Najazia hapo, kamwe usithubutu kununua gari USED ya mizigo au ya biashara ikiwa wewe ndio unaanza.Gari ya mizigo/biashara kwa beginner yeyote usijelogwa ukanunua used bongo , usijelogwa .. nunua used bongo ikiwa tayari ww Ni expert
Kwa hakika Tandam ndio best.Shukran, kwa mtu anae anza moja kabisa unamshauri achukue ipi kati ya Tandam na kipisi?
Hapana Tandam ipo juu ya kipisi, kwa maana kipisi kilichosimamia kucha unachukua kuanzia milion 25 hadi 32.Ni cheaper kidogo chini ya kipisi
Hongera mkuu, ama kwa hakika umepambana.Mimi hii kitu naijua nje ndani yani mkuu kuanzia kuendesha nilijipatia uzoefu najua mipigo ya madereva najua faida najua vimeo
Na ni kweli inawezekana kuanza na gari moja mie nilianza na Tani 2 ya Mazda Titan miaka Mingi nikaja Kenta 3.5 Fuso Tandam/Kipisi ambacho saiz ni Mende na nna Semi za Howo . Mungu akisaidia ntatafuta Pulling ila sio Scania
Na hizi price nazoona mitandani huko mbona naona kama zinafika over 60milHapana Tandam ipo juu ya kipisi, kwa maana kipisi kilichosimamia kucha unachukua kuanzia milion 25 hadi 32.
Hali kadhalika Tandam kuna wengne wananunua hadi million 70, 80, had 90.
Ni miaka mingi kidogo mkuu sio leo na janaHongera mkuu, ama kwa hakika umepambana.
No Dear, alisema alilinua kwa 15m i think kisha akalifufua hadi kufikia 83m, kwahio siku ile ndio ilikua trip yake ya kwanza tangu kulifufua na kwamba dereva alishalalamika kuwa kulikua na hitilafu.....Lakini alisema lile gari jipya ndo trip ya kwanza.
Nasikia ilikuwa safari yake ya kwanzaKuvuja kwa mafuta ya breki na kuisha/uchakavu wa breki pads/shoes, ndio common problems ambazo hupelekea breki kufeli.
Hapana mkuu huingii chaka ila tu vitu vinapatikana kutokana na mazingira na kujuana na watu, kwan gari ambayo wewe utainunua kwa milion 10 mie naweza kuipata kwa milion 4.Na hizi price nazoona mitandani huko mbona naona kama zinafika over 60mil
au hua naingia chaka?
Mkuu ngoja nikuoneshe kuna Canter ambayo sasa hv inapga kazi ila kiukwel imetugharimu kama milion 6 tuu kuifufua na kuifanyia kila kitu hadi rangi.Na hizi price nazoona mitandani huko mbona naona kama zinafika over 60mil
au hua naingia chaka?
nimefanya saabscania Miaka kedekede Kama bingwa wa scania lete hapa tukupongeze ama kukukosoaHuyo hajui systems za breki chief.
Siku nikipata muda, nitakuja nitowe somo la jinsi upepo unavyo fanya kazi kwenye systems za magari hasa Scania
Kwa kuwa wewe ni mmiliki naomba nisaidie kabla sijaenda field nikapigwa.Mimi nilianza biashara ya Usafirishaji miaka kama 10 iliyopita. Hata sasa hivi nafanya usafirishaji mizigo sana tu local ila kwakua imenibidi(Niko kwenye supply business) kwahiyo swala la kuwa na Gari linasaidia kupunguza gharama ya bidhaa nnazouza.
Ila kama ingekua ni uamuzi wangu nisingekuja kumiliki gari la mizigo tena KAMWE
Hio mil 100 tafuta biashara nyingine sio ya kuwa na gari moja.Ni Risk kubwa mno unajitafutia .Hakuna cha bima wala upuuzi wa bima .Utakufa siku sio zako
Ukiwa na magari mengi inasaidia kugawanyisha Risks. Madereva nao dahh kila siku ni kutishana na bastola mezani na kutiana lockup
Hakuna biashara pasua kichwa kama hii katika biashara zote nilizokwisha kufanya
Usione kina Usangu,Overland wanazungusha chuma tu kisauzi ila hii biashara sio mchezo.
Ungekua na mtaji wa Billion plus ningekushauri hata uanze kupambana na kina Sham Nunu na hao underdogs wengine na nisingekushauri huko kwenye Mascania. Howo anafanya vizuri sana saivi anaenda ligi za kina Daf/Volvo
Ukichukua wateja utatupata huku huku.Mkuu, ushauri nimeuvhukua na ufanyia kazi
Siku hizi teknolojia imeendelea unafatilia kila kitu ukiwa chumbani kwako.Dereva anapeleka mzigo mkoa wa rukwa ikifika wakati wa kurudi anakwambia hamna mzigo.kumbe kapakia tani saba za mahindi anapeleka manzese kushusha.
Hizo fuso tandam unakodisha? If yes Moshi Dar sh ngapi? Na makubaliano yakoje?Mkuu mie nakushauri anza na Fuso Tandam ndio utapiga pesa zaid. Ninakushauri hvo kwa kuwa hapa home tuna Scania tatu na Fuso mbili ila Fuso ndio zinapiga kazi kuliko Scania.
Na pia km ni Scania kwa wewe unaeanza sikushauri kwa kuwa ni sumbufu sana hasa ikishaanza kuchoka. Scania za kukutoa umaskini ni zile model za kizaman.
Na pia wanaokushauri kuhusu magari ya abiria naomba usiwasikilize kabisaa, maana yana changamoto nyingi sana. Mie binafsi nina Nissan Caravan mbili ila ni kichefu chefu kitupu.
NB: nimekushauri kutokana na uzoefu wangu wa kuishi na hayo magari kwa muda mrefu.
Lakini kwa nini mnawakatisha watu tamaa kwamba R hazifai achani hizo wewe mwambie tu kama ana nunua mtumba achague mzuri tu sasa hizo 113 zenyewe zinapotea saa hizi kuzipata kwenyewe kwa shida113 & 124 spare zapatikana kiurahisi na gharama nafuu. Kuliko hizi P.G.R. series gharama na ufundi ni pasua ukichwa usipo kuwa makini
Hata mitano haifiki halafu likifa halitengenezekiHamna gari humo, ukizitumia muda mrefu ni miaka mitano (probably haifiki) kati ya mitatu na mitano... hizi scania, Volvo, benz mjukuu wako anazikuta bado zinapiga route ya dsm lubumbashi