Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

 

Attachments

  • 20221014_175243.jpg
    545.8 KB · Views: 12
Mungu akubariki! Endelea kuamini..tunae Mungu mwenye Enzi yote nguvu na uweza wake ni hakika kabisa.

[emoji1479].
 
Reactions: ovi
Ha ha haaa, mburura hawatakuja kuisha. Mtaji wa fake pastors ni mburura kama hizi
Hizi mimi naita mbuzi!

Dhumuni la Mungu kuweka viongozi wa kiroho katikati ya watu wake toka mwanzo lilikuwa ni ili wawakumbushe watu namna nzuri ya kujiandaa na maisha baada ya kifo ila hawa fake pastors wanachokazana siyo kuwaambia watu wasizini,wasiibe wasioneane kijicho au kusemana vibaya wao wanawaambia wajiandae kupokea magari huku kazi hawana,wanawaambia wapokee nyumba hata bei ya misumari hawaijui wengine wanaambiwa pokea mtoto huku vizazi walishavitoa kwenye matukio ya utoaji mimba.

Mtu anajiita mtumishi wa Mungu lakini anakuhubiria mafanikio ya kidunia toka mwanzo wa ibada mpaka mwisho wa ibada mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wa mwaka hakuna alipokukumbusha usitende dhambi yeye ni utapandishwa cheo,kazi uliyoomba utapata hakwambii kasaidie watoto yatima na wasiojiweza huko mitaani yeye ni "toa sadaka injili isonge mbele,toa sadaka kwenye madhabahu ya bwana ndo utabarikiwa” anafunga hesabu anaondoka kesho tena hivyo hivyo hakwambii ni kwa namna gani hayo yatakufaa baada ya maisha ya duniani?

Na ni wajanja,huwakuti kujenga sehemu kwamba hapa ndo pakuabudia maana wanajua siku ”wapigwaji” wakiamka hakuna wa kuingia humo wao wanafanya kwenye viwanja vya serikali wakifunga hesabu yao ya siku kesho tena hivyo hivyo wakichuja wanaenda kwenye fursa nyengine huku ”wapigwaji" wakihamia kwengine kupigwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…