Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Umeandika kama utani, lakini kuna point ya muhimu hapo.

Ukiacha dini.

Hata katika CCM kwenyewe kuna watu wanautumbulia macho urais, hawataki kumuachia utamu mtu mmoja miaka yote.
Mimi ni mkristo ila huu ni utamaduni mzuri kuepusha migongano isiyo ya lazima.
 
Kama unakubali kirahisi hivyo uchaguzi wa 2020 ushapita, hata kama Magufuli akijiongezea muda wa urais 2025 hutafanya kitu.

Utasema tu uchaguzi wa 2025 ushapita.

Na kuanza kulalamika "Magufuli atajiongezea muda tena 2030".

Kelele zote ni bure tu.
Sina tatizo na magufuli kuongeza muda as long as Wananchi watakaa kimya na kukubaliana na hiyo hali.

Wananchi mamia kwa maelfu Wakiamka na kutaka kumtoa then sitakuwa upande wake.
 
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Just the facts please.

The facts are.

1. Tanzania haina utamaduni wa marais kuongeza muda.
2.Katiba hairuhusu hilo.
3.Magufuli kasema hataongeza muda.
4.Wapambe wa kusema rais aongeze muda walikuwepo tangu enzi za Nyerere.
5.Habari za kwamba Magufuli ataongeza muda ni speculations tu, hazina msingi wa fact.

kama hutaki kuamini, sasa nina uhakika gani hata ukijua utaamini ??...

1. Utamaduni ni mfumo wa maisha, sio static maana hubadilika kutokana na mahitaji ya muda.
Hakuna utamaduni wa Tanzania katika siasa usioweza kubadilishwa iwe kwa ugumu au urahisi mfano Tanzania ya baba zetu ilikuwa rais kukaa zaidi ya miaka 20 na hata baada ya kura za kupigia mfumo wa multipartism bado 80% walipigia monopartism. Multipartism ililetwa kwa Maamuzi ya VETO kwa hiyo tuseme tamaduni yetu ilikuwa monopartism au multipartism

2. Katiba ipi ilifuatwa kwa wabunge 19 kuapishwa pasipo barua kutoka katibu wa chama cha CHADEMA ,

Katiba ipi ilifuatwa kwenye sakata la CAG

Katiba ipi ilifuatwa kwa CAG mpya kuambiwa atafukuzwa kazi na Rais !!!..

3. Aliyesema maendeleo hayana chama na akakiri kuwa hakupeleka maendeleo baadhi ya sehemu kwa kuwa walimchagulia upinzani ni nani ??..

If you cant be consistence with your words, tukuaminije !!!

4. Wapambe sio waamuzi wa mwisho.. mwenye uamuzi wa mwisho ni muhusika japo wapambe mara nyingine hutoa alert

5. Speculations zaweza kuwa na baseless facts lakini haimaanishi ni za kupuuzwa maana wenye nia za kupindua mifumo siku zote hawaifanyi vikao hadharani. Kingine mfumo wa kitaifa hauwi launched kwa siku moja maana huwa carefully planned and excuted in phases.
Hakuna alieamini kirahisi kuwa April 1994 kungetokea Rwandese Genocide lakini haikuzuia hilo kutokea japo waliofanya speculation na wakakimbia mapema walipona kuliko waliosubiria "KUJUA NA SI KUAMINI"

Huwa siandiki JF politics cause i'm apolitic by nature but that can not remove the love i have for my people. KIKUBWA Nimejibu for the respect i have for you. ONLY THAT
 
Ulimsikia yule aliyesema "Atake asitake, tutamlazimisha tu" na akaungwa mkono na speaker Ndugai, akisema "shikilia hapo hapo, tukirudi hapa hoja iletwe, atake asitake" Sasa wamerudi, tena wako wenyewe bila "wapinga maendeleo", unategemea nini?
Hao wapambe mbona walikuwepo tangu utawala wa Nyerere.

