Natumai wote tumeshamaliza 'Kuushangaa' Utezi wa Mama, sasa kama JF 'Great Thinkers' jibuni Maswali yangu haya....

Hizi ni asante tu na ccm wasione aibu kuiiga chadema(kama kawaida yao serikali),wabebe na hili LA majimbo (nchi kuendeshwa kimajimbo
 
Sasa yeye ndo akili zitamrudi vizuri mpaka ataomba po.
 
Hayo maswali ungeanzia kuuliza kwa kipindi cha mwendazake
 
Uteuzi uko vizuri sana tena sana.
Kuteuliwa na Rais ni Heshima Kubwa sana.
Wote walio teuliwa ni watanzania wenzetu wa kuzaliwa hakuna mhamiaji wa kigeni, lkn pia wote walio teuliwa ni watu wenye uzoevu wa kuitumikia jamii ktk nafasi mbalimbali.
wote walio teuliwa ni watu wenye kuheshimika ktk jamii, hakuna mwizi wala muhuni, wanajiheshimu, hivyo nafasi ya U DC imeheshimishwa vilivyo, hakuna kasoro kwa wateuliwa.
tatizo la baadhi ya watanzania tulizoea au kudhani kuwa vyeo vya u DC au hata vingine ni kwa watu maaluum sana, hapana! kila mtanzania mwenye sifa ana uwezo wa kuwa kiongozi wa kulitumikia taifa lake, tuache mazoea na kudharauliana.
Pongezi kwa wateule wote, mara baada ya kula kiapo mchape kazi kwa bidii.tunawaamini sana kuwa mtaleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
 
Mkuu ukiwa rais chondechonde hii ID yangu usiisahau unipe nami japo uDC,hakika sitakuangusha
 
Hivi yule aliekua DC Ukerewe Somebody Magembe nae kapata tena? Pia yule wa Sengerema.Naombeni majibu wanajukwaa
 
1. Ukuu wa Wilaya kiheshima bado uko pale ila wateuliwa hovyo, hawajielewi.
2. Miaka 45 mpaka 50 siyo kijana, ila aliyekuzidi ana haki ya kukuita kijana.
3. Kuteua makundi maalum its a political strategy.
4. Siyo kila mtu anastahili kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya..
5. Kwa sasa uteuzi ni kulipana fadhila au kutaka fadhila..
6. Wako waliostahili ila wengine hawakustahili, ila who are we kumpinga RAIS WA JMT..
7. Bado sijafikia ule u GT, ila uteuzi ndio unaotufanya kujadili ule u personality kuliko majukumu yanaowasubiri, we hope they know and are prepared to face those challenges ahead.
Jamaa aliyeteuliwa Siha anayo elimu, kiutendaji hatujuwi, ila tumpe moyo afanye yake bila kuwaangusha raia wa huko..
 
Mama ametumia mfumo wa malezi kwa watoto katika uteuzi. Ni mfumo usiobagua watoto hata kama watoto wawili kati ya kumi hawana elimu nzuri Na uzoefu. Yeye ameona wote ni watoto wake tu Na wanahaki sawa.

Mama akipata pension watoto wanapata mgawo vizuri sio kama baba . Mama ni mtu wa haki kwa watoto.

Na kiukweli mfumo huu wa malezi ya usawa kwa watoto unachangamoto nyingi sana . Tuwape nafasi nao wafanye kazi yao Na wakishindwa tutawajadili humu humu JF
 
Well said, me naona tuwape muda tutaona utendaji wao, wahenga walisema umdhaniaye ndiye kumbe siye. I hope kati yao humo kuna viongozi wazuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…