dronedrake
JF-Expert Member
- Dec 25, 2013
- 23,901
- 58,103
sasa utashangaa yanavyojaza, rejea mwendokasi,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo waafrika muda sio diliKama unafika mapema let say nusu saa au dk 45 upo moro ni sawa.
Shabiby VIP45k ya wapi hiyo? Nauli ni 25k, imezidi 30k
Kwan nauli inategemea aina ya usafiriKwani bei ya nauli inategemea muda wa safari?
Wapanga bei wana mabasi yao. Je wakiweka bei ndogo ya treni nani atapanda basi?Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.
Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.
--
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu nauli za abiria kwa treni ya njia ya Reli ya Kisasa – ‘Standard Gauge Railway’ (SGR) zitakavyotumika kwa huduma ya usafiri wa treni za abiria.
Kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria Na. 3 ya LATRA, 2019 Mamlaka inapaswa kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwemo nauli za treni.
Katika kulitekeleza hilo, Mamlaka imeandaa mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa usafirishaji, ikiwa ni pamoja na watoa huduma, watumiaji wa huduma na wananchi kwa ujumla. Mkutano utafanyika tarehe 19 Disemba 2022 jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Anatorglo.
Nauli zinazopendekezwa na TRC ni Kama ifatavyo:
View attachment 2440636
View attachment 2440637
Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, LATRA inawaalika wadau wa sekta ya reli na wananchi kwa ujumla kushiriki katika mkutano huo wa kukusanya maoni ya wadau.
Vilevile, wadau wanaweza kuwasilisha maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu kwa maandishi kupitia LATRA Makao Makuu, Mtaa wa Tambuka Reli, Dodoma au ofisi za LATRA zilizopo Makao Makuu ya kila mkoa Tanzania Bara kabla ya tarehe 3 Januari 2023.
Aidha, maoni ya wadau yanaweza kutumwa kwa barua pepe kupitia anuani hizi: info@latra.go.tz na dg@latra.go.tz
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano – LATRA
06 Disemba, 2022
Hapa au hii ni kutaka kuwaonyesha wananchi kwamba kuendesha huu mradi ni garama kubwa au wananchi kutumia treni ni anasa.
Yaani kwenda Dodoma -60,000/-!.
Treni kwa waliostaarabika huko ni usafiri wa garama nafuu sana sisi unaenda kuonekana ni anasa.
Tatizo la tanzania tunatukuza Umasikini mno.sasa utashangaa yanavyojaza, rejea mwendokasi,
Mkuu ili wazo ni nzuri, tatizo mfumo wa maisha yetu waafrika hasa viongozi siyo wa kutatua changamoto+ kama hiyo bali wao wataongeza matatizo.Kwa nauli ya elfu 29 kama ni muda wa saa moja tu iko vizuri kuliko.kutumia karibu masaa saba kwa basi ma spidi limit barabarani kibao
Mabasi ya kwenda nyanda za juu kusini wajiandae kuwa na route za kuanzia morogoro kwenda mikoa hiyo sababu mtu akiua masaa sita ya barabara akishuka morogoro anapanda basi la kutoka Moro kwenda Iringa ,mbeya na Ruvuma anafika mapema tu
Treni hiyo iondoke mapema mfano saa 12 na nusu ifike morogoro saa moja na nusu watu wa mikoa ya nyanda za juu kusini wapande.mabasi yao kuanzia morogoro saa mbili yaondoke kwenda mikoani
Vivyo hivyo liwahi Dodoma wa mikoa ya kanda ya Ziwa wapandie mabasi Dodoma kwenda Kagera nk yawezekana kabisa watu wa kagera kufika siku hiyo hiyo bila kulala kahama
TRC wajipange kuhakikidha watu wana move faster kwa kushirikiana na wadau wa mabasi ya abiria
Ratiba zao wa consider hilo na Latra wajipange kupanga ratiba zao vizuri za mabasi ya Moro kwenda nyanda za juu kusini nk na Ya Dodoma kwenda kanda ya ziwa na kigoma nk
Treni ikimwaga mabasi yanapokea mbio yanakimbiza abiria
Hata sh 500 ya daladala ni nyingi Sana kwa mwananchi wa kawaida.Hizo bei ziko juu sana kwa Mwananchi wa hali ya chini.
Mbona kwenye sherehe mnachanga zaidi ya hizoUkiona hivyo huo usafiri siyo wa mwananchi wa hali ya chini. Umemlenga mwananchi wa hali ya juu