Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Kutakuwa hakuna maana Kama utachaji nauli ambayo haifikii hata robo ya gharama za uendeshaji na uwekezaji..
Uwekezaji ni long term kuna watu wanawekeza ku-break even ni after 200 years au generation...., Uendeshaji ndio ninakuuliza Je watu wakiwa wengi gharama za uendeshaji kati ya train na basi ipi ni nafuu ?
Sasa tulijenga Cha Nini Kama tutakuwa tunatumia Kodi ya Nchi kuendeshea sgr? Huu si Ni upumbavu?
Unajua kwa mizigo kutumia train tunaokoa kiasi gani katika maintanance ya barabara ?, unajua mtu kuja na kapu lake la machungwa Dar kwa bei nafuu au kuleta mchele kwa bei nafuu itapelekea wewe kuweza kupata bei nafuu ?

Hivi ingekuwa pesa tu ndio kila kitu kwanini hata DAWASA au TANESCO wasingechaji maji hata mara nne ya bei ya sasa kama issue ni kupata as much as possible moneywise ? Au ndio ile Unajiibia mwenyewe mfuko wa shati unaweka mfuko wa suruali....
Na hapa Sasa ndio huwa inakuja Ile maana ya private sector kujenga na kuendeshwa wenyewe.
Unadhani private sector ikisema hizo elfu kadhaa hazitoshi sisi na shareholder wetu kugawana faida nani atalipia difference kama sio sisi through kodi zetu ?

Au unadhani kwanini hata nje (UK for example) Privatization ya Rail ime-prove hard to implement na mpaka routes nyingine kuwa re-nationalized ?

Au unadhani Private company ikiona safari ya morogoro jumatatu faida yake ni ndogo kuweza kugawa na shareholders wetu bado watakwenda huko , au watapiga hodi serikalini kwamba gharama ya safari za jtatu nyie ndio mlipie ?
 
View attachment 2440365
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.

Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.
Hata watete hawatapata abiria,, nauli lazima iwe chini ya nauli ya mabasi
 
Uwekezaji ni long term kuna watu wanawekeza ku-break even ni after 200 years au generation...., Uendeshaji ndio ninakuuliza Je watu wakiwa wengi gharama za uendeshaji kati ya train na basi ipi ni nafuu ?

Unajua kwa mizigo kutumia train tunaokoa kiasi gani katika maintanance ya barabara ?, unajua mtu kuja na kapu lake la machungwa Dar kwa bei nafuu au kuleta mchele kwa bei nafuu itapelekea wewe kuweza kupata bei nafuu ?

Hivi ingekuwa pesa tu ndio kila kitu kwanini hata DAWASA au TANESCO wasingechaji maji hata mara nne ya bei ya sasa kama issue ni kupata as much as possible moneywise ? Au ndio ile Unajiibia mwenyewe mfuko wa shati unaweka mfuko wa suruali....

Unadhani private sector ikisema hizo elfu kadhaa hazitoshi sisi na shareholder wetu kugawana faida nani atalipia difference kama sio sisi through kodi zetu ?

Au unadhani kwanini hata nje (UK for example) Privatization ya Rail ime-prove hard to implement na mpaka routes nyingine kuwa re-nationalized ?

Au unadhani Private company ikiona safari ya morogoro jumatatu faida yake ni ndogo kuweza kugawa na shareholders wetu bado watakwenda huko , au watapiga hodi serikalini kwamba gharama ya safari za jtatu nyie ndio mlipie ?
Wampe azam,, maana bila hivyo watu watapiga pesa sanasana
 
Wampe azam,, maana bila hivyo watu watapiga pesa sanasana
Kwanini Azam asijenge yake ashindane na hii ? Au alete mabehewa yake na train yake alipie matumizi ya reli...

Am all for Free Trade and Minimum (if possible) non government interference...
 
Na ndio maana wamewaletea za kuendana na maisha yenu ya kulia.lia
kulia lia!! Ina maana huelewi usafir wa tren unatakiwa uwe ngarama nafuu au bure. Kwa nchi ambayo haina mikakati hata umeme wa kuchaji simu ni shidah, bwawa la nyerere limefanywa mtaji, kwaiyo unataka umeme wa kuzungusha rim za tren walipe wana inchi 100%😂😂😂 huoni ni vituko hivi mbaya zaid na umeme wenyewe haupo
 
View attachment 2440365
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.

Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.
Nauli za mabasi zitapanda zikaribiane na za SGR. Ili iwe rahisi kuchagua SGR
 
Hiyo ni bei ya nauli walizopendekeza wao trc then latra watakusanya maoni ya wadau ili wacrosscheck pande zote kupata bei sahihi ya mlaji. Kama mlaji napendekeza nauli ya dar moro iwe 6000
Sasa taarifa imetolewa na LATRA alafu unasema watatoa taarifa tena? Ni taarifa ipi hyo?
 
View attachment 2440365
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.

Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.
1. Kwa kuanzia wa round off hizo hela mfano; 394 iwe 400; 353 iwe 350 nk
Wasitengeneze gap la kutoa usumbufu kwa abiria na mwishowe kutengeneza hela isiyokuwa na mwenyewe
2. Waingie sokoni kwa ajili ya kurahisisha usafiri na kupunguza gharama kwa abiria; Nafikiri ndio yalikuwa mawazo ya msingi ya kuanzisha hiyo huduma
3. Pendekezo jipya;
Wangeweka treni ya Abiria kutoka Arusha saa mbili usiku (20h00) na kufika Dar saa kumi na mbili asubuhi; Waache kujipangia muda usioendana na matakwa ya Abiria. Hilo la mchana litabakia la x-mass
 
Unalipia kufika mapema au gharama halisi za kusafirishwa? Na mabasi yakiwahi kufika Moro wawatake abiria kuongeza nauli, kama 10,000/= waongeze shs 2,000/=.
Gharama halisi ni nini? Nikuulize ukipanda ndege kwenda mwanza na mimi nikapanda basi kwenda mwanza wewe utatumia masaa 2 hadi matatu .mimi nitatumia masaa siyo chini ya kumi na tano . Unadhani nauli zitafanana?
 
Sasa taarifa imetolewa na LATRA alafu unasema watatoa taarifa tena? Ni taarifa ipi hyo?
Mkuu hizo bei ni mapendekezo tu, bei halisi itatolewa baada ya kukusanywa kwa maoni ya wadau na kuyafanyia kazi
 
Tunarudi kule kule swali dogo majibu lukuki / nje ya point ?, Kwahio unakubali kwa utilities na Public transport ni huduma ? (Ndio au Hapana) ?
Kwani mjadala ilikuwa ni endapo sekta husika ni huduma ama sio huduma?!

Hoja hapa sio kama sekta husika ni huduma ama sio huduma bali ikiwa sekta husika inaendeshwa kibiashara au "kiujamaa"!!

Hata mtoto wa Darasa la IV anafahamu kwamba maji, usafirishaji, umeme, mawasiliano, and the like... zote hizo ni huduma lakini je, taasisi zake zinaendeshwaje au zinatakiwa kuendeshwaje!

Mifano ipo wazi lakini bado unaganda kwenye hiii huduma... SAWA, HUDUMA lakini wenzako hawaendeshi hizo taasisi kama unavyotarajia wewe!

Nani asiyefahamu umuhimu wa usafiri Dar es salaam! Je, ile Mwendokasi sio huduma ile?! Nauli zake ni ndogo compared to Daladala?!

Hiyo ndo reality ninayokuambia kila wakati!

Hivi unataka kuniambia Nauli ya Daladala Dar es salaam ni kubwa kuliko Mwendo Kasi?

Kama hoja yako ya huduma ingekuwa inatiliwa maanani, what would you expect kati ya nauli za Daladala vs Mwendokasi?
Pili kwako wewe at what cost inabadilika kutoka kuwa huduma ?
Kubadilika kivipi?!

Huduma ni huduma tu at any cost lakini huduma haimaanishi utalipishwa bei ndogo! Na hata kama inatakiwa ulipishwe bei ndogo, uhalisia haupo hivyo na ndo maana nikakupa mifano ya huduma zingine ambazo bado unalipishwa bei zinazolalamikiwa na wananchi!

