Mfano Dar es salaam watu wa aina hiyo wako kibao wanaitwa mamessenger wa watu binafsi unamtuma popote ofisi yeyote Hata kupeleka gari kuoshwa au gereji ,au kufuatilia maswala ya TRA,Benki,bandari,Tanesco ,kuwatuma hata wakuketee chakula kizuri kutoka restaurant unaipenda wakuketee ofisini ,kupokea mizigo stendi au abiria watoka mikoani au nje ya nchi na kuwafikisha nyumbani au hoteli nk Kwa malipo sio makubwa sana huku wewe ukiendelea na kazi yeye anasimamia huko Kila kitu.Badala wewe mfano hata kuacha kazi ukakeshe stendi kusubiri basi la nduguyo Toka mkoani waweza lala nyumbani akampokea akaja naye nyumbani bila shida nk kununua sanda ,kutafuta mahema viti, kusindikiza watoto shule na nkAisee ni akili tu kumbe kazi zipo kibao.
Ni hudumu ya muda ila mtu kupewa Huwa anakuwa anajulikana sana uaminifu wake.