Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

Hivi mmejaribu kupiga hesabu? Kuku laki 1 siyo mchezo!
1 chicken x 130g x 30days = 3900g or 3.9kg
For 100,000 chicken it will be 390000kg kwa mwezi sawa na tani 390 za chakula cha kuku! Au tani 13 kwa siku sawa na mifuko 260 ya 50kg! Siyo mchezo! Bora jamaa yangu angekuwa na lengo la kuku 10,000
 
Nimefikisha kuku 2000. Je ni leo sio leo? Acha nikufungue kidogo tu mkuu. Ukitaka kubadilisha maisha yako, anza kuota ndoto kubwa kubwa. Hata kama hutazifikia, lakini kuna hatua utakua umepiga
Mwaka 2015 nilienda kumtembelea mtu mmoja hapo Mbalizi, ni mbali kidogo, unaingia njia ya Utengule, alikuwa na Kuku elfu saba(7000) wa kyenyeji.

Lengo lake alisema anataka Kuku elfu kumi, aanze kuuza mayai tu. Mkuu uko sahihi shida Kuna watu wakishindwa wao wanaamini Kila mtu hawezi.
 
Unapiga hesabu in a wrong way Mkuu, Kuku wa kyenyeji wanajitegemea Kwa wadudu. Pumba zipo Mkuu, Kuna viwanda vingi vya UNGA siku hizi kupata pumba za mwezi mzima is easily possible. Pia hao Kuku atakuwa anawavuna periodically, hivyo gharama ya kuwalisha haipo. Watu wanafuga ng'ombe mamilioni, sembuse Kuku.

Mkuu try to think differently you will be more successful. Venture difficult path you will breakeven.
 
Watu wenye mindset hii duniani huwa masikini milele. And i bet hapo ulipo hata laki 3 hauna uhakika nayo NA AJABU U HAVE GUTS za kumkatisha mtu tamaa kwenye jambo ambalo kaamua na kuliwaza kwa njia zake. LOW MINDED KABISA
 
Watu wenye mindset hii duniani huwa masikini milele. And i bet hapo ulipo hata laki 3 hauna uhakika nayo NA AJABU U HAVE GUTS za kumkatisha mtu tamaa kwenye jambo ambalo kaamua na kuliwaza kwa njia zake. LOW MINDED KABISA
Nadhani sio wote mkuu, maana kwa tafsiri ya Maskini kama tuijuavyo hapana me sio Maskini labda uwe na tafsiri ingine

Bahati mbaya kwa asubui hii ni kweli hiyo Laki 3 mkuu SINA Kama ndio kipimo chako cha utajiri, ila sidhani kama kuna business man anakaa tu na hela ndani ili awe anaziangalia

Pia mkuu labda tu nikukumbushe kuwa ninazo Gut's sio Tu za kusema ukweli bali ninazo, Gut's za kufanya pia, sio kama wengi wenu keyboard warrior mlivo, hujawahi kufuga ata njiwa unataka kushauri kuhusu Kuku 100,000

Na mwisho kabisa, zingatia mtoa mada alivorudi karudi na same story ya kuku laki moja au karudi na kuku elf mbili? alafu kamuulize kachange wazo kwa sababu ya comment yangu unayoiita ya kukatatisha Tamaa au kachange kisa ukweli ambao amekutana nao Field
 
Akiweka chochote hapa kinachoendana na hicho anachosema mimi najipiga ban! Huyu mwamba ni aina fulani ya motivesheno spikazi!
 
Hawajui kama inawezekana ukiwa na nia. Shida yetu watanzania tunaogopa kuzikabili changamoto
 
Hawajui kama inawezekana ukiwa na nia. Shida yetu watanzania tunaogopa kuzikabili changamoto
Kibaya zaidi mtu anakaza kuwa haiwezekani. Wengine ni wakatisha tamaa watu, siyo vema kuwaamini na kuyatendea KAZI. Unaweza usifanikiwe kabisa
 
Upo sahihi kabisa. Target ilikua ni kufikisha kuku laki moja ndani ya miaka mitatu. Lakini kwa hali ilivyo na mazingira niliyopo, kufikisha kuku laki moja kwa wakati mmoja ni ngumu.

Kwa hapa nilipofikia, angalau nauona mwanga wa maisha nisiwe muongo.

