Nataka kununua router ya Airtel ila mitandaoni malalamiko ni mengi kuhusiana na network yao, naombeni ushauri

Nataka kununua router ya Airtel ila mitandaoni malalamiko ni mengi kuhusiana na network yao, naombeni ushauri

Mitandao yote kuna siku huwa lazima i-freeze, itasumbua masaa kazaa then inakaa sawa lakin sio kila siku.

Airtel Router package ya 70k ambayo ni 270k is much worse kuliko maelezo, Ipo slow na downloading speed haizidi 2 Mbps, (Wameandika 10 Mbps lakin haifiki).

Package ya 110k is a way better na naweza mshauri mtu atumie, ipo faster na downloading speed inafika mpaka 6 Mbps, (Wameandika 30 Mbps lakin hazifiki).

Note: Kama unaona 110k ni nyingi kulipia peke yako kwa mwezi basi nunua router then ongea na wapangaji wenzio upate angalau watu 3 muchange.
Kuna Mbps (megabits per second) na MBps (Megabytes per second). Speed inayotangazwa na ISP ni Mbps lakini speed ambayo utakayokuwa unaiona ni MBps.
8 Mbps = 1 MBps
10 Mbps = 1.25 MBps
30 Mbps = 3.75 MBps
 
Labda hivyo, ila unlimited naona ni much better.

Nimejaribu kuomba fiber ya ttcl ila kama kawaida yao, mwezi sasa hawajaja.
Yani mwezi tu 🤣, unaweza kata mwaka hao hata na zaidi
 
Kwa upande wangu naona mtandao wa Vodacom unajitahidi sana.

Nina 5G router yao na nimejaribu kuitumuia sehemu mbalimbali na ipo vizuri. Ninaitumia karibia miaka miwili na zaidi sasa.

Sehemu ambapo hakuna 5G inatumia 4G.

Pia baadhi ya router zao zina "band locking feature", hii inasaidia sana kama upo sehemu ambapo watumiaji kwenye mnara ni wengi.

"Customer service" yao pia ni nzuri.

Nilijaribu mitandao mengine haikuniridhisha.
Hii Ni Ile ya Sh ngapi?? Na Bando lao kwa mwezi Linakaaje??
 
Back
Top Bottom