Gibbethon bible code
JF-Expert Member
- Oct 9, 2023
- 439
- 677
- Thread starter
- #421
NAMNA MUNGU ANAVYO WEZA JIBU MAOMBI YAKO BAADA YA KUTAMKA BIBLE CODE
- Kama baada ya kutamka hizi code una-kifungo cha hofu endelea kutamka mpaka kiondoke na kije kifungo cha amani-hii ni moja ya ishara ya Mungu kujibu maombi yako au hitaji lako analifanyia kazi
- Utaacha kutamka hizi code pale ambapo kiu ya kuzitamka haipo tena ndani yako ni ishara Mungu kujibu maombi yako katika ulimwengu wa roho na kwa mda wake utaona katika ulimwengu wa mwili
- Mungu hajibu maombi kama unavyotaka bali anajibu anavyoona ni sahii kwako. Kuna watu baada ya kutamka hizi code Mungu ameshajibu maombi yao ila hawajajua kwa sababu wanataka Mungu awajibu kama wanavyotaka wao., jambo la kukumbuka ifanyie kazi fikra iliyokuja baada ya kutamka hizi code usiipuuzie hilo ndo jibu lako
- Mungu anajibu maombi in an ugly way, awkward way na kwa namna usiyotarajia na usiyoipenda ila in long run utaona ile picha uliokua unaitaka kuiona kwenye hitaji lako mwanzoni
- Mungu ni mara chache sana anatumia miujiza na ishara kujibu maombi yako., Ni mara nyingi sana na kawaida kutumia fikra zetu kujibu maombi yetu.
- Sio kila hitaji unalomuomba Mungu atakujibu mengine atakataa usijisikie vibaya fahamu ni kwa faida yako
- Kuomba hitaji kwa Mungu na akakujibu na ukapuuzia jibu la Mungu ukaendelea na mpango wako huo ni uasi sababu neno la Mungu ni sheria halitoki bure mfano umeomba mke/mme kwa Mungu amekuletea wewe umemuona sio mzuri au huna hisia nae ukaamua kuachana naye huo ni uasi na laana ya Mungu itakuandama maisha yako yote. Kuna baadhi ya mahitaji kabla hujamuomba au kumuuliza Mungu fikiria kwanza kwa sababu neno lake ni sheria na akiongea halirudi bure