Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Wiki hizo nilikuwa nafurahi sana kusafiri na tajiri!

Akiwepo kwenye gari tunakula na kulala hotel, changamoto yoyote inashughulikiwa kwa wakati na muda mwingine alikuwa akinisaidia kuendesha gari!

Kwa kifupi sigusi posho ya safari!
Kwa scenario kama hiyo ningeanzaje kuchukia tajiri kuwepo kwenye gari?

Dereva anaehudumiwa vizuri haibi! Ukiona unaibiwa ujue umeweka mbele ukali/ujeuri usio na maana/na ukorofi wa kipuuzi kuliko kuboresha mazingira ya kazi ya dereva wako..

Kwa tabia hizo utaibiwa, utaibiwa, utaibiwa mpaka uchakae hata kama unalala kwenye cabin!

-Posho unatoa kidogo tena kwa masimango!
-Dereva anaweza kukaa foleni hata siku nne, akihitaji umuongezee pesa ya matumizi anaambulia matusi!

-tairi ikipasuka unamlipisha! Na mambo mengine ya hovyo hovyo mengi tu kwanini usiibiwe? Kwa nini usiibiwe?
 
Naweza pata wapi mafunzo ya ufundi wa scania?
 
Naweza pata wapi mafunzo ya ufundi wa scania?
Kama ni mtaani naweza nikakupa a,ba,cha,da...
Lakini kama ni chuoni, nakushauri utembelee VETA iliyopo karibu na wewe.

Ingawa ufundi wa hizi chuma unanoga zaidi ikiwa utajifunzia kitaa, na unaanza kuwa alwatan mazima. Pia utapata kujitengenezea wateja polepole(sio wa sisiem), na usije ukatarajia kuajiriwa kwa kwenye hii fani.
 
Hapo ndipo watanzania tunapokosea kama umepata kwenye vanilla kwanini hiyo 100M usiwekeze zaidi kwenye vanilla

Kama ulikuwa na shamba la hekari 10 kwanini usiwe na shamba la hekari 100 hujui kumiliki ardhi na shamba ndio utajiri mkubwa nchini
 
Hapo ndipo watanzania tunapokosea kama umepata kwenye vanilla kwanini hiyo 100M usiwekeze zaidi kwenye vanilla

Kama ulikuwa na shamba la hekari 10 kwanini usiwe na shamba la hekari 100 hujui kumiliki ardhi na shamba ndio utajiri mkubwa nchini

Yani wewe ndo unakosea kabisa..,kwanza sidhani kama mleta maada kasema kaacha kulima. Pili, ukwasi mara nyingi unaletwa na chanzo zaidi ya kimoja cha mapato, mkuu wewe hujui kwamba kilimo ni moja kati ya biashara zisizotabirika KABISA???! au haijawahi kulima? hivi unafaham kwamba pamba msimu uliopita ilinunuliwa sh 1200 na mwaka huu mkulima kauza kwa sh 850???!.Bado hujalima wewe😁
 
kama ni hivyo leo cargill wangekuwa wanatengeneza ndege..the issue is kama ni line ya business inatwist but you dont change the industry ndio maana Hp wana laptops, pc na printers different businesses ila the same industry

mie ni muumini wa ku stick kwenye the same industry angekuwa ni mzungu angetoa m30 kwenye research and development ya new method of farming ya vanilla na hapo ndio inakufanya uwe the best katika biashara, ila eti unalima then kesho una duka la hardware kesho kutwa una sijui nini ni mwanzo wa kufilisika .. anaweza kuwa inspired by bakhresa na mo lakini those guys are conglomerate na huwezi kuwa conglomerate lazima the previously business uwe na track ya revenue inayoeleweka. na huajiri consultants wa maana wakitaka ku put their hands in the new field

Naweza kuwa sijawahi lima ila am damn good katika business ... sasa kilimo cha vanilla na transportation company ni industry ipi iko very complicated?
 
Mawazo ya kijinga.Si ajabu wewe ndio biashara unafanya na hutaki wengine wafanye.Hao walioweza wana nini yeye ashindwe.Watz ni kikatishana tamaa tu.
Ukitaka kuanzisha business yoyote halafu ukaomba mawazo kutoka kwa watanzania automatically hiyo biashara hutaianzisha kamwe utaghairi tu endapo utaamua kuchukua ushauri wao 90% watakukatisha tamaa na 10% ndio watakupa moyo uendelee, sijui watanzania tukoje yaani kwani hao wanaoifanya wana nini na kwa nini umkatishe tamaa mwenzako?

Though tunafahamu kila biashara ina changamoto lakini huwezi kuogopa kuingia humo kwa sababu ya changamoto ni lazima uingie ili upambane na hizo changamoto na utakapozishinda ndio mafanikio yanapoanzia. Tusitishane wala kukatishana tamaa wakuu akifanikiwa yeye itakuwa ni fursa pia ya kusaidia wengine na wanaweza wakawa hata ndugu zako pia.
 
Marehemu ,mzee Mengi aliwahi kuulizwa kwanini Watanzania hawakui kiuchumi alijibu akasema Watanzania wana tatizo la KUKOSA UTHUBUTU WA KUFANYA JAMBO.
 
engine mpya za 113 zinapatikana?
 
nasikia malawi magari yanauzwa kwa bei rahisi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…