Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Unadhani hakuna watu wanaoutumbulia macho URAIS Uganda ama Rwanda !!..

Kutamani ni jambo moja na kutimiza ni jambo jingine. Tamaa ni kama wishful thinking lakini mwisho wa siku mwenye kisu kikali ndiye atakaeweza kula nyama

Personally, Sijali hivyo vyama vitafanyaje lakini kinachoniogopesha ni pale watu wanapokuwa tayari kuvifia ama kuvilinda vyama ama watu kuliko hata nchi yao wenyewe

Tumepotea kama Taifa, Hatudiscuss nchi yetu tena ila kila mtu yupo busy na vyama kama mechi za simba na yanga. Kila mtu anasubiria ushindi lakini ni nani anafikiria kuhusu Future ya hii nchi. HAKUNA
Uganda haina utamaduni wa marais kuheshimu term limits.

Tanzania tangu aondoke Nyerere marais wote wameheshimu term limits.

Na hata Magufuli amesema hatazidisha muhula wake.

Sasa huu mchecheto wa kusema Magufuli ataongeza muda unatokea wapi?
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Magufuli ameshasema hataongeza muda wakubaki madarakani baada ya 2025 acha hofu.
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Lengo la JIWE ni kuendelea kutawala baada ya 2025 ,ndio maana anajenga IKULU dodoma ili akaendelee kujinafasi huko,wewe unadhani anamjengea RAIS wa 2025-2030? Sarakasi zote za Biashara ya utumwa lengo ni kuondoa wapiga kelele pindi akianza kuchezea katiba.

Kwa mwendo wake wa KUKUSANYA MABILIONI through manunuzi nakwambia mpaka 2024 wapinzani wengi watakuwa washafanya BIASHARA ya UTUMWA....Sugu washaanza kumtia jamba jamba ya kumbomolea HOTEL yake ,lengo wamfilisi ili aunge mkono JUHUDI.
 
Katiba itabadilishwa na kutakua shwari Kama ilivyokua ktk uchaguzi huu. Siku Magu anaapishwa nchi nzima ilikua busy na mapokezi ya bi Zari na Diamond.

Kwa aina ya raia wa nchi hii Magu atatawala hadi mola wake atakapomtwaa.
Ninakubaliana nawe kwa asili mia kubwa.
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Kwa Tanzania hii nayoifahamu? Ambapo hata lissu na mbowe wana kadi za ccm! Hebu kuwa siliazi kidogo.
 
Yupo wapi Ben saa nane??Siku hizi na wewe umekuwa wa kulia lia
Vipi mkuu? Umepotea Sana jukwaani kwema lakini?

Hizo tuhuma za kumpoteza Saanane mtoa mada amekuwa akizikanusha sana, kwanini hamuamini utetezi wake?
 
Mtu asiyeona madhara ya kukanyaga katiba ya nchi na sheria zake, bado anaaminiwa kufanya anayosema mdomoni tu?
Mtu asiyetambua haki na uhuru wa watu bado anatetewa kwa maneno ya ulaghai tu anayoyatembeza mitaani?

Kuna kipi kinachofanya wapinzani, wanaoonewa kwa kila hatua wawe ndio watu wa kutoaminiwa kwa vilio vinavyosikika kila sehemu?

Hata kama si mtetezi wa huyo mtesi wa watu unaowalaumu, kuna maswali ya kujiuliza utetezi huu hasa unatokana na nini!
Hata kama humuamini Magufuli, unatakiwa kutomuamini kimantiki.

Ama sivyo, unaweza kubakia unajadili speculations za ajabu.

Kwa mfano.

Je, ni sawa kujadili kwamba Magufuli ataiuza ardhi ya nchi yote iwe koloni la China, kwa sababu tu Magufuli haaminiki?

Where do you draw the line?

Magufuli kashasema hataongeza muda, mnataka afanye nini zaidi muamini hataongeza muda?
 
Lengo la JIWE ni kuendelea kutawala baada ya 2025 ,ndio maana anajenga IKULU dodoma ili akaendelee kujinafasi huko,wewe unadhani anamjengea RAIS wa 2025-2030? Sarakasi zote za Biashara ya utumwa lengo ni kuondoa wapiga kelele pindi akianza kuchezea katiba.

Kwa mwendo wake wa KUKUSANYA MABILIONI through manunuzi nakwambia mpaka 2024 wapinzani wengi watakuwa washafanya BIASHARA ya UTUMWA....Sugu washaanza kumtia jamba jamba ya kumbomolea HOTEL yake ,lengo wamfilisi ili aunge mkono JUHUDI.
Wakuu, hivi ikifika 2025 halafu Magufuli akajistaafia zake mtasemaje?

