Fahamu tu kuhusu haya machache.
1. Hakuna Dikteta aliyebadilisha katiba ili kuongezewa muda akawa analiongea hilo suala kabla. Mara zote hukana au kukaa kimya wakati vuguvugu likishika kasi. Wanaolisema huwa ni wapambe wa watawala.
2. Suala hili limekuwa likipigiwa debe na viongozi waandamizi na wateule wa Magufuli kwa muda mrefu sasa, na hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na Magufuli mwenyewe wala na CCM.
3. Jambo linalosemwa semwa na watu tofauti tofauti kwa nyakati tofauti kuwa linapangwa kutokea, maana huo mpango upo au huenda ukawepo tu nyuma ya pazia. Watu husema kile wanachokiona, kukisikia au kukihisi.
1. Kwamba hakuna dikteta aliyebadilisha katiba ili kuongezewa muda aliyeongelea hilo, hakumfanyi Magufuli aongeze muda.
Sasa, wewe unajuaje kwamba Magufuli ataongeza muda? Una ushahidi gani zaidi ya speculations tu?
2. Wapambe huwa hawakosi. Lakini hao ni wapambe, kitu muhimu ni rais mwenyewe anataka kufanya nini?
Nyerere alihutubia katika hotuba yake moja, akasema, alikuwa anataka kujiuzulu kwa muda mrefu.Lakini kila akitaka kujiuzulu, wapambe wake wakawa wanamuambia "Mwalimu endelea kidogo, taifa linakuhitaji sana".Kila akitaka kujiuzulu akawa anaambiwa hivyo.Mwishowe akasema akaja kugundua kwamba hawa wapambe waliposema "taifa linakuhitaji", maana yao haikuwa taifa linamuhitaji,ila wao wenyewe walikuwa wanahitaji Nyerere aendelee kuwa rais, kwa sababu walihofia akija rais mwingine atakuja na watu wake.
Nyerere alivyowasitukia, akasema aliwapuuza na kujiuzulu.
Kwa hivyo, hawa wapambe wapo tu, hawajaanza leo.Walikuwepo tangu enzi za Nyerere.
Sasa, mnashikia bango suala la wapambe ambalo rais mwenyewe kashasema hataongeza muda?
3.Let's separate facts from speculations.Ukitaka kujadili speculations unaweza kusema lolote. But where are the facts?
The facts are.
1.Mgufuli kakanusha kwamba ataongeza muda.
2.Katiba hairuhusu hilo.
3.Wanalosema hilo ni wapambe tu.
Magufuli ana makosa mengi sana, ambayo kashayafanya.Mengine ya juzi tu kwenye uchaguzi wa 2020.
Kwa nini tunamtungia makosa ambayo hata hajayafanya bado badala ya kuangalia makosa aliyokwishafanya tayari?
Mtu anayemlaumu na kumhukumu Magufuli kwa makosa atakayoyafanya mwaka 2025 ni kama tajiri bilionea mwenye mali nyingi sana, ambaye licha ya utajiri wake na kuwa na hela zote anazohitaji, bado anakwenda benki kuomba mkopo, tena mkopo wa riba ya juu sana.
Mna utajiri wa makosa ya Magufuli, kwa nini mnaenda kukopa benki kwa riba kubwa sana?