Natamani kujua muda sahihi wa Wakristo kufuturu

Nimecheka sana. Ila ni hivi kwa Mkristo siyo lazima afunge kula kipindi hiki cha Kwaresma. Anaweza kuamua kuacha jambo fulani sana sana starehe kama vile kula nyama akawa anakula tu mbogamboga au kufanya jambo fulani la toba. Au akawa hali chakula ila anakunywa tu maji kwa muda aliojipangia. Na mara nyingi inaendana na maombi ili kujiweka karibu zaidi na Mungu.

Fun fact, Mkristo anaweza kufunga hata siku 3 bila yaani hali chochote mfano kuanzia jumatano anakuja kufungua/kula ijumaa. So funga ya sisi Wakristo inaweza kumaanisha mambo tofauti tofauti sana wala usiumize kichwa kujiuliza sana. Huyo mzee yuko sawa tu.
 
Tatizo unaungalia ukristo na funga yake kwa jicho la uislamu na funga(ramadhani) yake
Kufunga si lazima iwe kula tu, umeieleza vizuri kuwa anaiangalia funga ya Quaresma kwa jicho la Kiislamu ilhali kumbe mtu anaweza hata akafunga kuachana na smartphone tu kipindi hicho cha 40days na ndiyo ikawa funga yake.
 
Hili sasa ndio jibu sahihi.

Ibada za Wakristo hazina asili kutoka kwa Yesu, ndio maana hazieleweki. Na kila mmoja anafanya anavyo jua na hii si sawa.

Hapo ukimuuliza Mkristo, mafundisho ya ibada yenu mnayatoa kwa nani hawakupi majibu.

Sababu wanajinasibu na Yesu, ilitakiwa kila jambo wanalolifanya liwe limefundishwa na Yesu moja kwa moja.
Pale msalabani alimaliza kila kitu 👌. Sisi wenzako tushanunuliwa kwa damu ya thamani sana.
 
Habarini wakuu, mimi uhuru one nataka kujua muda sahihi wa wakristo kupata kifungua kinywa baada ya fungwa ya kutwa nzima.

Tukumbuke Ramadhani hii imeambatana na ndugu zetu nao wanatimiza funga ya kwa RESMA ila nataka kufahamu namna ya kufuturu, kwanini nimeuliza hivi???

Nipo kariakooo pale, lakini ofisi zote za pale tupo changanyikeni wakristo kwa waislam, ila kwa upande wa wakristo namuona mzee mmoja wa makamo ndio anaofunga tuu.

Sasa huyu mzee wa makamo alivyoonza tukawa tunafuturu wote pamoja, ila kuna siku ananishangaza kidogo anafuturu hata saa 5:50 jioni.

Yaani akimuona tu yule muuza futari anapita kuchukua oda basi mzee anamwambia niletee na kwemi baada ya dakika 10 futari imefika mzee anafuturu ukiangalia saa ni 5:45 au 5:55.

NINACHOWEZA SEMA KWAMBA HUYU MZEE KUFUTURU INATEGEMEA NA MUUZA FUTARI KAPITA MUDA GANI, YAAN HANA MUDA MAALUM WA KUFUTURU.

Ndio nimekuja na jambo hili nataka ufafanuzi wenu wakuuu

Waluofunga huu mfungo unaoitwa kwaresma sio wa Kristo. Hao ni wa Roma. unadhani wakatoliki ni wa Kristo?
 
Mkuu binafsi nimekuelewa.
Angalau naweza kujifunza kitu.
Sasa mwongozo wa kufunga kwa mwenendo huo upo kimaandishi au inakuwaje, maana kila mmoja kati ya jamaa zangu ninayemuuliza naona ana majibu tofauti.
Tufafanulie japo kwa uchache
Kibiblia hakuna andiko linalotoa muda sahihi sasa mimi niliamua kumuuliza padri mmoja akanijibu kama nilivyokujibu kwamba mkristo wa kweli anatakiwa awe na ile ratiba yake ya chakula cha usiku kikawaida bila kuibadili kwa kisingizio chochote. Nilipouliza zaidi alinijibu fanya lolote lakini siku ikibadilika ikukute umeshakula alafu uendelee hivyohivyo mpaka jua likizama ndipo unaruhusiwa kula tena.

Nilipombana zaidi alinijibu utaratibu huo unawabana wakristo watakaotaka kuamka saa kumi asubuh au saa 11 wale daku kitu ambacho kitakua ni kama kumkejeli Mungu sababu kipindi hawajafunga walikuwa hawaamki muda huo kula.

Kwa kifupi tarehe ikishabadilika hutakiwi ule tena.... Fikiria umekula ukashiba saa kumi asubuhi au saa 12 kasoro asubuh utahesabuje umefunga wakati mchana wote umevimbiwa?

Yote kwa yote kila mtu ana maamuzi yake

Natamani dada Setfree atie neno katika hili ili kuwasaidia waumini wenzake 😊
 
Mkristo anaweza kufunga hata siku 3 bila yaani hali chochote mfano kuanzia jumatano anakuja kufungua/kula ijumaa. So funga ya sisi Wakristo inaweza kumaanisha mambo tofauti tofauti sana wala usiumize kichwa kujiuliza sana. Huyo mzee yuko sawa tu.
Siku tatu bila kula chochote si inawezekana nikafa mkuu?😁
 
Kwa hiyo hizo dk 15 bila shaka unazomhuku mwenzako ndo unafikiri zitakufikisha kwa mabikra 72?? Mungu hafungwi na haya maigizo ya wanadamu - tutende mema, tusaidiw watu - menginefanya sirini na Mungu wako
 
Kuna wakristo wengine kufunga si kwamba anacha kula bali anabadilisha mlo tu. kwa mfano kama asubuhi kila siku kula yake ni chai ya maziwa na chapati 3, mchana ugali nyama na vimboga vya majani kdg,basi badala ya kula hivyo anakuwa asubuhi anakunywa kikombe chake kimoja cha uji na mchana hivyo hivyo mpk muda wa kufungua unapo fika basi anaendelea kula mapocho pocho🍗🧃
 
Pale msalabani alimaliza kila kitu 👌. Sisi wenzako tushanunuliwa kwa damu ya thamani sana.