Mtaomba msamaha kwa kumsingizia makosa ambayo hajayafanya?

Tuwekane sawa, maana hizi nyuzi zinadumu na zinaweza kufika 2025.
 
Mkuu Kama hujamsoma vizuri mleta mada ni MATAGA na ni CCM kindaki ndaki. Huyu ndo aliyeshiriki ktk mission ya kumuondoa Ben Saanane.

Hakuna mpinzani anayeendesha hoja Ukomo ya urais wa Magufuli zaidi ya wanaCCM wenzie ambao tayari wameanza kuota kuhusu 2025 hivyo hawana imani sana naye.
Ningeomba sana akusome uliyemjibu na akuelewe ulichomjibu.

Ahsante sana kwa kuliandika hili kiurahisi hivi ili lieleweke na yeyote akusomae.
 
"If I wasn't on some shit, I'm getting on it"

Jadakiss - "Kiss of Death".

Mstari huu unaelezea hisia za Jadakiss, kama mtu aliyekuwa anasingiziwa sana mambo ambayo hakuyafanya.

Mwishowe akasema, kama sikufanya, sasa nafanya. Mnachonga sana.

Yani, kaona anasingiziwa sana, mpaka akasema, bora nifanye tu kile ninachosingiziwa. Kwa maana hata nisipofanya, watu washaamini kwamba nafanya.

Sasa, msimfanye Magufuli aseme kama Jadakiss.

Kwamba "If I wasn't on some shit, I'm getting on it".

Meaning if he was not going to extend his term, now, because of all this speculations and doubts on his intentions, he is going to extend.

Aah wapi!! Mipango kama ipo ya kuongeza muda ipo, kama haipo hata zikipigwa kilele haipo. Siasa na utawala wa taifa ni mikakati sio mihemko kama ya kina wasanii au mwanamziki yoyote, na hii mada inasemwa semwa sababu kuna wanufaika wanataka iwe hivyo, na kutokea inawezekana hatakama muhusika kasema hataki.
Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza na kuwa celebrity. Mfano wa Mziki wa jaakiss sijui kiss haufit kwenye mazingira haya ya siasa na utawala.
 
Mkuu haujaelewaa hoja yake? Anamaanisha kwamba Raisi atakuwa SAMIA (mwanamke),baada ya Mungu kutovumilia ushenzi wa huyu aliepo Sasa( Sasa sijui akiongea nae[emoji848]).Bawacha hawana hoja ya msingi, ukute yeye ndo atatangulia [emoji23][emoji23]

nimemwelewa sana,anajifanya ana uchungu usioelezeka[emoji23][emoji23].
 
Aah wapi!! Mipango kama ipo ya kuongeza muda ipo, kama haipo hata zikipigwa kilele haipo. Siasa na utawala wa taifa ni mikakati sio mihemko kama ya kina wasanii au mwanamziki yoyote, na hii mada inasemwa semwa sababu kuna wanufaika wanataka iwe hivyo, na kutokea inawezekana hatakama muhusika kasema hataki.
Kuna tofauti kubwa kati ya kuongoza na kuwa celebrity. Mfano wa Mziki wa jaakiss sijui kiss haufit kwenye mazingira haya ya siasa na utawala.
Hilo shairi la Jadakiss ni fasihi, sasa kama huelewi fasihi, kuelewa ni vigumu.

Hapa kuna mambo mawili.

1.Speculation/ ubashiri
2. Fact

Kwenye speculation na ubashiri hakuna mpaka, unaweza kutunga lolote.

Unaweza kusema 2025 tutagundua Magufuli ni mumiani aliyetoka sayari ya Zuhura.

Hakuna anayeweza kupinga hili kwa fact, kama ambavyo huwezi kuthibitisha kwa fact.

Kwa sababu hatujafika 2025.

Halafu kuna facts.

Tuna facts gani za kuonesha Magufuli ataendelea na urais baada ya 2025?

Magufuli amesema hilo? Hapana. Alichosema ni kukanusha hilo.

Magufuli ameanzisha mchakato huo? Hakuna ushahidi wowote.

Sasa mchecheto huu kuhusiana na hadithi zisizo na msingi unatokea wapi?
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba nakurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Ulais kazi nzito ngumu niombeeni kwa mngu nisijawe kiburi, sitoongeza muda wa kutawara
 
Hilo shairi la Jadakiss ni fasihi, sasa kama huelewi fasihi, kuelewa ni vigumu.

