Nataka kununua router ya Airtel ila mitandaoni malalamiko ni mengi kuhusiana na network yao, naombeni ushauri

Tangu lile tukio la kukatika nyaya bajarini ni kama mitandao imeathiriwa hadi sasa..Kuna mda Network inashuka kabisa then inarudi ili ni suala dogo kabisa huwa inaweza kuwa down kwa dakika kadhaa siku nyingine inakuwa down kwa Masaa kadhaa then inarudi

Sio Airtel ni mitandao karibia yote...Mkuu kama uwezo upo nunua iyo router inasaidia Sanaa usisikilize ya Mtandaoni yatakukatisha Tamaa wewe jivike Mabomu jilipue Ukanunue utafurahia
 
Usilongwe. Airtel ni hovyo kabisa kwenye internet.... Ukitoka maeneo ya mjini tu kwisha Habari..
 
Km upo nje ya mji chukua Ttcl fiber hapa inabidi uhonge iliupate huduma mapema toka Kwa mafundi hutajutia
 
Nyuki hakumbatiwi hata yanga wanajua
Sumu haionjwi hata waliopona kufa wanajua
Kuna baadhi ya maeneo iko okay lakini kingine ni majanga
 
Kuna jamaa anayo anasema iko poa japo mimi mwenyewe niliahirisha kuchukua sababu ya kuona malalamiko mengi mtandaoni...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…