Unafanya kosa. Ni-address mimi sio sisi.
Mimi sijui hao unaowasema. Haya ni mawazo yangu na hayafungamani na mawazo ya hao ulionao akilini...
Unajichanganya.
Humuamini Magufuli, unafikiri atajiongezea muda wa urais.
Lakini, ukiulizwa, sawa, labda atajiongezea muda wa urais, mzuieni. Lakini, hata mkimzuia asijiongezee muda wa urais, hilo litamzuia vipi kumuweka mtu wake awe rais baada yake na yeye Magufuli aendeleze mamabo yake kwa remote control?
Ukiulizwa swali hili, unajibu "sijui hilo unalitoa wapi".
Yani huyu Magufuli ambaye humuamini katika kujiongezea muda, unamuamini kwamba akizuiwa kujiongezea muda hatataka kumuweka rais wake kibaraka?
Inakuwaje usimuamini Magufuli kwenye kujiongezea muda wa urais, halafu ukaamini kwamba hatajiwekea kibaraka wake baada ya kushindwa kujiongezea madaraka?
Ukiweza kumzuia Magufuli kuongeza muda wake wa urais, una mkakati gani wa kuhakikisha rais anayefuata hawezi kuwa kibaraka wa Magufuli au mbaya kuliko Magufuli?
Kwa nini una focus kwenye mtu zaidi ya ku focus kwenye mfumo?
Kwa nini mtu akikuonesha kwamba your approach is narrow in vision and myopic, unaishia kusema "hiyo inatoka wapi na kwa nini iwe hivyo?
Hatujui hata kama Magufuli atafika hiyo 2025. Anaweza kuanguka mwaka huu asiuone hata mwaka ujao. Hakuna mtu aliyekuwa guaranteed kuiona kesho.
Una mkakati gani wa kuhakikisha rais wa Tanzania, yeyote yule, si Magufuli tu, hana mianya mingi ya ku abuse nguvu za kirais?
Una mkakati gani wa kuweka mabadiliko ya kikatiba ya kuzuia rais kuwa na nguvu sana?
Una mkakati gani wa kuhakikisha tunapata bunge lenye nguvu ya kufanya checks and balances?
Una mkakati gani wa kuhakikisha matokeo ya kura za urais yanaweza kupingwa mahakamani?
Una mkakati gani wa kuhakikisha tunapata tume huru ya uchaguzi?
Una mkakati gani wa kuzuia wizi wa kura?
Una mkakati gani kulazimisha uwazi zaidi na uwajibikaji zaidi kisheria?
Una mkakati gani wa kuhakikisha wananchi wanaondoa woga, wanapata elimu ya uraia zaidi na wanadai haki zao?
Hayo ndiyo maswali ya msingi.
Uki focus kuhakikisha Magufuli haongezi muda wa urais 2025, Magufuli anaweza kujifia hata 2025 asifike. Ukampata chinjachinja mwingine anapenda damu kuliko Idi Amin.
Magufuli kuondoka hapo kutakusaidia nini?