Nyerere alitoa hotuba moja akasema kila alipokuwa akitaka kujiuzulu, wapambe wakawa wanamuambia, Mwalimu, usituache, taifa linakuhitaji sana.

Akawa anaongeza miaka mitano, anasema hii ya mwisho.

Ikiisha, wapambe wanamwambia "Mwalimu, usituache, taifa linakuhitaji sana".
Mwisho akastuka. Akagundua kwamba issue si kwamba taifa linamuhitaji.

Issue ni kwamba hao wapambe walikuwa wanamuhitaji kwa faida zao binafsi. Walikuwa hawajui rais anayekuja atakuwa nani na atakuja na watu gani.

Akawakatalia, akajiuzulu.

Kwa hiyo hizi kelele za wapambe zipo tu.

Lakini je, rais mwenyewe anataka nini?

Rais kashasema hataongeza muda.

Na hakuna factual evidence kwamba ataongeza.

Ni speculations tu.
 
Hatuwezi kubishana bila fact.

Tutazozana tu.

2025 ikifika, Magufuli akastaafu bila kuongeza muda, utasema nini?

Utaomba msamaha kwa kumzushia habari za uongo?

Au utaendeleza uzushi?
Contextual speculation siyo uzushi. That's one.

Two, akiondoka 2025 ndiyo utakuwa mwisho wa speculation.

Three, huku kwetu hatuombanagi msamaha kwenye haya mambo ya siasa.... siyo utamaduni wetu, inajulikana. Tutatafuta tu ku justify kwa nini tuli speculate tulichokuwa tuna speculate - baada ya hapo kila mtu na hamsini zake, tunatafuta topic nyingine ya ku speculate!
 
Mm sina tatizo na magufuli kuongeza muda as long as Wananchi watakaa kimya na kukubaliana na hiyo hali.

Wananchi mamia kwa maelfu Wakiamka na kutaka kumtoa then sitakuwa upande wake.
Tatizo kwa hali ya sasa ambayo CCM inaiba kura na kufunga mitandao, unaweza kuambiwa wananchi wametaka hiki, wakati sicho.

Kama watu wameiba kura uchaguzi wa nchi nzima mpaka wanajikuta wanalazimisha kuwa na wabunge wa upinzani bungeni, utajuaje unachoambiwa hiki ndicho wananchi wanachotaka ndiyo chenyewe wanachotaka na si fake news iliyopandikizwa tu?
 
Mnahangaika kweli na JPM, Watanzania ndio wamemchagua kuwa rais wa awamu ya 5 na 6. Kama mapenzi ya Alhaji Mwinyi yatapendeza basi atapewa zawadi ya awamu ya 7 kama shukrani. Sasa hapo kuna shida gani? Hilo wala halihitaji kupigia kura yaani 2025 kutakuwa na uchaguzi mkuu wa kuwachagua wabunge tu na JPM atapewa shukrani kwa miaka mitano mingine. Kama umechukia jinyonge ndio imetoka hiyo!
 
HAMNA uzito wowote tukiamua sisi ndio wataalaamu....
 
Tqtizo kwa hali ya sasa ambayo CCM inaibq kura nq kufunga mitandao, unaweza kuqmbiwq wananchi wametakq hiki, wakati sicho.

Kama watu wameiba kura uchaguzi wa nchi nzima mpaka wanajikuta wanalazimisha kuwa na wabunge wa upinzani bungeni, utajuaje unachoambiwa hiki ndicho wananchi wanachotaka ndiyo chenyewe wanachotaka na si fake news iliyopandikizwa tu?
Kwangu mm kuukataa utawala ni kuchukua hatua kwenye sanduku la kura, na kama sanduku la kura limenajisiwa basi ni wananchi kwa umoja kupigania kura yao bila woga.

Kukaa kimya ni kukubaliana na hali. Ukiibiwa kura, ukakaa kimya, ukatii sheria basi umeitii mamlaka iliyopo bila kujali imetokana na wizi wa kura au la. Wananchi wakikubali kwa kukaa kimya basi wamehalalisha utawala uliopo, mengine yote yanabaki kuwa nadharia.

