Natamani tupatane watu 40 wenye milioni 5

Natamani tupatane watu 40 wenye milioni 5

Ndugu watanzania, nimewaza, hapa natamani TUPATIKANE WATU arobaini tuunganishe mitaji ya Mil 5 ili kuitimiza Mil 200 then tuwekeze kupitia Vodacom M-wekeza, huku tukitarajia kupata faida ya zaidi ya asilimia 13 kwa mwaka. Ambapo tujihakikishie kupata zaidi ya Mil 26 kwa mwaka na kwa mwezi 2.1M, ambapo tutakubaliana kuziacha kwa miezi sita then tukapanga mradi Upi wa kufanya.

UNAJUA..

Wenzetu wazungu wanaakilinsana huungana na kufanya mambo kama haya na mwisho wa siku hufanikiwa sana, ila sisi wabongo tunachoweza ni umimi na kupambana kiume. Sasa nimewaza why tusifanye kitu kama vijana?

If interested nicheki tuyajenge.

200M capital, na profit ya sawa na 1.2M kwa mwezi, gawanya kwa 40 inakuja elfu 30 tu.

It sounda good kuzitamka kwa pamoja lakini Net Growth per individual ni kidogo sana.

By the way ni idea nzuri
 
Kwanza watu 40 ni wengi sana kutatikea cgangamoto
Pili lengo linatakiwa lifanane ikiwa kila mtu analengo lake ni vigumu kufika hitimisho
 
Investment ya 200m upate 2m faida kwa mwezi ???

Haya mambo ya M-wekeza, UTT and the likes zimeundwa kwa ajili ya watu wavivu au kwa lugha nyingine waajiriwa kwa mpambanaji mwenye ndoto za kutoboa huko hakukufai
Kunabaadhi ya biashara ukiwekeza kwa hiyo M 200 unapata hadi M5 kwa mwezi
 
Huu ni ukichaaa wanangu yan uweke million 200 alafu usubiri million 26 kwa mwaka.??? Wastan wa million 2 na kitu kwa mwezi kwa mtaji wa million 200

Si bora mnunue hata bajaji tano zitafikisha hiyo hela kwa mwaka na kwa mtaji mdogo tu
 
mradi wa hovyo kuwahi kutokea, watu 40 kila mwezi faida milioni 2. kwa mwaka faida milioni 24 ukigawanya kwa watu 40 kila mtu anapata faida laki 6. huu ni ukichaa unaweka milion 5 upate laki 6 kwa mwaka
hapo umepinga ILA hujaleta WAZO mbadala ambalo ni zuri zaidi (low risk) kwa uwekezaji wa shs 5000,000 aliopendekeza. Amekuja na wazo lake msaidie sio kumponda.....
 
Hivi nikiweka mil 6 Vodacom M-WEKEZA nitapata kiasi gani faida kwa mwezi?
 
hapo umepinga ILA hujaleta WAZO mbadala ambalo ni zuri zaidi (low risk) kwa uwekezaji wa shs 5000,000 aliopendekeza. Amekuja na wazo lake msaidie sio kumponda.....
aendelee kufanya kilichompa hiyo m5, halafu wewe tunajua nia yako upate wazo. mawazo ya kuingiza pesa yanauzwa mkuu
 
aendelee kufanya kilichompa hiyo m5, halafu wewe tunajua nia yako upate wazo. mawazo ya kuingiza pesa yanauzwa mkuu
Kusema aendelee na alichokuwa anafanya, huo ni kati ya ushauri ambao siukubali kabisa
Kwa hiyo kama alikuwa anafanya boda boda kijijini kwake na sasa hivi hailipi tena; aendelee kukomaa nayo wakati kwa sasa hailipi tena?
Kusema wazo linauzwa ni sawa, ILA linalo uzwa ni wazo la kueleweka lililofanyiwa utafiti wa kutosha...
Hata hapa kwetu kuna Fursa
Mfano Kijana aje na wazo aseme; anawazo zuri sana ambalo linahitahi mtaji wa.........na faida yake inaweza kuwa kati ya ......na .......na aseme yeye yupo tayari kusimamia na kulipwa. Unaona hapo amejitengenezea ajira
Zipo fursa kama za mradi wa matofali, nk nk nk
 
Back
Top Bottom