NATO wanatishia, Urusi hatishii atavamia kweli na inaweza kutokea Vita kweli

Unajua historia vizuri wewe,kati ya Marekani na Urusi nani alisalimu amri kwa Watalebani kabla lengo lilimpeleka Afghanistan halijatimia?
Najua wewe unazungumzia miaka ya nyuma kwenye kuanguka kwa usoviety. Lakini Urusi hii ya Leo sio ya kipindi kile,cheki Putin alivyomzuia Marekani kumpindua Assad huko Syria,akamzuia kumpindua rais wa venezuela na akatwaa Jimbo la Crimea huku Marekani akijitahidi kuzuia lakini wapi.
 
Bado unakosea kumtaja Putin bora ungesema Rusia; sijui kwanini unapenda mtu tofauti na taasiai.
 
Likija swala la vita isee ..... Russia ni hatari ........lile ni jesh la mtu mmoja
Sawa lakini kumbuka NATO ni umoja wa nchi zaidi ya tano Tena zenye nguvu kijeshi na kiuchumi sidhan Kama Russia anauwezo peke ake kupambana na NATO yte watamtia vidole
 
Mkuu ni sawa kabisa ulivyoandika. Marekani kasalimu huko Afghanistan kwa wataleban.Hatamsogelea Urusi.
Marekani ndio dola lenye uwezo na nguvu zaidi sema ni wajanja Sanaa vita vyao hupigana kwa akili
 
Sawa lakini kumbuka NATO ni umoja wa nchi zaidi ya tano Tena zenye nguvu kijeshi na kiuchumi sidhan Kama Russia anauwezo peke ake kupambana na NATO yte watamtia vidole
Russia hata mkimchangia ni kazi bure aisee, awa jamaa kiukweli wanajiweza sana kwenye mambo ya kivita na pia ni watu majasiri na wenye mapenzi ya dhati na taifa lao.

Kwenye ww2 kulikuwa na mapigano ya kugombea jimbo la stalingrad.Mrusi akiwa peke yake huku upande wa pili yupo Mjerumani,Mtaliano, hungary na Romania.ilipigwa vita ya kufa mtu na mwisho wa siku Mrusi akaondoka na ushindi.
 
Sawa lakini kumbuka NATO ni umoja wa nchi zaidi ya tano Tena zenye nguvu kijeshi na kiuchumi sidhan Kama Russia anauwezo peke ake kupambana na NATO yte watamtia vidole
Of course hawez kuziweza nchi zote ila dunia itaaribiwa ..,..KUMBUKA RUSSIA ndo anaongoza kwa kuwa na SILAHA ZA NUCLEAR dunian
 
bila shaka muandishi ni dr shika
 

Kila nchi inajiweza kwa kiasi chake. Russia sio invincible kama wengi mnavyojaribu kuweka.
Ukipata muda kasome yaliyomkuta Afghanistan na Chechnya....bila kusahau kwenye WW2 kama sio ile baridi kumsimamisha Adolf historia ingeandikwa tofauti.
 
Kila nchi inajiweza kwa kiasi chake. Russia sio invincible kama wengi mnavyojaribu kuweka.
Ukipata muda kasome yaliyomkuta Afghanistan na Chechnya....bila kusahau kwenye WW2 kama sio ile baridi kumsimamisha Adolf historia ingeandikwa tofauti.
Hayo maneno ya kwenye vijiwe vya bangi.kwani WARUSI wao ni maroboti mpaka baridi isiwaumize.katika kosa kubwa Hitler alilofanya katika maisha yake ni pale alipojaribu kuivamia URUSI, naimani kama asingeivamia URUSI basi historia ingeandikwa vingine kabisa.na siyo Hitler peke yake Napoleon wa Ufaransa alipiga mataifa mengi makubwa ila alipoingia kwenye ardhi ya WARUSI ukawa ndo mwisho wake.

Kuhisu Afghanistan ni sehemu ngumu san ya kupambana na adui kutongana na mazingira yake ya milima, Marekani na Nato wana zaidi ya miaka 10 Afghanistan na bado Wataliban wana tawala maeneo mengi ya nchi.Na sasa ivi washaanza kuondoa vikosi vyao ndani ya ardhi ya Afghanistan.

Kuhusu Chechnya mbona tumeshasahau kuwa kulikuwa na waasi wa Chechnya.WARUSI walisafisha waasi wote mpaka leo ni moja kati ya jimbo linalovutia ndani ya Nchi ya URUSI.

WARUSI sio watu wa mchezo ndugu hata vifaa vyao ni moja kati ya vifaa bora kwenye uwanja wa vita.AK 47 hata ukichimbia chini miaka 100, siki ukitoa ni mwendo wa kufuta vumbi tu unaingia nayo uwanja wa vita.kafanye ivi kwenye bunduki ya KIMAREKANI uwone nini kitakutokea
 
Nadhan ameelewa mkuu.......sema Mara nying western media haziwazungumzii kiuwezo
 
Hoja yangu imejikita kwa Putin kutengeneza mifumo imara kama mpinzani USA na iwe na uwezo wa kupandikiza viongozi huko USA na kwingineko siyo yeye kua ndo kila kitu...ikitokea akifa leo ndo tena RUSIA irudi ilikotoka? nisome vizuri tena.
Tatizo watu mnaongelea Urusi utafikiri ni nchi yenye miaka 60 ya kujitawala...Hawa watu wapo na system ya utawala maelfu ya miaka nyuma huko, kabla hawajawa empire, russia empire, soviet union, russia republic, russia federation....
Hata Putin akifa leo..maisha yataendelea tu kwa hawa jamaa...either kuendelea na mfumo wa sasa au kuanzisha mwingine, wanaweza fanya chochote hawa...
 
Apigane na China, Urusi au Korea kaskazini atachukua nn? Ni bonge la hasara
Hivi unajua China na Russia wana rasilimali kiasi gani!? Kwa taarifa rare earth materials zaidi ya 80% yanapatikana China (usiniulize hayo materials yana umuhimu gani). Russia anatandika bomba la kusafirisha gesi kwenda ulaya, kutwa US anazusha visa juu ya hili (tafuta majibu kwa nini US anazusha visa hivi)
 
Anachofanya Urusi hata Hitler alianza hivyo hivyo,mwishoe akajitanua na kuota mapembe. Kama hujui kuwa Ulaya wanalichukulia hili jambo seriously subiri uone moto wake. Nchi kama Poland, Romania,Norway na Sweden wanalichukulia kwa uzito mkubwa sana.
Nchi gani ya ulaya inayotaka kugeuzwa kifusi na makombora ya Urusi ?
 
Nchi gani ya ulaya inayotaka kugeuzwa kifusi na makombora ya Urusi ?
Kwanza, Nadhani NATO wakimsumbua anaweza kuichukua Alaska kwa sababu mara kadhaa amesikika akinong'ona kuwa aliuza eneo lile kimangumashi. Hivyo ni muda mzuri anaweza "kuwarudishia hela kwa staili ya aina yake" na kuchukua eneo lake.
 
Jamaa wamejiandaa kitambo sana tokea baada ya vita ya 2 ,Kuna mpaka mifumo ya kibank ambayo muda wwote kikinuka wanauwezo wa kujidisconnect na mataifa wanayotaka ,Rafiki wake mkubwa ni China ambayo mji mmoja wa kawaida wa China GDP yake ni sawa na Uswizi au Italy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…