Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Itakuwa hivyo kama ndani ya CCM hawatakubali wenyewe wenye connection na deep state.

Shida karata ya kupoteza control ndio itakayokuwa mwanzo wa anguko.
Tusiwategemee ccm kumzuia Magufuli kuongeza muda maana wenyewe kwa sasa kuishi kwao kunategemea jamaa kaamkaje.

Sasa utaweza kuwategemea mateka wamzuie mtekaji wao ?
 
Itakuwa hivyo kama ndani ya CCM hawatakubali wenyewe wenye connection na deep state.

Shida karata ya kupoteza control ndio itakayokuwa mwanzo wa anguko.
After all kama alivyosema Kiranga pale juu hoja ya kuongeza muda kuipa nafasi kwa sasa ni kupoteza muda wakati kuna mambo mengi ya hovyo ambayo tayari ameshayafanya.

Hayo ndiyo tunapaswa kutumia kujenga hoja zetu na kuzifanya kuwa ni agenda za kitaifa.

Badala ya hili la term limit ambayo bado ni speculations tu.
 
Unajichanganya.

Humuamini Magufuli, unafikiri atajiongezea muda wa urais...
Sasa umetoka kabisa nje ya hoja, unatafuta tu visababu vya kuendeleza ubishi.

Eleza wewe, huko ku-'focus' kwenye katiba mpya kwa mtu asiyetaka hata kufuata mbovu iliyopo, utamlazimisha vipi akubali kuwepo katiba mpya?

Unaniuliza "Magufuli kuondoka hapo kunanisaidia nini?" Kwa hiyo kuendelea kuwepo yeye ndio kutakusaidia wewe? Hili swali kabla ya kuliandika hapa umepima uzito wake? Wewe ni kipi hasa kinachokufanya uamini kwamba akiondoka atakuja mbaya zaidi ya yeye? Kwa nini asije kiongozi atakayeheshimu katiba hata hiyo mbovu, kama hataweza kusimamia kutengenezwa iliyo bora!

Hayo maswali yote uliyouliza umeambiwa na nani kwamba juhudi hazifanyiki kiasi cha wewe kukazania tuu hilo la Magufuli kujiongezea muda ndilo liwe sababu kuu ya kuyaacha hayo mengine yote unayouliza hapa!

Magufuli hatumii 'mfumo' wowote ni 'sheer brute force' kuhakikisha kwamba anayotaka yeye ndiyo yawe. Huo mfumo uliokuwepo haukumhimiza akanyage katiba na kufanya mambo nje ya taratibu. Haya yote unayokazania hapa ni kisingizio cha kumfichia utetezi kwa maovu anayofanya.
 
Tusiwategemee ccm kumzuia Magufuli kuongeza muda maana wenyewe kwa sasa kuishi kwao kunategemea jamaa kaamkaje.

Sasa utaweza kuwategemea mateka wamzuie mtekaji wao ?
Ndani ya CCM sasa hivi hakuna mwenye ubavu wa kumzuia chochote Magufuli. Kwanza ataanzia wapi, maana kila aliyepo CCM yupo kwa fadhira ya Magufuli.

Kuhusu mchango wako wa pili hapo juu kuhusu 'speculation' ya Magufuli kujiongezea muda; hivi kuzungumzia tu jambo hilo kunazuiaje kumpinga kwa hayo mengine yanayopendekezwa?

Kusema atajiongezea muda kunamaliza vipi nguvu na juhudi za kuyafanya hayo mengine yote ya kumzuia asijiongezee muda?
 
Ndani ya CCM sasa hivi hakuna mwenye ubavu wa kumzuia chochote Magufuli. Kwanza ataanzia wapi, maana kila aliyepo CCM yupo kwa fadhira ya Magufuli
Mpaka anawaambia vila yeye wasingekuwa wabunge.

Tusiwategemee ccm kwa lolote
 
Sasa umetoka kabisa nje ya hoja, unatafuta tu visababu vya kuendeleza ubishi.

Eleza wewe, huko ku-'focus' kwenye katiba mpya kwa mtu asiyetaka hata kufuata mbovu iliyopo, utamlazimisha vipi akubali kuwepo katiba mpya?...
Umejikita kwenye kumtazama mtu mmoja tu bila kuangalia matatizo ya kimfumo.

This is a strategic mistake.

Kwa sababu hata ukiweza kufanya huyo mtu mmoja asiongeze muda wa urais, kama hujaweza kuzuia abuses za presidential powers systematically, huyo anayezuiwa anaweza kuondoka akamuweka kibaraka wake.

Huja address hii issue.
 
CCM inataka iige mfumo Wa chadema JPM awe mwenyekiti wa kudumu, yajayo yanafurahisha.
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba na kurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili...
Nimetafakari sana Ila bado sijaelewa maana ya kutabiri Kwa maana ya Uzi huu! Tusifanye uchonganishi usio na maana! Fanya kazi Acha kuhangaika!
 
