Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

faida kwa nani na vipi ? na faida ipi ? Monetary yaani Shirika lipate mapato zaidi au faida ya watu kuweza kufika point B kwa gharama nafuu ?

Huu ni muda wa kufanya nini na huduma zipi mwananchi anayezipata kwa sasa ? Na hii huduma ya usafiri wakati wake sahihi ni upi ? na kama ni kosa limefanyika / lilifanyika suluhisho ni kuweka bei ambayo sio rafiki kwa mwananchi wa kawaida hence kukosa yote yaani (monetary na socially)?

Wateja wakiwa wengi sana kati ya basi na train ipi ina gharama kubwa ya uendeshaji ?

unamaanisha ya kuwa na njia nyingi au chache ? Kama nyingi tuongeze njia zaidi ? Hizo njia hazina gharama ya kuzitengeneza na kuzifanyia repair ? Na usafirishaji wa mizigo mizito kipi ni cost effective train au magari / malori ?

This is another argument ambayo sioni faida ya kuongelea hapa huenda miaka kumi ijayo tukawa tunasema aliyeingia mikataba na hao wachina na sijui kina nani alikuwa mjinga wa kutupwa..., that's a blame game ambayo kwa leo nadhani nina more constructive issues za kufanya..., Na kama tungetaka kama nchi kuondoa uwezo wa mtu mmoja kuamua aliyepo sasa asingekubali kuendelea na Sheria inayomruhusu kufanya anachotaka
Shirika lipate mapato mengi na litoe gawio la faida kwa Serikali.Kwani saizi hawafiki point B kwa gharama nafuu?

Huu Ni mda wa kuendelea kujenga msingi kwa Maumivu,wakati wa kuja kupata Huduma Bora nj baada ya kukuza Uchumi na Watu kuwa na kipato Cha Kuridhisha Middle Income.
Kosa lilifanyika na sukuhisho Ni wekeka hizo Bei ili kupunguza hasara,ukumbuke ndege Zina Bei kubwa na Watu wanapanda Hakuna Cha Kukosa vyote..

Wateja wengi Ila wanalipa jero keep Ni hasara Ni Kama Tanesco mnakiwa na wateje weeengi wa buku 2 mbili mwisho wa siku Hakuna Cha Maana mnapata Ni Bora upeleke kwa wateje wachache wenye viwanda na Pesa unaonekana.

Nyandao wa Barabara ukiwa mkubwa unapunguza gharama za matengenezo na unazalisha Uchumi kwa haraka kuliko ujinga wa reli.Malori Ni flexible na yanafika kila sehemu tofauti na reli so principal ya demand vs supply itashusha Bei za usafirishaji wa Barabara/malori..

Mliojenga reli Ni tembo mweupe ndio maana mnatumia nguvu Sana na itakuwa hasara mazima.
 
Hizo bei sio kubwa endapo muda utazingatiwa
Maaan kama una haraka n nzur sana sasa hzo naul znafkia za ndege?
IMG_20221209_162432.jpg
 
Hapa au hii ni kutaka kuwaonyesha wananchi kwamba kuendesha huu mradi ni garama kubwa au wananchi kutumia treni ni anasa.

Yaani kwenda Dodoma -60,000/-!.

Treni kwa waliostaarabika huko ni usafiri wa garama nafuu sana sisi unaenda kuonekana ni anasa.
Nchi nyngne ni usafir wa bure kabsa uku kwetu ni anasa
 
Kama ni saa

Yaan ushakalili kwamba Bei ya tren ni ndogo kuliko basi..haiko hivyo inadepend na huduma unayopewa.leo hii Azam marine wanachaji 25000 had 30000 Kwa usafir Zanzibar.. Kwa mwendo wa saa moja na nusu. NeNda mwanza hadi ukerewe masaa matatu hadi manne, nauli haizid 8000/ Kwa Meli.
Kwani bei ya nauli inategemea muda wa safari?
 
Yaan 5000/= kwa lisaa limoja na nusu morogoro haiwez kuwa sawa kbsaaaaaaa
Afadhal hata 15k au 18k ili fedha zliztumik zird
 
Hapa au hii ni kutaka kuwaonyesha wananchi kwamba kuendesha huu mradi ni garama kubwa au wananchi kutumia treni ni anasa.

Yaani kwenda Dodoma -60,000/-!.

Treni kwa waliostaarabika huko ni usafiri wa garama nafuu sana sisi unaenda kuonekana ni anasa.
Hizi nauli ni bei rahisi sana. Sijui kwa nini mnalalamika?
 
Walamba Asali Wanataka Kutuuwa Bure, Wamezidi Fitna
 
Hili ni tatizo linalotengenezwa ataibuka mwingine ataunda kamati ifuatilie itakuja na bei tunayoitaka halafu tutaambiwa Fulani anajali wanyonge,ni msikivu mitano tena.
 
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.

Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.

--

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu nauli za abiria kwa treni ya njia ya Reli ya Kisasa – ‘Standard Gauge Railway’ (SGR) zitakavyotumika kwa huduma ya usafiri wa treni za abiria.

Kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria Na. 3 ya LATRA, 2019 Mamlaka inapaswa kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwemo nauli za treni.

Katika kulitekeleza hilo, Mamlaka imeandaa mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa usafirishaji, ikiwa ni pamoja na watoa huduma, watumiaji wa huduma na wananchi kwa ujumla. Mkutano utafanyika tarehe 19 Disemba 2022 jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Anatorglo.

Nauli zinazopendekezwa na TRC ni Kama ifatavyo:

View attachment 2440636

View attachment 2440637

Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, LATRA inawaalika wadau wa sekta ya reli na wananchi kwa ujumla kushiriki katika mkutano huo wa kukusanya maoni ya wadau.

Vilevile, wadau wanaweza kuwasilisha maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu kwa maandishi kupitia LATRA Makao Makuu, Mtaa wa Tambuka Reli, Dodoma au ofisi za LATRA zilizopo Makao Makuu ya kila mkoa Tanzania Bara kabla ya tarehe 3 Januari 2023.

Aidha, maoni ya wadau yanaweza kutumwa kwa barua pepe kupitia anuani hizi: info@latra.go.tz na dg@latra.go.tz

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano – LATRA
06 Disemba, 2022​

Kuna mkono wa wenye mabasi kuhujumu mradi siyo bure
 
Mhuu mradi utakufa kabla ya kuanza. Hapo Abood lazima achekelee sana. Mtu alipe 2.5x ya nauli basi kwa kisa gani? Upuuzi mtupu
Ndipo hapo akina abood, allysaid, newforce watatuma watu wao kwenye huo mkutano kama wadau, hao ndiyo watapiga kelele kwenye mic kudai nauli ya treni ibaki hiyohiyo.

Lengo ikose abilia.
 
Hata watete hawatapata abiria,, nauli lazima iwe chini ya nauli ya mabasi
Kwa sababu ya ushamba zile siku za uzinduzi mtapanda wengi na baada ya ushamba kuisha mtaanza kupungua na kurudi kwenye mabasi.
 
Back
Top Bottom