Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Una uhakika na ulichokiandika? Do simple research pls. Usafiri wa train ndio very chip duniani na ndio unapendwa na wengi. Usijaribu kutudanganya. Mradi wenyewe tulipigwa, haikutakiwa kujengwa kwa trillioni saba na ushee. Kwenye vichwa napo tumeletewa vibelenge (huyu anasema vibelenge vipya yule anasema vibelenge vilivyofufuliwa (used) tena kwa kusisitiza kwamba lazima aseme ukweli). Tumwamini nani kwenye hizi kauli kinzani?? Aya forget about that, kwenye nauli wanapendekeza hizi nauli za kimchongo ili magari yao yaendelee kutembelea barabarani. Are these people really serious? Hope hawa wanaishi ile Tanzania ya uchumi wa kati.
Tuwekee Bei za huko kwingine sio kubwabwaja bila ushahidi..
 
Tazara Ina nauli ndogo Ila mabus na malori yako njiani..

Sgr haikujengwa Kuondoa mabasi Bali ku compliment usafiri mwingine
 
Unataka chap chap vya haraka afu hutaki kitoa Pesa ya haraka? Panda bus..
Hujui kwamba Pesa yako hapo umeshatoa kwenye kulipa Mikopo na utaendelea kutoa kwenye maintanance ya barabara kama alternative SGR isipokuwepo ?
Uliwahi ona ndege Ina nauli ya chini?
Unajua kitu kinaitwa budget airlines (ingawa this is beside the point)...
Boti za fast ferries Zina nauli ndogo?
Demand and Supply na Operation costs ila ukifahamu kwamba the only time train inakuwa cheaper than alternative ni pale wateja wanapozidi nadhani ungebadilisha hii kauli..., train watu wakizini unaongeza behewa sidhani kama fast ferries unaweza ukafanya hivyo...
Barabara za express way ndio maana zinalipiwa huwezi komaa kwenye km 80km/hr..
Na kama hakuna mtu anapitia huko bei haitashuka kulingana na wingi ?
Hamtaki hizo Bei hiyo sgr itakuwa tembo mweupe na italeta hasara Kama atcl na buses za Dart.
Kwahio hasara hizi zimetokana na bei na sio uendeshaji wala mirija ya walaji ?.., kwamba bei kubwa watu wasipande ndio italeta faida, kuliko bei ya kawaida na watu wapande ? Kwamba wakati wa UDA ipo one peak waliwezaje ? au gharama ilikuwaje kulinganisha na kipato cha mtu ?
 
Sasa mtu awaze kuhusu mabasi wakati Ni suala la kuhamisha route tuu?
So mtu aliekua ana mabasi nane ya kwenda route ya dodoma atayapeleka route ya mbeya. Na ya mbeya nayo yatakuwepo hapo watabanana wenyewe na wateja. Mind you, ile mikoa watu wanaenda kwa issue maalumu tofauti na dodoma tangu mji uhamie huko, movements zimekua nyingi sana. Unless kama wewe ni mmliki wa mabasi au unafanya biashara ya mabasi una uzoefu nayo basi huwezi kuelewa namaanisha nini.
 
Hivi unajua hata maana ya huduma ni nini ? Hebu nipe definition ya Huduma
Yaani tatizo lako BADO LILE LILE!

Narudia, angalia REALITY ON THE GROUND na sio mambo ya "what ought to be"!

Zamani kuvuka to/from Kigamboni ilikuwa TZS 100/= baada ya kununuliwa kivuko kipya nauli ikapanda to 200/= na wakaambiwa wasiokuwa na 200/= wapige mbizi...

Je, kile Kivuko hakikuwa huduma ile?

What happened baada ya kufunguliwa Daraja la Kigamboni!

Unajua magari yanatakiwa kulipa shilingi ngapi pale?

Sio huduma ile?

Na baada ya watu kulalamika kuhusu tozo kubwa kupita pale darajani, walijibiwa nini?!
Kwahio sababu reality watu ni wezi na wapigaji ni kwamba ni sawa na hakuna alternative ?..., Kwahio sababu Utumwa ulikuwa jambo la kawaida wakati ule ile ndio ilikuwa the way to go....
You've a very long way to go!

From economic theories, YOU'RE RIGHT, especially kwenye hili la reli lakini mimi najikita kwenye uhalisia!!

Kwani kuna mtu asiyetaka umeme wa Sh 50/Unit?!

Sasa hapa ndo watu tunaongea uhalisia kwa kuangalia huko tulikotoka!

Hata wakati Gesi ya Songosongo inaletwa Dar tuliambiwa bei ya umeme itashuka!

Sasa watu tukikuambia reality on the ground wewe bado unajikita kwenye theories!
Kama hatujengi Hoja kwa the best case scenario sasa tunafanya nini si tuache kujadili ideas na tuendelee kujadili issues and people......

Au unadhani mimi ni reporter and am reporting what is happening....
Nimesema yote...
 