Kwangu Mimi: jibu ni the lowest price possible na hii price tutajua iwapo tukishajua production costs na kipato cha mpewa huduma (ndio maana nchi zote serikali inatoa ruzuku kwenye huduma kama hizi iwapo bei itakuwa sio rafiki kwa mwananchi wa kawaida) sababu kama ferry kuvuka mtu kuja kuzalisha ni shida impact yake kwa nchi ni astronomical kwa uchumi.., Pia hizo ruzuku ndio kodi zetu zinatoka hapa na pale...
Hivyo ndo kwako wewe... FINE, sina tatizo na hilo!

The question is: UHALISIA kwa zile huduma zingine upo hivyo unavyojua wewe?

Hata ukiwauliza serikali, watakujibu kama unavyojua wewe, na watakuambia na hiyo ruzuku wanatoa ndo maana pricing ipo kama ilivyo.
Sasa kama Realistically Prices zinakuwa-inflated, uendeshaji mbovu, wizi na walamba asali kuiba.... Ni busara kusema kwamba hii ndio reality na tuiweke katika equation kwamba how things should be ?
How should be?! Sizungumzii "how should be" nazungumzia uhalisia uliopo!

Wewe unataka nifanye janja ya mbuni kana kwamba uhalisia siuoni bali nizungumzie "how should be"!!
(Yaani hakuna alternative) ?

There was a time Utumwa ulikuwa ndio way of life (reality) sasa watu ambao walisema / waliona kwamba utumwa haufai na unaweza kubadilika walikuwa wanaishi kwenye fantasy World ?
Mfano wako wala haufanani...

Nakuambia unaishi kwenye fantansy world kwa sababu uhalisia unauona lakini unajifanya huuoni!!

Unaona hapo nauli to Morogoro 24K... twice as much-- na huo ndo uhalisia wenyewe na sio "how should be"

Na hata wakisema washushe, maybe to 10K... je, itakuwa imekidhi tafsiri yako ya huduma?!
 
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.

Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.

--

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu nauli za abiria kwa treni ya njia ya Reli ya Kisasa – ‘Standard Gauge Railway’ (SGR) zitakavyotumika kwa huduma ya usafiri wa treni za abiria.

Kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria Na. 3 ya LATRA, 2019 Mamlaka inapaswa kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwemo nauli za treni.

Katika kulitekeleza hilo, Mamlaka imeandaa mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa usafirishaji, ikiwa ni pamoja na watoa huduma, watumiaji wa huduma na wananchi kwa ujumla. Mkutano utafanyika tarehe 19 Disemba 2022 jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Anatorglo.

Nauli zinazopendekezwa na TRC ni Kama ifatavyo:

View attachment 2440636

View attachment 2440637

Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, LATRA inawaalika wadau wa sekta ya reli na wananchi kwa ujumla kushiriki katika mkutano huo wa kukusanya maoni ya wadau.

Vilevile, wadau wanaweza kuwasilisha maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu kwa maandishi kupitia LATRA Makao Makuu, Mtaa wa Tambuka Reli, Dodoma au ofisi za LATRA zilizopo Makao Makuu ya kila mkoa Tanzania Bara kabla ya tarehe 3 Januari 2023.

Aidha, maoni ya wadau yanaweza kutumwa kwa barua pepe kupitia anuani hizi: info@latra.go.tz na dg@latra.go.tz

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano – LATRA
06 Disemba, 2022​
WAMILIKI WA MABASI MIONGONI MWAO NI WATU WENYE MAMLAKA.

TUNALINDA MASLAHI YA BIASHARA ZETU ZA MABASI.

NA KWA HILI MMEFANIKIWA.
 
kulia lia!! Ina maana huelewi usafir wa tren unatakiwa uwe ngarama nafuu au bure. Kwa nchi ambayo haina mikakati hata umeme wa kuchaji simu ni shidah, bwawa la nyerere limefanywa mtaji, kwaiyo unataka umeme wa kuzungusha rim za tren walipe wana inchi 100%😂😂😂 huoni ni vituko hivi mbaya zaid na umeme wenyewe haupo
Wapi ambako treni Ina gharama nafuu? Tuwekee ushahidi hapa..

Kama mlijua hamna umeme na mva vipaombele vingine vya maana kwa Nini kukimbilia sgr wakati hamna uwezo nayo? Huu so upimbi huu?
 
Back
Top Bottom