Mambo ya raisi wa mioyo, na huzuni sijui malalamiko ya wizi kwenye mitandao yapo kila chaguzi na hayana maana yoyote kiutawala maana hayabadili utawala uliopo.
 
Contextual speculation siyo uzushi. That's one.

Two, akiondoka 2025 ndiyo utakuwa mwisho wa speculation.

Three, huku kwetu hatuombanagi msamaha kwenye haya mambo ya siasa.... siyo utamaduni wetu, inajulikana. Tutatafuta tu ku justify kwa nini tuli speculate tulichokuwa tuna speculate - baada ya hapo kila mtu na hamsini zake, tunatafuta topic nyingine ya ku speculate!
Kwa nini uhitaji kufanya speculation ya aina yoyote kuhusu wizi wa 2025 kwa mtu ambaye kuna ushahidi kuwa kafanya wizi tayari 2020?

This is a waste of time and resources.

Magufuli na utawala wake hawana upungufu wa makosa. Ana makosa kemkem ambayo kashayafanya.

Mnaposhikia bango makosa ambayo mnafikiri atayafanya 2025, mnachofanya ni ku ya minimize makosa aliyoyafanya 2020 kwamba haya yameshapita.

Na kitakachotokea ni kwamba, hata hiyo 2025 akifanya mnachohofia, kwa utamaduni huu wa kuangalia uchaguzi unaokuja na kusahau yaliyopita, mtakubali kwa falsafa za "hewala hewala" na kuanza kubashiri tena "Magufuli atajiongezea muda 2030".

Hizi speculations zisizo na fact wala mkakati zinaondoa focus kwenye mambo muhimu kama kupanga mkakati wa kupata tume huru ya uchaguzi, kudhibiti wizi wa kura, kutafuta katiba mpya, kujiwekea mkakati wa kimataifa etc.

Mimi huwa napenda kufanya kitu kinaitwa "immanent critique".
Yani, katika uchambuzi na mijadala, najiuliza, huyu mtu ninayepingana naye, suppose he is right. Suppose I am wrong, then what?

Suppose the people who say Magufuli will extend his term are 100% right, and I am wrong.

Then what?

Kuna mkakati gani wa kumzuia?

Ukiliangalia hili kwa miwani hii, utaona kwamba speculation hii haisaidii kitu.

Kitakachoweza kusaidia ni kuweka misingi ya kuhakikisha kwamba, rais yeyote, si Magufuli tu, hawezi kujiongezea muda.

Katiba mpya iliyo madhubuti zaidi, kuzidisha elimu ya uraia, kuweka mkakati wa kupata tume huru ya uchaguzi, kudhibiti madaraka ya rais, kuweka sheria na cha muhimu zaidi utamaduni wa uwazi zaidi etc etc.

Hizi speculations tu hazisaidii kitu.

Kwa sababu.

Kuna possibilities mbili hapa.

1. Ni kweli, Magufuli anataka kujiingezea muda. Lakini speculatiins bila mkakati wa kumzuia haisaidii kitu.

2. Hizi ni empty speculations tu. Magufuli hana mpango wa kuonheza muda. Hizi soeculatiins ni a waste if time and energy. Watu wangeweza kujadili wizi wa kura 2020, kuweka mikakati ya kupinga matokeo ya ubunge, kujioanga wasiibiwe tena kura, kudai tume huru, katiba mpaya etc.
 
Kwangu mm kuukataa utawala ni kuchukua hatua kwenye sanduku la kura, na kama sanduku la kura limenajisiwa basi ni wananchi kwa umoja kupigania kura yao bila woga.

Kukaa kimya ni kukubaliana na hali. Ukiibiwa kura, ukakaa kimya, ukatii sheria basi umeitii mamlaka iliyopo bila kujali imetokana na wizi wa kura au la. Wananchi wakikubali kwa kukaa kimya basi wamehalalisha utawala uliopo, mengine yote yanabaki kuwa nadharia.