Ila kama mradi utakaa sawa hivi hivi kwa muda mrefu kidogo, basi nitajipanga mpaka nije nifikishe hao kuku laki moja aisee
 
Nimefikisha kuku 2000 mpaka sasa. Japo nilipata changamoto hapo kati, ila safari ndo imeiva hivi sasa. Nimetenga tray 10 kila siku za kuhudumia kuku wote. Mpaka ndoto yangu itimie.

Karibu tule vijogoo vya kuchoma na mayai ya kuchemsha kwa mama mkuu
Kwahiyo tunakudai kuku 98000 aisee si mchezo. Endelea kupambana. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu naomba mawasiliano yako nikutafute tushauriane mimi pia natamani kufuga
 
Nimekupata vizuri mkuu, ata hao sio haba unaejitahidi sana

ila kama hutojali kuna sehemu nimekuomba utuwekee tupicha picha ili tujifunze baadhi ya vitu kutoka kwako

Kama vile layout ya mabanda yako, vile unalea vifaranga wako,vile unawawekea maji na chakula kuku wako

Na mwisho kabisa kuna sehemu ulisema ushapata Dawa ya MDONDO, kwa tujuavyo wengi wetu huo ugonjwa hauna dawa ispokuwa chanjo tu

Sasa kama mfugaji mwenzetu umepata dawa ya MDONDO nadhani ni vizuri ukashea nasi ili tujifunze, na kupita wewe utaenda kuokoa hasara kubwa ambazo wafugaji wenzio wanazipata kutokana na athari za ugonjwa wa MDONDO
 
Okay....
Ipo hivi mkuu. Sehemu ninayofugia ilijengwa maalum kwaajili ya project ya zao la kahawa. Yaani eneo la kukoboa, kuloweka, kuosha, kuanika na kuhifadhi.

Eneo hili lina maghala makubwa matatu na mashimo ya kulowekea hizo kahawa. Mwenye eneo ni uncle ila alimpa mama aishi hapa yeye na familia yake. Pana fence kubwa sana na mradi wa kahawa kwa sasa, uncle ameuhamishia sehemu nyingine ambako ni makazi yake.

Hivyo, niliporudi niliiona fursa ya eneo hili ambalo lina maghala matatu, mashimo yaliyosakafiwa na fence kubwa. Fursa niliyoiona ni ufugaji wa kuku wa kienyeji maana ni nafuu kwenye kuwasimamia.

Hivyo kuku wangu nawafugia kwenye haya maghala. Yaani wanalala humo na kutagia humo ila masindo yao ni nje yaani ndani ya fence.

Vifaranga nawalelea kwenye mafactory ya kusindikia kahawa ambayo hayatumiki. Nawaweka pamoja na mama zao kwaajili ya kuzalisha joto mwezi mmoja.

Nawapa broiler starter ndani ya mwezi mmoja wanakua wanaweza kujitegemea.

Kuhusu dawa, hapo pana ukakasi maana ni sawa na kutoa formula ya kitengeneza soda, bia na vitu kibao. Hata nikikutajia, inaweza niletea shida kubwa. Ingekua physical mimi na wewe, ningekuonyesha
 
kuku wamefika wangapi kwa sasa mkuu
 
Sawa Mkuu Kwa maelezo hayo nimekupata in term ya structure ya mabanda unayotumia

ila sijaona uhusiano wa uliopo kati maghala unayotumia kufugia kuku wako na kutoshea picha zake

Me niliomba Kwa niaba ya wengi tuone vile unalea na kufuga kuku wako maana sidhani kama kuna ubaya, mwingine nayeye anaweza akawa na hayo maghala ila hajui namna ya kuyatumia kwenye ufugaji na ukawa umemsaidia

Na kuhusu Dawa ya MDONDO sidhani kama ukisema hivo ni Sawa, ingekuwa hivo basi kipindi cha Corona watu wangeuchuna tu na kushuudia ndugu zao wakifa ilhali kuna dawa wao zinawasaidia

Unless otherwise watu tutaamini umeamua kutupiga kamba Tu kama kamba zingine maana hakuna ulicho prove hadi sasa, yani ujue dawa ya ugonjwa usio na dawa na usitake kushea ili upate faida gani?

Kama hutojali mkuu, sie tunaomba tu ushee picha za mradi wako tujifunze na muhimu zaidi hiyo dawa ya MDONDO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…