Suggest mkakati wa kumzuia ili watu wa stop speculation.
Maana uchaguzi wa 2020 uliporwa kwa nguvu ya jeshi... je, mkakati wa kupambana na jeshi ni upi if I may ask?
Haya mambo complex, hayana majibu mepesi na mimi sijifqnyi kuwa na utaalamu wa kujua majibu yote.
Ingekuwa ni rahisi hivyo, wengine wangekwishatekeleza utatuzi kwa ufanisi.
Hilo jeshi unalolisema lenyewe limegawanyika. Kuna watu wengi sana jeshini hawaoendi ujinga unaoendelea. Na wengine waliandika moaka "waraka wa jeshi" miaka michache nyuma kupinga uozo wa muelekeo wa nchi.
Kitu cha kwanza kabisa ni kupinga matokeo ya 2020 na ku expose fraud. Kuanalyze makosa ya 2020 na kutafuta utatuzi.
Bila hilo, hata Magufuli asipoendelea 2025, ataweka pandikizi lake litakaloendeleza sera zake.
Hapo ndipo utakapoona ku fight Magufuli asiongeze muda 2025 tu ni smallmindedness. Kwa sababu badala ya ku fight mfumo, mtakuwa mnaishia ku fight mtu.
Na hata Magufuli akiondika, kama mfumo unaruhusu mwingine aendeleze alipoachia Magufuli, mnaweza kusema afadhali ya Magufuli kuliko huyu aliyemfuatia.
Tulikuwa tunamsema vibaya Kikwete hapa, nikawaambia rafiki zangu kwamba siwezi kushangaa rais qtakayemfuatia Kikwete akawa wa ovyo kuliki Kikwete kwenye utawala bora.
Nimetaja baadhi ya mambo hapo juu.
Mkakati unaweza kuhusisha kufungua kesi za uchaguzi kupinga matokeo na kuanika uozo. Yani hata mahakama zikiendeshwa kwa amri kutoka juu, media coverage tu ya uozo itasaidia ku expose mambo.
It is one thing nchi kujua CCM wameiba kura, it is quite another upinzani ku expose hili systematically katika court system, with full evulidence. Halafu kufanya a countrywide and unternational PR campaign kuanika uozo wa CCM walivyoiba kura.
Na kama mahakama za ndani hazitoi haki, mkakati uhusishe kuimulika nchi kimataifa zaidi mpaka watawala watie adabu.
Sasa hivi Tanzania imejitoa Mahakama ya Afrika, kwa kiasi kikubwa ili kuepusha upinzani kupeleka kesi za ku challenge matokeo ya urais (ambazo mahakama za Tanzania haina jurisdictiin nazo). Lakini sinasikia hata mpinzani mmoja akiliongelea hili. Watu wanaongelea Magufuli atajiongezea muda 2025!
Kuna mambo yanayoendana na kuingiliana kama kutafuta katiba mpya, kupunguza madaraka ya rais, kutafuta tume huru ya uchaguzi, kuimar8shq nankushirikishq civil society zaidi, kuwa na utamadunibwa uwazi na zaidi, kuweka utamaduni wa consumer protection.
List ni ndefu sana. Na mimi sina majibu yote.
Hii si kazi ya upinzani tu.
Kuna hata wazee wa CCM kina Warioba, Msekwa, Butiku wanaojiheshimu nanm kuheshimiwa wanaweza kutumika kurudisha mambo fulani yanayoenda arijojo kwenye mstari.
Ila, ninachoona ni utamaduni wa "electocracy". Badala ya democrqcy, tuna electocracy.
Kuanzia CCM mpaka upinzani, watu wako focused kwenye elections tu.
CHADEMA ndiyo kabisa wanajichanganya.Huku wanasemq uchaguzi haukuwa wa huru wala haki, huku wengine wanataka ubunge uliotokana na uchaguzi huo huo.
Ndiyo maana uchaguzi wa 2020 umeisha tu, watu wanaanza kuongelea 2025.
Bila hata kuchambua uchaguzi wa 2020 ulikuwaje, makosa yalikuwa wapi, tuyasahihishe vipi ili tusirudie tena makosa hayo 2025.