Natafuta Santuri (CD kubwa za zamani aina ya Gramophone)

Bado natafuta santuri. Kama kuna mtu anazo au anamjua mwenye nazo nanunua. .
 
.
 

Attachments

  • IMG_20220130_204306.jpg
    143.5 KB · Views: 14
Mkuu , nenda Arusha , pale mnara wa saa, pandisha na njia ya Safari hotel kama unaelekea Ofisi za Jiji.

Jengo lapili mkono wa kushoto, utapata hapo.
 
1- 08- 2022
Bado natafuta santuri. God bless.
 
Hiyo mashine inaitwa Vinyl player sio santuri. Santuri ni hizo sahani kwa English zinaitwa Vinyl.
 
Mashine za kuplya hizi kitu huwa zinakuwa na switch ya kubalance speed.
 
Gramophone ni aina ya player sema inakuwa ya zamani a zote zinafanya shughuli moja. Mimi ninayo moja hapa ni ya mzee Philips ya miaka ya 1980's.

Inapiga sahani kubwa na ndogo. Alikuwa na sahani za akina Rwambo, chakachaka, Michael Jackson, Madonna, hawa tabora Jazz Band, Juwata, Elvis Presley, Don Williams, kuna visanturi hivi vidogo vimejaa sana bendi za zamani za Tanzania nashangaa sana namna tulikuwa na wasanii na walikuwa wanarekodi miaka hiyo halafu hawajulikani kwa kizazi cha sasa ukiuliza sana utaambiwa marijani wakati kuna ambao walikuwa wanaimba vizuri sana kumshinda marijani.
 
Hizi nazoziona kwenye picha ni 45 RPM unaona nyingine zimeandikwa 45 RPM. Una aina hii moja tu?
Aaaaah we unataka za speed ya 78rpm kumbe?! player yako kwani hairekebishi speed?
 
Nazunguka sana mwaka wa kumi na moja huu. Nikizipata nyingi huwa ziko badly stired. Kwenye uhifadhi watu walifeli sana. .
Watu hawajui kuheshimu vitu vya enzi. Hii mashine na hizi records mshua alinunua akiwa bado kijana mdogo. Ila leo hii kama unavyoona chombo kipo kinapiga mziki mzuri balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…