Natakiwa kumfukuza kazi muajiriwa aliekuwa kwenye kampuni kwa miaka 17, Nifanyeje?

Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Tekeleza order za wakubwa wako
Lakini hakikisha una evidence za maagizo hayo ili kukulinda huko mbeleni.

MPe darasa muajiriwa anaweza kudai haki zake CMA
 
Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Wewe ndio HR kwanini waboss wakuagize umfukuze?na kwanini watoe hukumu wao?Hamna kamati ya nidhamu?

Je kabla ya kumfukuza umefuata utaratibu wa kisheria wa kumwajibisha mtumishi?Yaani

Mmefanya uchunguzi
Mkampa mashtaka
Akajibu
Mkampa muda wa kujitetea
Mwisho disciplinary commitee ikaamuakwamba kosa lake ni la kufukuzwa?

Nakashauri,fuata utaratibu wa kisheria wa kutoa adhabu kwa watumishi,kumbuka mtumishi analindwa kisheria.

Mambo yakifika mahakamani utawajibika.
 
Hiyo miaka 17 aliingiza
nn mwenye kampuni?
Every thing happen for a reason Mungu hutafuta njia yoyote kukupeleka anakotaka mambo ya kulazimisha abaki akaja kupata majanga?
Mpe
 
Hapo kwenu hakuna idara ya sheria?,kama ipo,hebu mueleze haya mawazo yako na takwa la uongozi juu ya huyo mfanyakazi .
 
Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Huyo ni kama Kaka yako yupo kwenye game kitambo. Fanya mumpitishie msamaha
 
Kazi yako ni si kusimamia nidhamu ya Wafanyakazi tu, bali kulinda maslahi yao pia.

Washauri Maboss zako wakueleze ni kwa nini wanaona kumfukuza mhusika kazi ni jambo jema kwa taasisi yenu. Kisha washauri ni njia gani nzuri ya kumuondoa. Waambie wasubiri mpaka mwisho wa Mkataba kisha wasirenew.

Je, ni kosa hilo ndo haswa linamfukuzisha au wana sababu nyingine tofauti?

Lakini siku zote kufanya kazi kwa viwango, kukaa kwako muda mrefu si kinga ya wewe kuondolewa. Bali ufanyaji wako wa kazi. Fanya kwa bidii kiasi kwamba unakuwa na jeuri ya kuondoka, Mkurugenzi na vigeregezwe wake wote wanakulilia kukubembeleza.
 
Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Ushauri

Mimi pia ni.mtaalamu wa mambo haya.

Jambo la Kwanza

Pitia makosa yake yote wanayomtuhumu.
Mwisho washauri Viongozi wako kwa kosa hili huyu jamaa ataenda mahakamani na itailazimu kampuni kumlipa pesa nyingi sanaaa.

Hivyo ni vyema mkampa worning letter .

Ushauri wangu ndio huu
 
Kama hutaki tutakufukuza wewe
 
HR bila shaka umesoma business ethics na pia unaelewa kuwa kuna wakati unapaswa kusimamia kile unachoamini ni moral right hata ikimaanisha kubakia peke yako.

Kujiamini katika majukumu yako kama afisa utumishi ni pamoja na kusimamia haki za wafanyakazi wako na ku-harmonize hali za wale wanaokandamizwa au kuumizwa na wenye nguvu zaidi yao na ndiyo maana unakalia kiti hicho lasivyo department yako isingepaswa kuwepo ikiwa kazi yake ni kufukuza na kuajiri tu na siyo kulinda haki za wafanyakazi,maslahi, mienendo na kuimarisha mahusiano mazuri kazini.

Tumia mbinu yeyote ile kumbakiza mfanyakazi hodari kama huyo katika himaya yako, aidha msimamishe kazi,au mkate mshahara (au vyote viwili ili mradi mabosi waridhike) na umwite umweleze kile ulichopaswa kumtendea, huku ukiendelea kumwombea msamaha kwa mabosi kama kuna mfanyakazi haeleweki na ana madhambi kadhaa unaweza mfanya escape goat kumnusuru huyo mfanyakazi.

Njia nyingine ni kutafuta wakukuunga mkono katika jambo lako, jaribu kuchunguza ni nani anaweza ku-side na wewe katika kushinikiza jamaa asifukuzwe kazi ikiwemo bosi ambaye zinaiva, wafanyakazi wenzake au mtu wa nje ya taasisi ambaye ana nguvu fulani yakuweza kumkingia kifua, ila vyote vikishindikana muue nyani kistaarabu huku ukimwangalia usoni kwa kumwita kistaarabu ofisini na kumwelezea kila kitu kinagaubaga kisha mlime barua.
 
Ushauri

Mimi pia ni.mtaalamu wa mambo haya.

Jambo la Kwanza

Pitia makosa yake yote wanayomtuhumu.
Mwisho washauri Viongozi wako kwa kosa hili huyu jamaa ataenda mahakamani na itailazimu kampuni kumlipa pesa nyingi sanaaa.

Hivyo ni vyema mkampa worning letter .

Ushauri wangu ndio huu
Kesi za CMA/Mahakamani zinachukua mpaka miaka 10
 
kufukuzwa kazi inauma sana, najua unapata ugumu sana namna ya kumwambia maana usiopofanya hivyo nawe kazi huna, sasa njia rahisi kwa akili yangu piga naye stori hapo na umueleze hasara za kuajiriwa yaani mjaze mpaka akubali kuajiliwa ni kubaya ukimuona amejazika na amekubaliana na wewe hapo ndipo unamwambia ukweli sasa, na unamuonyesha chimbo jingine la kujiajiri kwishaaaaaa
 
Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Fuata sheria...

Sent from my vivo Y67 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom