Chukua boss. Five years of owning one.
Ila nunua angalau la kuanzia 2011; ukiweza 2014. Hiyo 2nd generation kama pesa ipo chukua ya kuanzia 2016.
XC90 ni bonge la gari. Chukua diesel D5. Hii ni turbocharger na inaweza kufanyiwa stage 1 tuning.
Shida ni moja kubwa. Za kuanzia 2011 zote zinakuwa ni Euro 5 kwenye suala la exhaust emission regulations. Hivyo, kwa diesel zinakuwa na vitu vinaitwa diesel particulate filter (dpf) na exhaust gas recirculation (egr). Hii ni mifumo ya kuzuia uchafu wa mazingira kwenye magari ya diesel. Tatizo linakuja kuwa kama wewe siyo mtu wa kusafiri safiri sana (yaani mtu wa safari za home-work-home za mjini), D5 itakuletea shida. Kwani dpf na egr zitajaa na kuziba zile carbon soot/deposits. Dpf ni chujio la hizo gas mbaya na egr urudisha hizo gas mbaya ndani ya injini ili zisitoke kuchafua mazingira. Dpf na egr zikijaa carbon, hapo a spiral of problems ufuata. Una machaguo matatu manne ya kutibu. Moja ambalo ndiyo bora, uwe unafanya safari za mbali angalau mara kadhaa kwa miezi ili uruhusu exhaust kupata joto la kuchomq vizuri hizo carbon soots. Safari fupi fupi, exhaust haichemki vya kutosha kuchoma carbon. Mbili, kuna additives za kununua na kuweka kwenye mafuta, ambazo ufanya kazi ya kusafisha dpf na egr. Hii ni suluhisho lisilo la kudumu na la gharama, na kwa uzoefu wangu siyo la uhakika sana. Tatu, tumia hizi obd2 diagnostic machines kufanya forced regeneration ya dpf. Pata machine yenye function ya kuruhusu kuipa moto exhaust gari ikiwa imesimama, mpaka carbon soot utoka kwenye dpf. Hii nayo siyo ya kudumu, kwani gari nyingi zinaruhusu forced regeneration mara tatu tu. Nne, fanya dpf na egr deletes. Hizi ni reprogramming ya ecu (control box) ili kuifundisha gari kwamba dpf na egr hazipo tena. Hii inaenda pamoja na physical removal ya dpf. Mara nyingi egr inabaki lakini. Changamoto ya hii ni kupata mtaalamu wa uhakika wa kufanya remapping ya hizi ecu za European makes. Maana remapping yake inahitaji umakini mkubwa mno, makosa kidogo tu, upelekee a spiral of problems. Kwa mazingira yetu ya kibongo hii ndiyo suluhisho la kudumu endapo remapping itafanyika kwa usahihi. Kama pesa si shida unaweza kupelekea ecu Afrika ya Kusini au hata Ulaya. Maana remapping inaweza kufanyika hata kama gari halipo hapo.
Ukiona diesel pasua kichwa chukua petrol. Ila chukua T5 ya kuanzia 2011 au ukiweza T6 ya kuanzia 2016.
Utafurahia sana gari. Ila kuwa makini na mafuta. Jitahidi siku zote uweke kwenye vituo vya Total, Puma, Oryx na Engen tu. Maana European makes na mafuta machafu ni kujitafutia shida. Ingawa unaweza kufanya pia remapping ya kuruhusu gari iweze kuvumilia mafuta ya kiwango duni. Au utumie fuel treatment angalau mara 1-2 kwa mwezi.
Mafundi pia kuwa makini. Wengi wanaweza kusema wanaweza, kumbe ni makanjanja. Hapa ni muhimu kulijua gari lako vizuri haswa. Tembelea fora mbalimbali za Volvo. Cheki mafundi na watalaamu wa Volvo Youtube. Pia kuwa na obd2 yako ndogo ya kuangalia afya ya gari lako mara kwa mara.
Na daima lazima ufanye preventive maintenance. Mfano, ujue kama kuna part ambayo gari likifika umbali fulani, ni lazima ukibadilishe n.k.