Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Hahahahaha, eti Kenya yote!
Kuna graduate dropper yaani mhitimu msaka ajira zikabuma, leo ni milionea alianza na kuku 3 tena alipewa na shangazi yake alifaulu kuwamanage wakaazaana na kuongezeka ana supply mayai na kuku Kenya yote.
 
Hongera sana, vipi mbolea ya kuku wa mayai inapatikana?
Ngoja nikupe mchanganuo wa mradi wangu wa broilers

Hapa sijaweka eneo ambalo nilinunua milioni 20 kiasi cha Sqm 5900...
 
Kuzalisga sawa ila kuwalisha ndo utakwama hapo. Labda uwe na pori lakufikia eka 5 hadi 10 then fuga kwa kuwaachia wajilishe wenyewe
Hata eka 10 haitoshi kwa kuku laki moja. Afanye jaribio tu kuku 500 awaweke kwenye eneo la ekari 5 aone wanavyotawanyika na kusambaa shamba lote. Kumbuka kuku wa kienyeji kama hauna mazingira ya wao kujilisha kwenye nyasi na wadudu huko nje kama unategemea mfuko wako lazima ulie.

Tatizo ni muda mrefu wa kuwahudumia kabla hawajaanza kukurudishia hela na hapo uombe magonjwa yasiwapitie.

Hilo eneo la shamba hata iwe kubwa kiasi gani, watakula siku ya kwanza na ya pili baada ya muda itabaki ardhi isiyo na hata jani moja, hapo sijasemea msimu wa kiangazi ambapo hakuna majani
 
Kila jambo kabla ujalianzisha utatakiwa uwe na way out na way forward , pili strategic plan iki ni kitu muhimu sana maana utajiona wapi unakwenda , tatu technical know how (ujuzi wa fani husika) mleta Uzi alisema waliokuja kupata huduma mashineni walileta magonjwa kuku wakafa Moja Kwa moja akujua kuhusu biosecurity measure, nne kwakuwa alishafuga kidogo Kuna vitu alishanote some details hivyo Kwa sasa akianza tena na vifaranga 300-500 hataweza fikia malengo yake .Dunia Ina fursa za kumtosha Kila mtu.
 
Yaani bana watu Kama wewe yaani wewe kushindwa kwako Basi unajua naye Ni Kama wewe. Tunatofautiana mkuu. Motivation yako sio ya kaangu
Ila ndyo ukweli kuku 15 kufika 1000 cio leo na sio kimahesabu ya kichwa tu
 
Nimecheka sana.Vijana wanatoka shule wakiwa na motivated na mitandao.Mwambie ajaribu kuku 100 kwanza,ndiyo ataelewa Somo ni kwa nini watu hatufugi Kuku wa kienyeji kwa idadi ya broiler
 
Nimefikisha kuku 2000 mpaka sasa. Japo nilipata changamoto hapo kati, ila safari ndo imeiva hivi sasa. Nimetenga tray 10 kila siku za kuhudumia kuku wote. Mpaka ndoto yangu itimie.

Karibu tule vijogoo vya kuchoma na mayai ya kuchemsha kwa mama mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…