Hapa kuna mambo mawili.

1.Speculation/ ubashiri
2. Fact

Kwenye speculation na ubashiri hakuna mpaka, unaweza kutunga lolote.

Unaweza kusema 2025 tutagundua Magufuli ni mumiani aliyetoka sayari ya Zuhura.

Hakuna anayeweza kupinga hili kwa fact, kama ambavyo huwezi kuthibitisha kwa fact.

Kwa sababu hatujafika 2025.

Halafu kuna facts.

Tuna facts gani za kuonesha Magufuli ataendelea na urais baada ya 2025?

Magufuli amesema hilo? Hapana. Alichosema ni kukanusha hilo.

Magufuli ameanzisha mchakato huo? Hakuna ushahidi wowote.

Sasa mchecheto huu kuhusiana na hadithi zisizo na msingi unatokea wapi?
Ok, mm sipo vizuri kwenye mambo ya fasihi za muziki hivyo sawa.
Mchecheto upo unaweza kuwa na sababu kuu mbili.. Kwanza ni kuweka presha kama kuna kusudio la kuongeza muda, au kupima upepo juu ya kusudio la kuongeza muda.
 
Kwanza kabisa, niseme mimi si mtetezi wa Magufuli wala CCM. Ni mtetezi wa haki na mchambuzi wa siasa na mantiki.

Magufuli nishamsema sana, hivyo, ninachoandika hapa si kwa sababu ya kumtetea Magufuli.

Twende kwenye hoja baada ya dibaji hiyo.

Magufuli ameshasema mara kadhaa hataki kuongeza muhula wa urais.

Kwa nini mnafanya hili suala kuwa hoja?

Hususan kama kuna makosa mengi sana ambayo Magufuli ameshayafanya ambayo yanaweza kujadiliwa kama hoja halali, factually, na si speculation?

Mimi naona wapinzani wa Magufuli kuongelea hili kunaonesha yafuatayo.

1. Hawana focus. Wanakuwa kama mtu tajiri mwenye hela nyingi sana (wana hoja nyingi sana halali za kumsema Magufuli) lakini ambaye bado anaenda kukopa hela benki kwa riba kubwa sana (licha ya kuwa na hoja nyingi halali za kumsema Magufuli, wanaenda kukopa hoja qmbayo haina uhalali ya kuhusu makisa ambayo hayajafanyika,kiasi cha kufanya watu wahoji umqkini wao).

2. Hawajadili mambo kwa facts. Bali kwa speculations.

3. Wanahukumu kosa ambalo wanafikiri litatetendeka, badalq ya kuhukumu kosa lililotendeka. Hili ni jambo hatari. Kwa msingi huu, Magufuli anaweza kuamka siku moja akasema ameota wapunzabi wanataka kumpindua. Akawafunga wote.

4. Wanapoteza muda na nguvu kujadili speculations wakati kuna mambo muhimu ya kubana sasa hivi kama wizi wa kura katika uchaguzi, tume huru yq uchaguzi, katiba mpya etc.

5. Wanaonesha paranoia. Kitu ambacho hakifai katika uongozi.
Fahamu tu kuhusu haya machache.
1. Hakuna Dikteta aliyebadilisha katiba ili kuongezewa muda akawa analiongea hilo suala kabla. Mara zote hukana au kukaa kimya wakati vuguvugu likishika kasi. Wanaolisema huwa ni wapambe wa watawala.

2. Suala hili limekuwa likipigiwa debe na viongozi waandamizi na wateule wa Magufuli kwa muda mrefu sasa, na hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na Magufuli mwenyewe wala na CCM.

3. Jambo linalosemwa semwa na watu tofauti tofauti kwa nyakati tofauti kuwa linapangwa kutokea, maana huo mpango upo au huenda ukawepo tu nyuma ya pazia. Watu husema kile wanachokiona, kukisikia au kukihisi.
 
Wakuu, hivi ikifika 2025 halafu Magufuli akajistaafia zake mtasemaje?

Mtaomba msamaha kwa kumsingizia makosa ambayo hajayafanya?

Tuwekane sawa, maana hizi nyuzi zinadumu na zinaweza kufika 2025.
Mkuu tunapenda iwe hivyo lakini kwa plan za JIWE sidhani ila ikitokea 2025 akastaafu itakuwa ajabu sana.
 
Back
Top Bottom