Nataka Kuoa japo sijui Namuoa Nani? Mwanaume mwenzangu umeshawai kutokewa na hali hii?

Nataka Kuoa japo sijui Namuoa Nani? Mwanaume mwenzangu umeshawai kutokewa na hali hii?

Mi pia nipo kwenye hali hiyo natamani kuoa lakini sijui ntamuoa nani
 
Wala haihitaji kuumiza kichwa, kama ni mzinzi na muasherati utaowa mzinzi na muasherati mwenzako tu.
 
Ndugu yangu hongera.
matamanio yangu ufanikiwe kwa kikamilifu hitaji lako hili.
Binafsi nilipata shida sana wakati nilipoamua kuoa, mpaka nakuja kupata wa kumuoa iligharimu miaka mitatu ingawa nina muda wa kutosha wa kutoa uzoefu baada ya kuoa lakini sikufanikiwa kikamilifu, ila kwa vile binadamu haturidhiki moja kwa moja hata ningepewa nafasi nyingine ya kuoa bado kuna mahali ningeona kukosea tena, so kilicho baki ni ile kauli mbiu yetu ya kuvumiliana.

Sasa ningekua sijaoa halafu nahitaji kuoa kamwe nisingeoa mwanamke ama msichana wa mjini.
Ningeenda ama kijijini kwetu ama maeneo ya kijijini kabisa, huko ningeongea na wazee vijana wenzangu, wakina mama na hata viongozi wa kiimani waniunganishe na familia yenye binti afaae kuoa, kama ningefanikiwa kwa hilo nitakavyokuja naye mjini kuendelea na maisha, huyo binti mpaka jua la mjini limpambazukie tutakuwa tayari familia imefika mbali .

Natamani kuwa shauri hivyo vijana wenzangu.

Lakini pia ukipata binti mwenye asili ya mkinga Mbena ambae bado asili haijamuacha sana please weka vigezo vyako vyote pembeni mchukue huyo.

Ufanikiwe ndugu yangu.
Ngoja niujaribu huu ushauri wako mkuu. Tabora, Mara, Dodoma nina ndugu na Iringa kwa Wakinga na Wabena nina ndugu pia. Ngoja niingie mzigoni kumsaka wife pande hizo.
 
Habari wadau.

Kuna hali inanitokea inanishangaza sana, nimekua na hamu na ndoa ghafla since mwaka jana. cha kushangaza sasa sijui namuoa nani na nipo 35 yrs.

Wanaume tunatumia nguvu kubwa kujitafuta na kulea wadogo zetu na wazazi wetu mpaka tunasahau kuandaa spouse. Hapa wanaume tunakosea sana.

Najiona kabisa nitazeeka bila familia kwa uzembe wangu. wazee wa kupoint mnisaidie connection na wadada mnaowajua wenye vigezo.

Wasifu wangu

1. Mwanaume miaka 35, muajiriwa sekta binafsi
2. Kipato kidogo japo wengine wanaita cha kati
3. Makazi Dar es salaam
4. Elimu ya chuo kikuu
5. Dini Mkristo Anglican

Wasifu wa Mwanamke naependa awe nijenge nae familia

1. Elimu isipungue kidato cha nne, awe na uwezo wa kuchanganua mambo kutambua facts na bullshits, sense na non senses. Wazungu wanasema awe open minded
2. Awe mkazi wa Dar es salaam,
3. Awe mkristo. hata kama akiwa dini nyingine awe tayari kuishi kwenye ukristo
4. Awe mrefu mrefu maana nami ni mrefu mrefu
5. Awe hajawai kuolewa ama kuzaa
6. Umri asiwe mdogo sana na wala asiwe mkubwa sana wa kunizidi umri

WENYE VIGEZO AMA KAMA UNAMJUA MWENYE VIGEZO KARIBU UNISAPOTI MWAKA HUU TENA USIISHE BILA BILA
Nakupa Siri moja tu ukimpata Patna nae

Akikuudhi nenda zako Rudi saa nane usiku Na mitungi ya kwenda.
 
Mi nakuelewa japo sio mwanaume.
hata sisi kuna mda tunatakaga kuolewa ila wakuolewa nao hatuwaoni
 
Back
Top Bottom