Ili itete faida italazimu mabasi yasitishwe!, na nauli washushe.
N. B, priority ya mradi huu ibidishwe Kigoma na mwanza.
Nilikwambia hii mradi Ni tembo mweupe na itakuwa hivyo..

MGR ulivyokuwa inasumbua na hii sgr itakuwa Mara 2.

Unataka starehe wakati huna uwezo? Treni sio kipaombele Cha maskini Bali watu wa kipato Cha Kati ambao Tanzania Ni wa kutafuta kwa tochi..
 
Hizo rush hours, huku ni critical. Na almost throughout the day. Hakuna AC. Muda wa kufika haueleweki. Ukifika uendako, nguo zimejikunja na unanuka jasho. Hii sio kawaida. Tusizoee shida
Nenda China afu uulizie AC
 
Wakati ulipoanza mjadala wa High Speed Train, niliuliza hapa hivi zikizeletwa hizo high speed trains kama mnazoziona kwenye tv, mtaweza nauli zake!!
Mburula na manyumbu walikuwa wanashangilia tuu 😁😁.

Mimi.nilipinga directly kujenga sgr kupeleka Mwanza ambako Hakuna hata mzigo..

Walikuwa wanasema ooh gharama za mizigo zitashuka Sasa ngoja tusubirie nazo zishuke 😆😆
 
Bora kuyatesa makalio kwa masaa 4 kwenye abood kwa sh 10000 kuliko makalio kupata raha kwa saa moja kwa sh 24000 au 29000 kwenye behewa
 
Mkuu nenda na kwenye mabasi check zile free riders zilikuwaje. P

Pamoja na kuwa ni huduma baadhi ya maeneo lakini nauli ni kubwa kuliko mabasi na serikali inatoa ruzuku. Mkuu kwenye hii bei, na uwekezaji haviendani. Serikali itatoa ruzuku. Lakini vyovyote vile treni lazima iwe ghali kulipia hizi trillioni. Vinginevyo, tutazalisha kila siku ili tulipie deni la SGR
Kutakuwa hakuna maana Kama utachaji nauli ambayo haifikii hata robo ya gharama za uendeshaji na uwekezaji..

Sasa tulijenga Cha Nini Kama tutakuwa tunatumia Kodi ya Nchi kuendeshea sgr? Huu si Ni upumbavu?

Na hapa Sasa ndio huwa inakuja Ile maana ya private sector kujenga na kuendeshwa wenyewe.
 
Yaani tatizo lako BADO LILE LILE!

Narudia, angalia REALITY ON THE GROUND na sio mambo ya "what ought to be"!

Zamani kuvuka to/from Kigamboni ilikuwa TZS 100/= baada ya kununuliwa kivuko kipya nauli ikapanda to 200/= na wakaambiwa wasiokuwa na 200/= wapige mbizi...

Je, kile Kivuko hakikuwa huduma ile?

What happened baada ya kufunguliwa Daraja la Kigamboni!

Unajua magari yanatakiwa kulipa shilingi ngapi pale?

Sio huduma ile?

Na baada ya watu kulalamika kuhusu tozo kubwa kupita pale darajani, walijibiwa nini?!

You've a very long way to go!

Kwani kuna mtu asiyetaka umeme wa Sh 50/Unit?!

Sasa hapa ndo watu tunaongea uhalisia kwa kuangalia huko tulikotoka!

Hata wakati Gesi ya Songosongo inaletwa Dar tuliambiwa bei ya umeme itashuka!

Sasa watu tukikuambia reality on the ground wewe bado unajikita kwenye theories!

Nimesema yote...
Tunarudi kule kule swali dogo majibu lukuki / nje ya point ?, Kwahio unakubali kwa utilities na Public transport ni huduma ? (Ndio au Hapana) ?

Pili kwako wewe at what cost inabadilika kutoka kuwa huduma ?

Kwangu Mimi: jibu ni the lowest price possible na hii price tutajua iwapo tukishajua production costs na kipato cha mpewa huduma (ndio maana nchi zote serikali inatoa ruzuku kwenye huduma kama hizi iwapo bei itakuwa sio rafiki kwa mwananchi wa kawaida) sababu kama ferry kuvuka mtu kuja kuzalisha ni shida impact yake kwa nchi ni astronomical kwa uchumi.., Pia hizo ruzuku ndio kodi zetu zinatoka hapa na pale...

Sasa kama Realistically Prices zinakuwa-inflated, uendeshaji mbovu, wizi na walamba asali kuiba.... Ni busara kusema kwamba hii ndio reality na tuiweke katika equation kwamba how things should be ? (Yaani hakuna alternative) ?

There was a time Utumwa ulikuwa ndio way of life (reality) sasa watu ambao walisema / waliona kwamba utumwa haufai na unaweza kubadilika walikuwa wanaishi kwenye fantasy World ?
 
Kwani ule umeme wa kuendesha hizo treni atakuwa analipia nani?
 
Back
Top Bottom