Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?


Eti kuhonga michepuko...ila madereva huwa wanapata pesa sana..sema umalaya ndo unawaponza
 
Ila wabongo kwa kurekebisha vitu tumeshindikana tani 5 mpaka tani 18 sio poa kabisa
 
Gharama za kazi hii hutofautiana kulingana na kazi itakayofanywa kwa gari hisika. Fuso zote za tani 3 huitajiwa kuwekewa double chasis ili ziweze kubeba tani 10 kwa single au 16 kwa tandam

Kwahiyo tani 10 ndiyo mwisho mwa single diff?

Jee kama una DAF LF truck yenye GVW 12 tonnes, nayo pia huruhusiwi kuzidisha tani 10?
naombeni elimu hapo, wanaojua mambo ya mizani
 
Kwahiyo tani 10 ndiyo mwisho mwa single diff?

Jee kama una DAF LF truck yenye GVW 12 tonnes, nayo pia huruhusiwi kuzidisha tani 10?
naombeni elimu hapo, wanaojua mambo ya mizani
Kuna kitu inaitwa axle configuration kwa magari yenye GVM zaidi ya 3500, hii ndio huamua gari ibebe mzigo kiasi gani regardless ya engine na uwezo wa gari husika. Mfano gari yenye axle mbili yenye tairi moja moja kwenye axle ya mbele na mbili mbili kwenye axle ya nyuma itakuwa configured as 1:2 na GVM yake utakuwa 18000kg.

GVM ni uzito wa gari pamoja na mzigo uliobebwa kwa hiyo kama gari likiwa tupu uzito wake ni 8000kg (tani 8) basi gari hili litabeba kilo 10,000 (tani 10) na iwapo gari hilo likiwa tupu uzito wake ni tani 10, basi mzigo itakaoruhusiwa utakuwa tani 8.
 
Uzi unamadini huu.basi tu lakini nyuzi kama hizi ni za kuzitunza hazina kabisa.
Ila kuna bingwa mtaalam wa haya mambo hajaja hapa sijamuona.

Huu uzi una mafunzo basi watu wanachukulia poa,,,, mungu awabariki waliotoa mawazo chanya.
 
Je nikiwa na gari yenye configuration hiyo ya 1:2, lakini GVW ya gari ni tani 7.5, Jee gari hiyo pia mwisho wake kubeba ni tani 18?
 
Naomben uzoefu wenu
Scania ambayo mende yake imetengenezwa na waswalihili Tabata na kwingineko ,
Performance yake barabaran ikoje?
Ni ya kuaminika?
Asanten
 
Je nikiwa na gari yenye configuration hiyo ya 1:2, lakini GVW ya gari ni tani 7.5, Jee gari hiyo pia mwisho wake kubeba ni tani 18?
Kwa axle configuration ya 1:2 GVM yake ni 18000kg (tani 18) na GVM ni uzito wa gari pamoja na mzigo uliobebwa. Ili kujua mzigo unaoweza kubebwa chukua GVM (kwa kuangalia axle configuration husika) toa uzito wa gari likiwa tupu.
 
Vip kuhusu magar ya TATA, REUNALT, KENWORTH, PETERBILT na VOLVO yenyewe yapoje kwenye ulaji wake wa mafuta na maintenance?
Kwa mwenye uzoefu atusaidie kufafanua.
 
Asante kwa maelezo yako. Ni kweli biashara yoyote ni kujitolea muda wako kwa asilimia zote, hasa nchi kama yetu yenye culture ya watu kupenda kusukumwa kama ng'ombe. Kwa upande wa gari ndiyo zaidi kabisa. Bila wewe kuwepo mwenyewe kuwepo lazima utaumizwa.

Ukitaka kujua biashara ya usafirishaji imejaa watu wenye ''ubongo wa kupenda kuiba'' wewe nunua chombo cha usafiri kwa ajili ya biashara halafu ambatana nacho mara kwa mara.

Utachukiwa na dereva na hata watu wa pembeni. Utasikia wanabeza ''tajiri gani habanduki kwenye gari''. Nchi yetu ni nchi pekee watu mfanyakazi anachukia tajiri kusimamia kazi yake.
 
Kuna siku niliongelea kuhusu bei za Scania 93 na model za aina hyo kuwa unaweza kuchukua kwa bei ndogo na ukaifanyia service ila baadhi ya wanajamvi waligoma kuwa sikuwa sahih kwenye bei.

Sasa chuma hiyo hapo kesho mungu akipenda tunaenda kuilipia kwa milion 17 tu, baada ya hapo inaingia garage moshi ikitoka huwez kuifaham.

NB: kama ni mgeni na chuma usijaribu kununua kwa mfumo huu.View attachment 1502384View attachment 1502380View attachment 1502382View attachment 1502383View attachment 1502381
 
Scania? Moshi naona wako njema .. HP ngap mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…