Nataka Kuoa japo sijui Namuoa Nani? Mwanaume mwenzangu umeshawai kutokewa na hali hii?

Kemea hilo pepo mkuu, Shukuru umefanikiwa kufika miaka 35 bila attachment, don't try to ruin the rest of your life. Neno langu sio sheria.
 
Oya wanawake wote hawa unashindwa kupata mmoja tu wa kuoa?
 
Ndugu yangu hongera.
matamanio yangu ufanikiwe kwa kikamilifu hitaji lako hili.
Binafsi nilipata shida sana wakati nilipoamua kuoa, mpaka nakuja kupata wa kumuoa iligharimu miaka mitatu ingawa nina muda wa kutosha wa kutoa uzoefu baada ya kuoa lakini sikufanikiwa kikamilifu, ila kwa vile binadamu haturidhiki moja kwa moja hata ningepewa nafasi nyingine ya kuoa bado kuna mahali ningeona kukosea tena, so kilicho baki ni ile kauli mbiu yetu ya kuvumiliana.

Sasa ningekua sijaoa halafu nahitaji kuoa kamwe nisingeoa mwanamke ama msichana wa mjini.
Ningeenda ama kijijini kwetu ama maeneo ya kijijini kabisa, huko ningeongea na wazee vijana wenzangu, wakina mama na hata viongozi wa kiimani waniunganishe na familia yenye binti afaae kuoa, kama ningefanikiwa kwa hilo nitakavyokuja naye mjini kuendelea na maisha, huyo binti mpaka jua la mjini limpambazukie tutakuwa tayari familia imefika mbali .

Natamani kuwa shauri hivyo vijana wenzangu.

Lakini pia ukipata binti mwenye asili ya mkinga Mbena ambae bado asili haijamuacha sana please weka vigezo vyako vyote pembeni mchukue huyo.

Ufanikiwe ndugu yangu.
 

Nakuelewa sana mkuu. Umakini muhimu sana..usije weka ndani kurumbembe..kahaba mstaafu akakupiga matukio ya kufa mtu..ukajutia
 
Ni lazima, hii ya kufichaficha imekaa kizamani sana...sahivi mwanaume anataka ajue mwanamke anajishughulisha na nini na kiasi gani anapata na kwa mwanamke vivyohivyo.....la sivyo utachina sana mkuu


Wanawake na mambo ya vipato ni chanda na pete
 
Hapo kwenye umri ingependeza awe mdogo kulinganisha na umri wako heshima itakuepo ndani milele
 
Hapo kwenye umri ingependeza awe mdogo kulinganisha na umri wako heshima itakuepo ndani milele

Hata uzazi pia. Mwanamke mdogo atamzalia watoto. Familia itakuja.. mwanamke wa age yake 35 uzazi ishu
 
Huo ni umri hatari sana kutafuta mke mtoa mada…. Ulipaswa uwe na candidates walau wa3 uchague mmoja, ila from no where tu…..

Hata hivyo nikutakie heri… kama una imani omba Mungu sana wakati huu.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…