Natakiwa kumfukuza kazi muajiriwa aliekuwa kwenye kampuni kwa miaka 17, Nifanyeje?

Natakiwa kumfukuza kazi muajiriwa aliekuwa kwenye kampuni kwa miaka 17, Nifanyeje?

Soma Sheria ya Kazi.
Cheki code of conduct
Angalia company policy
Weka kosa mizani then km halina mantiki muandikie warning letter tu coz akienda mbele badae utalumiwa wewe tena kwa nn hukuishauri management vizuri.
 
Oral warning mbili na written moja on same kosa lapse of 6 months jichanganye mshtakiwe mlipe mamilioni na wewe utafuatia kufukuzwa trust me. Simamia haki usibembeleze urafiki na kaisari
 
Habari wana JF, Mimi ni HR wa kampuni fulani kwa miaka 2 sasa. Nimepewa order na maboss zangu kumfukuza mfanyakazi ambae amefanya kazi kwenye kampuni hii kwa miaka 17. Amefanya kosa ambalo ni la kusamehewa tu ukiangalia na muda aliojitoa kwenye kampuni hii.

Bado hajui chochote na kwangu imekua ngumu kumwambia, NIFANYEJE wadau?
Wewe ni HR. Fuata sheria ya ajira na mahusiano kazini.
Kama wamemchoka, basi waache kumtafutia zengwe. Wavunje mkataba. Mbona rahisi.
 
Ukiachana na zengwe la kuonewa, wakati mwingine na sisi Wafanyakazi tujitathmni. Huwa tunalalamika sana kuwa ma-boss wenye kazi zao wanatuonea hasa private sectors, ila ukweli tunaouficha ni kuwa wengi wetu tuna matatizo yetu mengi sana kazini. Yaani unakuta tunafanya kazi kwa mazoea na hatujali kabisa kuhusu productivity kazini. Tubadilike aisee.!
 
Kama sio murder case, ubadhirifu au safegurding policy issue nadhani kuna taratibu za kufuata. Kama kweli wewe ni hr nadhani unajua steps za kumfukuza mtu kazi. Je kuna barua ya onyo alishapewa?
 
We una miaka miwili tu, unajuaje aliyofanya kwa hiyo miaka 15 mingine? Pengine wamemvumilia wamemchoka
 
Soma Sheria ya Kazi.
Cheki code of conduct
Angalia company policy
Weka kosa mizani then km halina mantiki muandikie warning letter tu coz akienda mbele badae utalumiwa wewe tena kwa nn hukuishauri management vizuri.
Sawasawa 👍 👍
 
Every one can be replaced....Kuna kipindi....
Nilitakiwa nifukuzwe kazi ila replacement yangu ilikua ni ngumu...Kila replacement hai work out....
Ni kama kum tafuta mbadala wa Lionel Messi....
Waeleze asemehewe tu utaangalia response yao kama wametaka afukuzwe basi ndio moja ya kazi yako uliyoajiriwa Hapo hio huwezi jua kuna mtu mwengine Mungu anataka ampe riziki hio ajawai kufanya kazi hata mwaka 1 na ana mahitaji
...
 
Wewe ni HR uliyesomea? Basi unajua utaratibu wa kisheria wa kufukuza mfanyakazi.
Ili mtu wafukuzwe anahitajika
kwanza kupewa onyo la mdomo
Pili kuandikiwa barua ya onyo
Tatu kusimamishwa huku anapokea nusu mshahara
Nne kufukuzwa.
Waelekeze maboss utaratibu ulivyo.siyo kukurupuka tu.
Coz huyo mkongwe hapo kazini akifukuzwa nje ya utaratibu akienda mahakama ya kazi taasisi itatumia.
 
Simamia taaluma yako, ikiwezekana wafukuze hao mabosi zako kazi, utakuwa umetengeneza legacy, kuliko kuwa 'cheap labour' kufanya nje ya taaluma yako kwa kuwasikiliza hao wapiga majungu.​
 
Back
Top Bottom