Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Mkuu mimi sio mtaalamu wa magari wala sijawahi kufanya biashara ya magari lakini nimeukubali sana ushauri wako. Watu wanadanganyana sana mitaani kuhusu biashara za magari wakidhani ni rahisi kama wanavyofikiria.
 
Inategemea mkuu.
Usifanye kitu kwa kuwaiga wengine, fanya kitu pale inapobidi kufanya kutegemea na uwezo wako.
Biashara ya magari haina urafiki na mtu maskini, risks zake ni nyingi sana na zote zinahitaji pesa.
Matajiri wanaiwezea kwa sababu wanakuwa nazo nyingi so ikianguka moja wala hashtuki anajua atazitumia zingine na kupata pesa za kuiokoa iliyoanguka.
Tanzania yapo magari mangapi?? yote yametumbukia ? biashara zote zina risk mkuu, na zote zina risk za kuhatarisha na kuua mtaji wote , ndio maisha yalivyo, tuna options mbili tu either tufanye au tusifanye
 
Hapa umeeleweka
 
Mkuu sorry, hiyo fuso tandem inapatikana kwa bei gani hapa Tanzania ikiwa used na haijachoka?
 
Ina maana gharama ya mafuta haizidi laki tatu?
 
Mkuu mambo yalivyo tofauti kabisa na wewe unavyofikiria, kila biashara inarisk zake.

Kuna mtu ana roli moja tu ama mawili na mambo yanaenda.

Eti kwa sababu kuna ndege imeanguka ikateketea basi mwenye wazo la kuanzisha biashara ya anga ahairishe!!?
Lori limetumbukia mtoni basi watu wasifanye biashara ya maroli kisa kuna lori liliingia mtoni!!?
 
Mtoa mada kama kweli kilimo cha vanilla kimeweza kukupatia mil 100 nakushauri endelea tu na kilimo.

Kuhamia kwenye biashara ambayo huijui tena ya magari hii inaweza kuwa ndo downfall yako na baadaye kwenda kwenye uzi uleeeee wa waliowahi kushika pesa ndefu halafu ghafla zikapotea.

Hili ni wazo tu lakini maana kuna wengine wameweza kubadili biashara pia wakafanikiwa.
 
[emoji1][emoji1]
 
Kweli ndugu Tabutupu tunaomba utupe muongozo umetoboa vipi kwenye vanilla
 

Nakushauri uendelee kulima vanila, uko unakotaka kwenda muda si mrefu utaingia kwenye imani za kishirikina, kwani yatakayokusibu kuhudumia hilo gari utasema umelogwa.
 
Scania ni Gari Nzuri sana
Tatizo kubwa kama ilivyo kwa biashara nyingi ni hulka ya Watanzania kutokupenda kazi na kuiheshimu. Hulka hiyo chafu iko kila sehemu.

Dereva wanaiba sana tairi na mafuta na kama huna Proper management atakumaliza.

Tatizo ninaloona kwako ni mtaji mdogo maana ukinunua hiyo R 440 kwa bei za Dar itasoma 80 Flatbed used nzuri ni 25 hapo unasoma 105.

Bado hujanunua Tairi say labda unaweka super single na zile zingine za deef ziko 4.

Baada ya muda utaona kabisa mtaji wako huo hautoshi nashauri uwe na 115. Ili ubadili tile zote za horse na pia ukate bima kubwa turubai na vitu vidogo kama jack na wheel spanner.

Jitahidi kuweka mpango mkali wa kuimanage hasa mafuta na tairi andika uwe na daftari unaandika. Kingine hakikisha unasaka maduka ya spea unaulizia spea.Kama hujui spea na zinapouzwa utaibiwa sana utafilisika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…