Mambo ya raisi wa mioyo, na huzuni sijui malalamiko ya wizi kwenye mitandao yapo kila chaguzi na hayana maana yoyote kiutawala maana hayabadili utawala uliopo.
Sasa hapa mbona watu hawajikiti kukataa wizi kwenye uchaguzi wa 2020, kitu ambacho kishafanyika na kina ushahidi.

Wanajikita kwenye kubashiri kwamba Magufuli atajiongezea muda 2025?

Kitu ambacho hakijafanyika na hakina ushahidi.
 
Aongeze hata miaka 100 at the end atajiona amekimbiza tu upepo.
Kama umiliki amani ya moyoni hata umiliki dunia yote ni bure.
 
kama hutaki kuamini, sasa nina uhakika gani hata ukijua utaamini ??...

1. Utamaduni ni mfumo wa maisha, sio static maana hubadilika kutokana na mahitaji ya muda.
Hakuna utamaduni wa Tanzania katika siasa usioweza kubadilishwa iwe kwa ugumu au urahisi mfano Tanzania ya baba zetu ilikuwa rais kukaa zaidi ya miaka 20 na hata baada ya kura za kupigia mfumo wa multipartism bado 80% walipigia monopartism. Multipartism ililetwa kwa Maamuzi ya VETO kwa hiyo tuseme tamaduni yetu ilikuwa monopartism au multipartism

2. Katiba ipi ilifuatwa kwa wabunge 19 kuapishwa pasipo barua kutoka katibu wa chama cha CHADEMA ,

Katiba ipi ilifuatwa kwenye sakata la CAG

Katiba ipi ilifuatwa kwa CAG mpya kuambiwa atafukuzwa kazi na Rais !!!..

3. Aliyesema maendeleo hayana chama na akakiri kuwa hakupeleka maendeleo baadhi ya sehemu kwa kuwa walimchagulia upinzani ni nani ??..

If you cant be consistence with your words, tukuaminije !!!

4. Wapambe sio waamuzi wa mwisho.. mwenye uamuzi wa mwisho ni muhusika japo wapambe mara nyingine hutoa alert

5. Speculations zaweza kuwa na baseless facts lakini haimaanishi ni za kupuuzwa maana wenye nia za kupindua mifumo siku zote hawaifanyi vikao hadharani. Kingine mfumo wa kitaifa hauwi launched kwa siku moja maana huwa carefully planned and excuted in phases.
Hakuna alieamini kirahisi kuwa April 1994 kungetokea Rwandese Genocide lakini haikuzuia hilo kutokea japo waliofanya speculation na wakakimbia mapema walipona kuliko waliosubiria "KUJUA NA SI KUAMINI"

Huwa siandiki JF politics cause i'm apolitic by nature but that can not remove the love i have for my people. KIKUBWA Nimejibu for the respect i have for you. ONLY THAT
Unaelewa hata tofauti ya kujua na kuamini?
 
Sasa hapa mbona watu hawajikiti kukataa wizi kwenye uchaguzi wa 2020, kitu ambacho kishafanyika na kina ushahidi.

Wanajikita kwenye kubashiri kwamba Magufuli atajiongezea muda 2025?

Kitu ambacho hakijafanyika na hakina ushahidi.
Wanajikita mitandaoni kama walivyojikita kutabiri kuwa 2020 uchaguzi hautakuwa huru na haki sababu tume si huru ila uchaguzi ukapita na wakashiriki, baada ya kuibiwa(kama wanavyodai) hawakufanya lolote.
 
Nimeandika hapo juu, kwamba bila mkakati, hata Magufuli akijiongezea muda hiyo 2025, hawatafanya kitu.

Watarukia uchaguzi unaofuatia na kusema "Magufuli atajiongezea muda 2030".

