Ningependa kuwaona ndugai, Mwigulu na Msukuma, wakipigwa chini huko majimboni. Maana hawa wamelewa madaraka sana.
Chadema tutapata wabunge sehemu nyingi hapa nchini. Mikoa ya Mara, Katavi, kagera, Rukwa, Mbeya, Arusha, Dsm, Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Singida, Morogoro, Manyara kigoma (kwa upinzani hata kama sio chadema) na Geita. Huko mchuano ni mkali.
Tanga, Dodoma, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Shinyanga, Njombe, Pwani, na Tabora huko tukipata hata mbunge mmoja itakuwa ni bonus. Kwa tathimini pamoja na mazingira magumu na figisufigisu hatutakiwi kukosa wabunge 50+. Na hao inabidi tukaze kweli kweli.