Nataka nikusanye kiasi cha million 25, nitumie mbinu gani?

Vicoba nishacheza nikachemka m-wekeza na Utt kwa target ya muda mfupi naona ugumu flan hivi vipi mkuu hakuna njia nyingine hata ya kienyej naweza itumia kusave
 
Sina matumizi makubwa sana almost ninachokipata mwisho wa mwezi kinaweza seviwa chote au nikatoa kidogo mimi sio muajiriwa ni mfanya biashara hiyo take home nimemaanisha faida kwa mwezi ukitoa mtaji na cost za ku-run biashara kwa mwezi
kama ni mfanyabiashara hiyo faida kwann usiizungushe ikaongezeka kuliko kuiweka tu mkuu
 
25M ndani ya muda gani ?
 
Kama huakika unapata 800k kwa mwez unan uwezo wakutumiaga 200k tu na 600k ukaiweka kwenye acc maalum apambo iyo 600k × 12=7200000 kwaiyo itakubid upambane ndan ya miaja mitatu na nusu adi minne apo kama umechagua kupata 25m kwanjia ya mshahara na posho zakazin kwako ila kama utaruhusu kuongeza njia ni chap tu
 
Hela ya kuweka huwa haiongezeki mkuu.

Ukiipata hela, Ipe kazi, itume ikakuletee hela nyingine.


Fungua biashara ambayo mtaji wake ni mdogo sana katika hiyo 500k unayopata kwa mwezi inaweza kuwa 50k au 100k

Kopesha kama una uhakika itarudi.

Unaweza uka bet katika moja na mbili kuituma hela yako.


Ukisema uiweke kwenye kibubu haikui bali inadumaa
 
Biashara inahitaji maandaliz mkuu ukikurupuka kisa una balance 1m iko pending na huna kazi nayo mda huo basi uanzishe tu biashara unaweza poteza zote na nyingine unazopata zihudumie hiyo biashara hadi isimame

Umenichukua miaka 6 kufikia faida hiyo katika kazi ninayofanya na bado kuna miezi mingine naambulia patupu
 
Ushauri mzuri nafikiria kufungua account ya bank niweke nione kama nitavumilia kutochungulia huko
 
Tafuta nyoka mkuu, wanapatikana Morogoro na Sumbawanga
 
Muda sio shida sana shida ipo kwenye kuweza kusave hadi ifike hiyo maana nimejaribu mbinu moja mwaka mzima nimejikuta patupu japo walau miaka mitatu na isizidi miaka minne
kwa huo mshahara hauwezi kusave ndani ya huo muda hadi ufikie 25M maana hata ukisave 600k ambayo ni mshahara wako wote bado itachukua miaka 3, chakufanya, iweke kwenye kitu kingine mfano biashara ili ikue japo na risk pia inaongezeka
 
- Huna Familia? Kwa sababu kwa hayo malengo yako utasababisha familia kula chakula kidogo,Cha hali ya chini, hutaweza kuwanunulia nguo nzuri,na ww pia hutaweza kula Wala kuvaa
 
fungua akaunti benki then uifungie ndani ya miaka mitatu usiweze kutoa hela, uwe unaweka tu. weka lengo kuwa kila mwezi uhakikishe umedeposit kiasi fulani, pia hela zinazopita bila malengo unazitupia huko hata kama ni buku

mfano wa account ni Malengo account ya NBC
 
huko vicoba, m wekeza atakula mkuu, si umeona alianza kucheza kikundi aaishia kusolve matatizo yake
 
Hivi NBC na NMB vs CRDB ipi bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…