Umejikita kwenye kumtazama mtu mmoja tu bila kuangalia matatizo ya kimfumo.

This is a strategic mistake...
Ndio, sasa hivi hakuna cha mfumo ni "mtu mmoja" ndiye anayeendesha kila kitu. Kama hata hili bado hulijui ni tatizo kwako.

Kabla ya "mtu huyo mmoja" mfumo uliokuwepo pamoja na kuwa mbaya, lakini iliwezekana kuukabili na kuwepo uwezekano wa kufanya mabadiliko bila ya watu kuumizwa kama ilivyo kwa huyu "mtu mmoja" aliyeteka kila kitu kwa kutumia dola.

Chini ya ule mfumo mbaya, wapinzani waliweza kufanya siasa na hata kupata wawakilishi katika ngazi mbalimbali, na hata jaribio la kuubadili mfumo liliweza kuanzishwa kwa uwezekano wa kupata katiba mpya.

Huyu mtu mmoja unayemtetea hataki kusikia lolote juu ya hayo yote.
 
Yaani kwa Tanzania hi na wananchi wake hawa katiba itabadilishwa na ukomo wa kugombea uraisi utatolewa na wala hakuna kitakacho tokeq
 
Kwa hii mbinu CCM waliyoitumia ya kuondoa imani ya wananchi kwa upinzani (rejea covid 19 bawacha) na kufuta upinzani bungeni sitegemei kuona wananchi kuwa concerned sana na ishu za siasa, hivyo tutegemee hiyo hoja ya kurefusha au kuondoa kabisa ukomo itakapoibuka kusiwe na kipingamizi kikubwa.

Matabaka yatakuja kutokea ndani ya CCM yenyewe, na yatachochewa na wale wenye ndoto za kutawala Tanzania. Hao nategemea ndio wataleta resistance ingawa haitakua na immediate effect
 
Ndio, sasa hivi hakuna cha mfumo ni "mtu mmoja" ndiye anayeendesha kila kitu. Kama hata hili bado hulijui ni tatizo kwako.

Kabla ya "mtu huyo mmoja" mfumo uliokuwepo pamoja na kuwa mbaya, lakini iliwezekana kuukabili na kuwepo uwezekano wa kufanya mabadiliko bila ya watu kuumizwa kama ilivyo kwa huyu "mtu mmoja" aliyeteka kila kitu kwa kutumia dola.

Chini ya ule mfumo mbaya, wapinzani waliweza kufanya siasa na hata kupata wawakilishi katika ngazi mbalimbali, na hata jaribio la kuubadili mfumo liliweza kuanzishwa kwa uwezekano wa kupata katiba mpya.

Huyu mtu mmoja unayemtetea hataki kusikia lolote juu ya hayo yote.
Kwa hizi kelele za kijinga za kuangalia mtu badala ya mfumo mtaendelea kulalamika kila siku, wakati wenzenu wanawachezea, wanaiba kura, wanaendelea kuwatawala kimabavu.

Mkiendelea hivi, uchaguzi wa 2025 mtapigwa tena hivihivi, whether Magufuli anaendelea kuwa rais au haendelei is immaterial.

Kwa sababu bila mabadiliko ya msingi, anaweza kupachika mtu wake akaongoza kwa remote control.
 
Anazuga hataki wakati sikuyoyote bunge likianz rasmi huo mswada kuna mbunge atauanzisha nak wakiupitisha atalazimishwa kukubali hapo watanzania dole litakuwa lishatuingia hatuna budi kutulia nalo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha deep state wala jeep! Deep state gani hii ya kufavor chama kilekile kuendelea kudidimiza nchi miaka na miaka? Tena kwa kodi ya wananchi? Wote ni wachumia tumbo tu. Daah!
 
Mkuu,
Kwa hali ilivyo mtaani jambo lolote ambalo halihusu namna ya kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha litakutana na ukingazi mkubwa sana maana hali halisi tuliyo nayo sasa ni "we have nothing to loos by fighting against the tyranny" watujaribu waone!
Mbona walisha wajaribu kwa kuiba kura na hakuna lililotokea?
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba na kurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Hakutotokea lolote lile, watanzania domo kubwa bila vitendo. Wabunge wote ni ccm wakitakacho kitapita tu, ataekataa atafukuzwa uanachama. Wote wanajua kuwa asilimia kubwa yao wameingia bungeni kwa mlango wa nyuma, kwa hiyo watabaki kimya! Ama wananchi wa kawaida ni mahodari wa kupiga domo tu hakuna atakaefanya lolote kuzuia suali hili endapo CCM wakiamua kulijadili.
 
Back
Top Bottom