebea bebea Mimba bila ruhusa ya Mwanaume. Hii itaathiri Uwajibikaji huko mbeleni.

Hii itamaanisha, ili mwanamke abebe mimba itampasa afanye makubaliano na mwanaume. Makubaliano hayo yapo ya aina mbili;

1. Ndoa
Haya ni makubaliano ambayo ni maarufu. Mke wa ndoa hana haja ya kuomba Ruhusa kuomba Kupata ujauzito kwa Sababu Moja ya majukumu yake kama Mke ni KUBEBA MIMBA. Yaank Hilo ni Moja ya majukumu Makuu ya mwanamke kwenye Ndoa.

2. Makubaliano ya kibinafsi ya hiyari
Kwamba mwanaume anakubaliana na mwanamke ambaye sio mkewe kuwa amzalie mtoto/watoto.
Makubaliano haya lazima yawe na mashahidi. Na yawe ya maandishi.

Kwa Sheria za Kitibeli, ni jinai mwanamke kubeba Mimba ya Mwanaume mwenye Mke bila RIDHAA ya Mke.

Kama ilivyo, ni jinai kwa mwanamke aliyeolewa KUBEBA Mimba ya Mwanaume mwingine asiye mumewe bila RIDHAA ya Mume. Hiyo ni dhulma na haramu.

Makubaliano yoyote ya KUBEBA Mimba yatakuwa batili bila ya uwepo WA mashahidi ambao ni Halali.

Kwa Watibeli, KUBEBA Mimba bila RIDHAA ya MWANAUME mtoto husika hata akizaliwa hatatambulika kama mtoto wa huyo mwanaume. Mtoto atakuwa wa Mama au huyo mwanamke aliyembeba.

Ni vizuri, kabla hamjafanga ngono muweke wazi lengo la ninyi kufanya ngono. Je ni starehe au kwaajili ya kuleta kiumbe.
Kama ni biashara au ni kitu gani.

Sheria za HAKI zinapovunjwa huko mbeleni huleta madhara kwa watoto na jamii.

Bila ridhaa ya Mwanaume, baadhi ya wanawake matapeli hutumia mwanya huo kuvunja makubaliano na kuharibu familia za watu.

Ngono sio kwaajili tuu ya kuzaa Bali ngono ni starehe.
Ndio maana siku za Hatari zipo Tisa. Siku za kufanya ngono ziko kumi na Moja na siku za period zipo 5-8

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Watibeli ndo wakina nani?
 
Back
Top Bottom