Tatizo la Watanzania wengi kwa sasa, ni ukweli kwamba wamepoteza au hawana uwezo wa kujadili hoja kimantiki.
Wamechagua upande mmoja, na katika mjadala wowote wanatetea timu yao kishabiki zaidi. Bila kujali principle wala fact.
Ndiyo maana ni vigumu sana kumpata mtu ambaye mara nyingine anamsema Magufuli vibaya, na mara nyingine anamtetea. Kama ninavyofanya mimi leo, kumtetea Magufuli based on principle ingawa mara nyingi namsema vibaya.
Hii ni kwa sababu wapinzani wa Magufuli, wengi wao wako tayari kuunga mkono uzushi wowote unaomtuhumu Magufuli vibaya.
Na watetezi wa Magufuli, wengi wao wako tayari kumtetea katika uozo wowote.
Jiulize, wewe unayemtuhumu Magufuli leo, lini uliwahi kumtetea? Je, hana cha kumtetea?
Na wewe unayemtetea Magufuli leo, lini uliwahi kumtuhumu? Je, hana cha kumtuhumu?
Watu wachache tunaoangalia mantiki ya hoja tu tunaweza kumsema vibaya Magufuli anapokosea, na kumtetea anapoonewa.
Kumhukumu mtu yeyote, kwa kosa analotarajiwa kufanya mwaka 2025, ni kitu kibaya sana.
Hiki kitu kinaitwa pre-crime
Tukiendelea na mawazo haya, tunaweza kusema tuwafunge watoto wanaozaliwa Manzese Kwa Mfuga Mbwa, kwa sababu watoto hawa, wakikua wakubwa ni lazima watakuwa majambazi tu.
Pre-crime wiki
en.m.wikipedia.org
Pre-crime (or precrime) is a term coined by science fiction author Philip K. Dick. It is increasingly used in academic literature to describe and criticise the tendency in criminal justice systems to focus on crimes not yet committed. Pre-crime intervenes to punish, disrupt, incapacitate or restrict those deemed to embody future crime threats. The term pre-crime embodies a temporal paradox, suggesting both that a crime has not occurred and that the crime that has not occurred is a foregone conclusion.[1]