Mkuu ilikuwaje mpaka aya ikafikia hapo hyo matayo?
Weka mlolongo tuone kisa kizima kwa mujibu wa matayo ilikuwaje na kilisemwa nini na wanafunzi mpaka wakasems hivyo.
Yani tupate ushahidi wa maandiko juu ya yesu kuelezea kuhusu wanandoa kutengana kwa kurejeana.
Kuns kutengana kwa muda kishs mksrejeana alafu kuna kuachana moja kwa moja bila kurejeana(haya uislsmu umeruhusu yote)
Samahani mkuu
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kisa chenyewe hiki hapa mkuu:
Mathayo 19
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³ Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
Mafarisayo walikuwa wajuzi wa torati, hivyo mara nyingi walimuuliza Yesu maswali ya majaribu ili avunje torati wamshitaki. Hapa wanamtega kuhusu kumwacha mke kwa kila sababu.
⁴ Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba Yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
⁵ akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
⁶ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Hapo Yesu anatumia reference ya uumbaji kuelezea mpango wa Mungu tangu mwanzo. Hakuumba mwanamume mmoja na wanawake wengi ili achague wa kuoa na kuweza kuacha pia. Anamaliza kwa kusisitiza
aliowaunganisha Mungu mwanadamu asiwatenganishe. Swali la msingi kabisa hapa, ni ndoa zipi zinaunganishwa na Mungu? Amini nakwambia sio kila ndoa kwa sababu tu imefungwa na kanisa basi Mungu ameiunganisha, hapo ndipo palipo na hekima.
⁷ Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
⁸ Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
Hapo ndipo penye msingi wa talaka za agano la kale. Kwamba ni ugumu wa mioyo ya wanadamu uliomlazimisha Musa awaruhusu kutoa talaka, lakini mpango wa Mungu tangu kuumbwa kwa mwanadamu haukuwa hivyo. Mpango wake ulikuwa mke mmoja, mume mmoja basi.
⁹ Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Ruksa pekee kwa ndoa za kikristo kumwacha mke ni kama amekuwa mwasherati. Sasa uasherati ni tendo la ndoa pasipokuwa na ndoa. Kama binti ataanza ngono mapema kabla ya kuolewa maana yake atapoteza bikra. Mumewe baada ya kufunga ndoa anapomwingilia kwa mara ya kwanza akakuta barabara imewekwa lami kabisa hapo ndipo anaruhusiwa kumwacha.
Huyu mwanamke maana yake alikuwa mwasherati kabla ya kuolewa, ndio maana kuna maandiko mengi tu yalisisitiza mwanamke atoe damu siku ya kuolewa na iletwe kama ushahidi kwa wazee. Kwa sababu siku hizi tumefanya uasherati kuwa sehemu ya maisha, hatuzingatii maagizo ya Mungu, kwa kuwa kuna neema, hivyo tutapata tu msamaha. Basi sawa, lakini tukiiwasha tamaa ya mwili, ndoa haiwezi kuituliza, zaidi tutaishi kwa kutamani kulala na watu nje ya ndoa ili kukidhi tamaa za mwili tulizoziamsha na kujizoesha hivyo. Ndoa sio jibu la tamaa za ngono hata kidogo.
¹⁰ Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
¹¹ Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
Kwa kulitazama kibinadamu wanafunzi waliona kabisa kuwa jambo hili haliwezekani. Watu wanakorofishana na wake zao kwa mambo mengi mno, hivyo sio rahisi kuweka kipengele kimoja tu kumwacha mke.
Lakini Yesu aliwajibu kimaandiko, neno hili sio la wale wanaoishi kwa kanuni za ulimwengu huu. Kwamba vijana wanajifunza ngono mapema, wanajifunza miondoko mbalimbali, wanachezeana kutwa kucha, kisha wanaingia kwenye ndoa. Kwa sababu ya ladha mbali mbali walizopitia kabla ya ndoa (vionjo, utundu, saizi n.k), ni vigumu kuwa na utulivu tena. Moyo umejaa ubatili, nafsi haiwezi kutulia kwa mwanamke ama mwanamume mmoja. Lazima baada ya muda mfupi kila mmoja atajisikia tamaa kuonja vya nje alivyovimiss, kila mmoja ataona mapungufu ya mwenzake kwa kulinganisha na uzoefu alioingia nao kwenye ndoa.
Ila wale waliojaliwa, hawa ni wale waliojaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu. Hawa tangu malezi yao hawakujishughulisha na mambo haya ya kidunia, bali waliweka muda wao mwingi katika kufuata maagizo ya Mungu. Mioyo yao imeshiba neno la Mungu, hakuna nafasi ya udanganyifu wala hila za shetani.
Watu kama hawa ndio wanaotoka kwa Bwana na hawa wamelelewa na Bwana, ndio hawa wanaoozwa na Bwana. Kuishi kwao ni Kristo na kufa kwao ni faida, hawaishi kuufurahisha ulimwengu, bali kumpendeza Mungu. Kwa watu kama hawa mwili umekufa tayari bali roho ndiyo iko hai. Hawa ndio wale wanaoweza kusema hapa duniani tu wasafiri.
¹² Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
Hapa anamaliza kwa kufananisha na matowashi. Wako wanaume ambao wamezaliwa mahanithi toka tumboni mwa mama zao, hawa hawana tamaa za mwili za ngono.
Wapo mahanithi wa kufanywa na wanadamu, ambao katika nyakati hizo wale watumwa waliofanya kazi kwa mfalme walihasiwa ili wasije wakapanda mbegu yao kwa mfalme. Hawa nao neno hili kwao si kitu.
Lakini wapo ambao wamejifanya mahanithi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, hawa ndio wale wanaoishi kwa kufuata maagizo. Wameuua mwili na tamaa zake na hivyo hawaendeshwi na ulimwengu. Hawa ndio waliojaliwa kulipokea neno hili nao hawataona ugumu wowote.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk[/b]