Hakuna dini ya hivyo kijana, na kila mtu atabeba mzigo wake.

Hakuna kubebewa mzigo yaani Wakristo sijui akili zenu mnazitumia kwa mambo gani ?

Hakikisheni mnapata mafundisho sahihi aliyoyafundisha Yesu kuhusu dini yenu, sio kina Paulo.
 
Mimi ninaokaa nao wamechukua ratiba ya Waislam....daku na futari na wajua kabisa adhana ya futari bila hiyo hawali
 
Waluofunga huu mfungo unaoitwa kwaresma sio wa Kristo. Hao ni wa Roma. unadhani wakatoliki ni wa Kristo?
Roma ndio kanisa mama, hili utake au usitake.

Ukristo umehifadhiwa na Roma, nenda Italy na Vatican utaiona mpaka sanda ya Yesu, na kaburi la Petro wamehifadhi wao, hiyo Biblia wameandika wao, sasa niambie wewe unajiona mlokole una kipi ulichohifadhi kinachohusiana na Ukristo, Biblia yako ni version gani? Au Hellen G White version?
 
Habarini wakuu, mimi uhuru one nataka kujua muda sahihi wa wakristo kupata kifungua kinywa baada ya fungwa ya kutwa nzima.

Tukumbuke Ramadhani hii imeambatana na ndugu zetu nao wanatimiza funga ya kwa RESMA ila nataka kufahamu namna ya kufuturu, kwanini nimeuliza hivi???

Nipo kariakooo pale, lakini ofisi zote za pale tupo changanyikeni wakristo kwa waislam, ila kwa upande wa wakristo namuona mzee mmoja wa makamo ndio anaofunga tuu.

Sasa huyu mzee wa makamo alivyoonza tukawa tunafuturu wote pamoja, ila kuna siku ananishangaza kidogo anafuturu hata saa 5:50 jioni.

Yaani akimuona tu yule muuza futari anapita kuchukua oda basi mzee anamwambia niletee na kwemi baada ya dakika 10 futari imefika mzee anafuturu ukiangalia saa ni 5:45 au 5:55.

NINACHOWEZA SEMA KWAMBA HUYU MZEE KUFUTURU INATEGEMEA NA MUUZA FUTARI KAPITA MUDA GANI, YAAN HANA MUDA MAALUM WA KUFUTURU.

Ndio nimekuja na jambo hili nataka ufafanuzi wenu wakuuu
Hawana mda maalum wakihisi njaa tu wanapakia shehena kwa tumbo
 
Hakuna dini ya hivyo kijana, na kila mtu atabeba mzigo wake.

Hakuna kubebewa mzigo yaani Wakristo sijui akili zenu mnazitumia kwa mambo gani ?

Hakikisheni mnapata mafundisho sahihi aliyoyafundisha Yesu kuhusu dini yenu, sio kina Paulo.
🙄🙄
 
Habarini wakuu, mimi uhuru one nataka kujua muda sahihi wa wakristo kupata kifungua kinywa baada ya fungwa ya kutwa nzima.

Tukumbuke Ramadhani hii imeambatana na ndugu zetu nao wanatimiza funga ya kwa RESMA ila nataka kufahamu namna ya kufuturu, kwanini nimeuliza hivi???

Nipo kariakooo pale, lakini ofisi zote za pale tupo changanyikeni wakristo kwa waislam, ila kwa upande wa wakristo namuona mzee mmoja wa makamo ndio anaofunga tuu.

Sasa huyu mzee wa makamo alivyoonza tukawa tunafuturu wote pamoja, ila kuna siku ananishangaza kidogo anafuturu hata saa 5:50 jioni.

Yaani akimuona tu yule muuza futari anapita kuchukua oda basi mzee anamwambia niletee na kwemi baada ya dakika 10 futari imefika mzee anafuturu ukiangalia saa ni 5:45 au 5:55.

NINACHOWEZA SEMA KWAMBA HUYU MZEE KUFUTURU INATEGEMEA NA MUUZA FUTARI KAPITA MUDA GANI, YAAN HANA MUDA MAALUM WA KUFUTURU.

Ndio nimekuja na jambo hili nataka ufafanuzi wenu wakuuu
Wanafunga kweli? Mbona vibao vya vyumba vimejaa havigeuzwi
 
Sawa wewe Mkristo uliyetokea kwa wasio Wakristo
unadhani uKristo ni dini? RC ni dini tu kama zile ambazo zilikwepo duniani kabla hata Kristo hajaja duniani katika mwili. Kazi ya dini ni kumuua Yesu, hata leo zinamuua.

Na jambo la uhakika ni kuwa Usipozaliwa mara pili huwezi kuuona ufalme wa Mungu, kamwe! YOHANA 3:3-5
 
Mlivyojutahidi sasa kutafsiri hiyo maana ya kuzaliwa upya! Si kwa level hiyo ya kujihesabia haki. Poleni sana
 
Back
Top Bottom