Nategemea hii ndio itakuwa story ya mwisho kuileta humu kumuhusu huyu mwanaume

Nategemea hii ndio itakuwa story ya mwisho kuileta humu kumuhusu huyu mwanaume

Sizani mimi najua kutakuwa na ka mtu ambako lazima akapigie simu kukauliza mawili matatu
Amini usiamini dada yangu unaweza kukuta hata hiyo mtu hayupo, mimi mwenyewe na shemeji yako tunataka kupigana chini kwasababu ya expectations kama hizi
Yaani unataka nikuwaze siku nzima, kazi nifanye na hela pia nikutumie?
 
Labda niseme hivyo
Kuna namna unatamani mtu akupigie simu hata siku moja kukusalimia au kusema tu nimekumis hata kama hatuna bond but sioni kwake yaani njia yetu ya mawasiliano ni sms tu no calls… yaani ukitaka kusikia sauti ya mpnz wako usubiri siku muonane live ndio uisikiee ni kama date ya mabubu
MAana ya 'communication is key' ni ww umfungukie hvyo ajirekebishe. Effort itoke pande zte mbili. Tofauti n hpo itakua One sided love.

Dont be hard on yourself. If u need someone to talk to am available
 
uandishi wako inaonesha b
Habari zenu wana JF

Nimekuwa nikileta story ya huyu mwanaume ni kama huu ni uzi wake wa 4 ama wa 3 nikihitaji ushaurii kuhusu mahusiano yetu mimi na yeye.. ninafikiri Leo Hii ndio itakuwa mara ya mwisho kumjadili humu na maamuzi nitayafaya kupitia huu uzi wa Leo Hii ( kuachana ama kubaki nae )

Huu mwezi unaenda wa 5 niko na huyu Kijana nashindwa kumsoma kabisa sijui ni mahaba yamezidi kwake ama nimeanza kupoteza kujiamini..

Nilileta kisa kuwa huyu Kijana anatabia ya kuni ghost kiaina kitu ambacho kinaniweka dilemma..

Kwa upande wangu sijui kama nitakuwa ninakosea ama niko sawa

Hipo hivi, kutokana na mahusiano niliyopita nilishazoea hiki kitu kwamba mwanaume ndio ana jukumu la kupambania penzi haswa kwenye upande wa mawasiliano.. nimezoea kupigiwa simu, kutumiwa sms na kujaliwajaliwa.. sasa huyu mtu niliempata sasa ni tofauti kabisaa hali inayonifanya nijisikie vibaya nihisi kama hanipendi

Nisiwe Muongo, huyu Kijana mara nyingi amekuwa akinitafuta yeye kunisalimia na kuongeaongea blablah.. mimi humtafuta mara chache sana na hiyo kama nikiona amenichunia sana ndio namtafuta

Kinachoninyima raha zaidii huyu jamaa yeye hapigagi Simu zaidii ya sms tu.. yaani kuchat, na siku ukiona amekupigia simu ujue ni siku mnaenda kuonana ndio atapiga simu kukuelekeza alipo ama mtakapoonana zaidii ya hapo hutopokea simu yake.. na Kama ukimpigia simu huwa hapokei atakutumia sms am busy

Jamani huyo ni mpnz gani ambae hamiss sauti ya mpnz wake, yaani husuniano letu tangu tuanze ni hivohivo.. sikatai anaweza kuwa ni mtu ambae hapendi kuongea na simu but mara mojamoja kuna shida gani kama tutaongea.. mimi sio kwamba siwezi kumtafuta ni naweza sana ila kuna yake mazingira siyaelewi kwake,, yaani nahisi kama hanipendi najipendekeza kwake , kwaiyo napata ugumu sana kuwa namtafutatafuta

Navowaambia Leo ni siku ya 2 hatujawasiliana… mimi kwakweli sijui ni kiburi ama ni nini nashindwa kumtafuta kabisaa akili yangu inaniambia kama ananipenda yeye ndio aniangaikie sio mimi kumuangaikia yeye

Na kila nikisema namuacha unakuta ananitafuta basi Kuna vitu ananiambia ambavyo vinanifanya nimuonee huruma, utasikia kuna vitu napitia tukionana nitakwambia basi naghairi ila ndio hivyo mpk now sijaonana nae kutokana na sababu za kikazi

Naombeni ushaurii kwa Hii changamoto ninayopitia… je ninachofanya Mimi ni sahihi kumuacha yeye aniangaikie kwanza,, je Kuna mahusiano kweli hapa au napotezewa muda
Kweli mwanaume anaekupenda anaweza kukaa hajakutafuta siku 3 wala haongeagi na simu na mpnz wake maana Hii imekuwa mpya kwangu
huyo ni TISS
 
Binti we angalia moyo wako tu,,npo na uyo jamaa ukipga asipopokea ole wako umuulize jibu utalopewa utajuta kuuliza,au asipojib mesej uliza uone🤣,na akikumis hakikisha upo active ole wako asikupate..........mambo ni mengi
Hizi code ni unique kwao
 
hahaha alafu unakaita kakijana kama yupo humu ujue ndio na msg hupati tena
 
MAana ya 'communication is key' ni ww umfungukie hvyo ajirekebishe. Effort itoke pande zte mbili. Tofauti n hpo itakua One sided love.

Dont be hard on yourself. If u need someone to talk to am available
Okay nashukuru
 
nayeye ukimpigia au akitaka kukutafuta anawaza haka kabinti kanataka kunichuna au kana taka kuniharibia malengo
Always he said this “ nimekuchagua wewe kwasababu sio binti wa mambo mengi uko loyal “ jamani mimi kweli sina mambo mengi ila watu naokutana nao ni wa mambo mengi wananivuruga
 
Always he said this “ nimekuchagua wewe kwasababu sio binti wa mambo mengi uko loyal “ jamani mimi kweli sina mambo mengi ila watu naokutana nao ni wa mambo mengi wananivuruga
njoo inbox nikufunde
 
Sasa wewe ni sawa mimi hata sekunde 1 sijawahi ongea nae kwa simu ukiachana na siku ambazo tunaonana tu.. yaani mawasiliano yangu na yeye ni through text
Kumbe hata sms anajibu, hakuna cha ajabu hapo inawezekana nyie ni watu wakanisani sana, au mnaishi kwa kuogopana hata mkipigiana mtakosa story tu 😂 bora mchat tu, damu zenu bado hazijaendana vzur, mvumiliane tu
 
Back
Top Bottom