Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Umetoka kwenye utapeli umeamia kwenye wazimu kama mstari wa luka hautibu we shida yako ni nini
Mbona unateseka kwani umelazimishwa kutumia
Majungu sio mtaji
Ughushi mkubwa katika Luka 24:44-48 kuhusu “ufufuo wa Yesu siku ya tatu” ukidai kwamba ulitabiriwa katika Agano la Kale wakati ni uongo hakuna hicho kitu katika agano la kale!
Hebu tuangalie Luka 24:44-48 kutoka katika Biblia ya NIV:
Luka 24
44 Akawaambia, Haya ndiyo niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi: Ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Mose, na katika Manabii na Zaburi.
45 Kisha akazifungua akili zao wapate kuelewa Maandiko.
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 Na toba na msamaha wa dhambi utahubiriwa kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu.
48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.
Wapi katika Agano la Kale yameandikwa maneno hayo?! Nionyeshe mstari mmoja wa Agano la Kale uliotabiri kuhusu ufufuo wa siku ya tatu wa Yesu?