UTANGULIZI
Daniel 5:25 Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Ukisoma huu mstari utaona ni mara moja kwenye biblia yote Mungu ametumia mfano wa code kufikisha ujumbe, japokua anaweza tumia njia nyingine sababu anazo nyingi kufikisha ujumbe. Mimi binafsi natumia bible code kuwa agano kwa watu na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
SINA KANISA HUDUMA YANGU NI ONLINE ASILIMIA 100 (DIGITAL) NA LENGO NI KUFIKIA WATU WENGI KIURAHISI
- Kama kichwa cha habari kinavyosema sina kanisa na sina mpango wa kufungua kanisa ni asilimia 100 online
- WhatsApp only 0713520180 ni kwa maelezo zaidi ya code nazozitoa kama una-maswali binafsi
- Hii ni ibada ya sirini nikimaanisha kama ni mkristo dhehebu la roma unabaki huko, same kwa lutheran, wasabato, na hata kama ni muislamu unatumia code ukiendelea kubaki kuwa muislamu
AINA ZA CODE NTAKAZOZITOA
- Zinazohusiana na binadamu
- Zinazohusiana na viumbe tofauti na binadamu
- Zinahusiana na kutumia nguvu za Mungu (Yahweh) kupambana na ufalme wa giza kujua aina za shetani. Shetan aliyehasi ni mmoja ila baada ya kutupwa nje ya mbinguni walifaraka na kutokea mashetani wengi na falme zao na wenyewe kwa wenyewe wanapigana vita mpaka sahivi
- Zinahusiana na science
- Zinazohusiana na universe kwa ujumla maisha kabla ya uharibifu
MAMBO YA KUZINGATIA
- Usifanye masihara na hiki nachofanya sikutishii ila kama unaona hakina msaada kwako achana nacho sababu una-haki hiyo ila usifanyie masihara na mizaha na hizi code
- Kama huna iman juu ya hizi code ni ngumu sana kufanya kazi
- Code zinatolewa bure hulipii gharama yeyote ntakua nazituma huku kwenye huu uzi na matumizi yake
- Nia yako moyoni mwako ndo itakayoamua either code ifanye kazi au la nikimaanisha kama una nia ovu kama kisasi, kuwa kikwazo kwa wengine, kuwakera wengine, n.k hazifanyi kazi ili ifanye kazi inatakiwa uwe mnyenyekevu
- Code hazina ishara yeyote ile sababu zimejikita kwenye ulimwengu wa roho na zinafanya kazi kimya kimya na ni mara chache sana zina miujiza
- Code inachukua mda kufanya kazi means inafanya kazi pole pole ni kwa mda gani exactly mapenzi ya Mungu ndo yatakayoamua na ni mara chache sana inafanya kazi mara moja (instantly)
- Kwenye suala zima la kipato inakupa unachostahili kama ni utajiri itakupa utajiri ila huwezi lazimisha kupata utajiri
- Inabadilisha sheria za ulimwengu wa roho
- Hakikisha unafanya kazi hizo code zisiwe tiketi ya wewe kusubiria miujiza
- Code mda mwingine inaweza isiondoe tatizo linalokukabili ila ikalisitiri (kulifanya kuwa irrelevant) lisiwe ni kikwazo kwako lakin litaendelea kuwepo
Karibuni katika utukufu wa Mungu
Usisahau kushare hizi code na jirani yako ni bure gharama yake ni imani tu
"Don’t stop praying because you don’t see results immediately"