Unavyolala chali, regardless ni mchana au usiku halafu hali hiyo ikatokea ni jambo la kawaida, sayansi inaliezea vizuri tu, hata mimi limenitokea mara nyingi mno, mchana au usiku,
Hali yenyewe inajulikana kama "sleep paralysis", kuna aina mbili ya sleep paralysis, moja ni wakati umeingia kulala, kabla hujasinzia kabisa, nyingine ni kabla hujaamka, Sababu hasa ni nini?
Kulala kuna stage mbalimbali, ukiwa kwenye stage moja inayojulikana kama Rapid Eye Movement (REM), ubongo unazima signal kwenda kwenye misuli ili ukiwa ndotoni usijitingishe sana, sasa ikitokea ukaamka ghafla wakati bado upo kwenye REM stage, lazima u-experience hili tatizo sababu bado ubongo haujaamua kucontrol misuli ya mwili, Ukiwa kwenye hii stage, tulia tu usikilizie ndani ya sekunde chache ubongo utajishtukia kua kuna kitu hakiposawa na control itarudi kama kawaida,
Na haihitaji hata kumuona daktari wala kuondoa sijui mapepo, ni jambo la kawaida sana lisilo na hatari yoyote.
Hiyo pekee ndiyo sababu, imehakikiwa mara nyingi tu kwenye experiments na mjadala ukafungwa,
Anayesema jinamizi muulize kama alishawahi kuliona umkamate uongo, ataanza kutapatapa.