Ni mawazo fulani kama ya kuku anayeweza kufikiri wakati mfupi tu bila kumbukumbu wala mkakati wa muda mrefu.
 
Kwa nini uhitaji kufanya speculation ya aina yoyote kuhusu wizi wa 2025 kwa mtu ambaye kuna ushahidi kuwa kafanya wizi tayari 2020?

This is a waste of time and resources.

Magufuli na utawala wake hawana upungufu wa makosa. Ana makosa kemkem ambayo kashayafanya.

Mnaposhikia bango makosa ambayo mnafikiri atayafanya 2025, mnachofanya ni ku ya minimize makosa aliyoyafanya 2020 kwamba haya yameshapita.

Na kitakachotokea ni kwamba, hata hiyo 2025 akifanya mnachohofia, kwa utamaduni huu wa kuangalia uchaguzi unaokuja na kusahau yaliyopita, mtakubali kwa falsafa za "hewala hewala" na kuanza kubashiri tena "Magufuli atajiongezea muda 2030".

Hizi speculations zisizo na fact wala mkakati zinaondoa focus kwenye mambo muhimu kama kupanga mkakati wa kupata tume huru ya uchaguzi, kudhibiti wizi wa kura, kutafuta katiba mpya, kujiwekea mkakati wa kimataifa etc.

Mimi huwa napenda kufanya kitu kinaitwa "immanent critique".
Yani, katika uchambuzi na mijadala, najiuliza, huyu mtu ninayepingana naye, suppose he is right. Suppose I am wrong, then what?

Suppose the people who say Magufuli will extend his term are 100% right, and I am wrong.

Then what?

Kuna mkakati gani wa kumzuia?

Ukiliangalia hili kwa miwani hii, utaona kwamba speculation hii haisaidii kitu.

Kitakachoweza kusaidia ni kuweka misingi ya kuhakikisha kwamba, rais yeyote, si Magufuli tu, hawezi kujiongezea muda.

Katiba mpya iliyo madhubuti zaidi, kuzidisha elimu ya uraia, kuweka mkakati wa kupata tume huru ya uchaguzi, kudhibiti madaraka ya rais, kuweka sheria na cha muhimu zaidi utamaduni wa uwazi zaidi etc etc.

Hizi speculations tu hazisaidii kitu.

Kwa sababu.

Kuna possibilities mbili hapa.

1. Ni kweli, Magufuli anataka kujiingezea muda. Lakini speculatiins bila mkakati wa kumzuia haisaidii kitu.

2. Hizi ni empty speculations tu. Magufuli hana mpango wa kuonheza muda. Hizi soeculatiins ni a waste if time and energy. Watu wangeweza kujadili wizi wa kura 2020, kuweka mikakati ya kupinga matokeo ya ubunge, kujioanga wasiibiwe tena kura, kudai tume huru, katiba mpaya etc.
Suggest mkakati wa kumzuia ili watu wa stop speculation.
Maana uchaguzi wa 2020 uliporwa kwa nguvu ya jeshi... je, mkakati wa kupambana na jeshi ni upi if I may ask?
 
Nimeandika hapo juu, kwamba bila mkakati, hata Magufuli akijiongezea muda hiyo 2025, hawatafanya kitu.

Watarukia uchaguzi unaofuatia na kusema "Magufuli atajiongezea muda 2030".

Ni mawazo fulani kama ya kuku anayeweza kufikiri wakati mfupi tu bila kumbukumbu wala mkakati wa muda mrefu.
Hakuna utashi mitandaoni, mfano sasa hivi Zanzibar naambiwa raisi kaita watu wawekeze hatojali wala kuuliza walipotoa pesa. Sasa hapa fuatilia wapingaji watapinga bila kuhoji, na wanaosifia watasifia bila kuhoji sababu kupinga kwao ni kazi si utashi na kusifia ni kazi si utashi. Na sidhani kama hizi kazi zina malipo.
 
Back
Top Bottom